Kutengeneza bisi (pocorn)kwa mashine

Kutengeneza bisi (pocorn)kwa mashine

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
5,707
Reaction score
7,384
Najaribu kutengeneza bisi kwa popcorn mashine lakini sifanikiwi nyingi zinauungua tu,naweka mafuta kwenye kichombo,yakichemka naweka bisi,sasa shida ni kwamba chache zinapasuka vizuri ila. nyingi zinaungua.Naomba mwenye ufahamu juu ya hizi mashine zinavyofanya kazi anifundishe nifanyeje.Ni zile mashine kubwa ambazo hutumiwa na wafanyabiashara wa popcorn hii yangu ni mr uk
 
Kama ukishindwa mahali nishtue hapa, nimeifanya hii kazi japo ni muda kidogo lakini naamini nitakumbuka zinavyo pikwa kwa mashine.
sawa shida yangu kubwa ni kwanini,nikiweka bisi nyingi zinaungua na hazipasuki,ndio naangalia huko utube,naona vitu vingi mno lakini bado sijaweza kujua ni kwanini,bisi ningi huungua tu na pili je nitumie blueband au mafuta? je niache dk ngapi mafuta yachemke kabla ya kuweka bisi?
 
sawa shida yangu kubwa ni kwanini,nikiweka bisi nyingi zinaungua na hazipasuki,
Sawa mkuu nitakujibu swali moja moja, ni hivi..

zinaungua na hhazipasuki kwa wingi kwasababu moja kati ya hizi ama zote kwa pamoja:

1. Unaweka mahindi mengi kwenye sufuria.

2. Unaweka mafuta kidogo sana kwenye sufuria.
 
Mahindi naweka saizi ya kikombe kidogo cha chai,mafuta nimeka,nilijatibu kuweka kidogo,yakaungia,nikafanya tena nikaweka mengi bado yakaungua hivyohivyo
 
je nitumie blueband au mafuta?
Nakushauri tumia mafuta kwa sababu:

1. Mimi nilikuwa natumia mafuta.

2. Sehemu zote ambazo nimewahi kuona popcorn zikichomwa ni kwa kutumia mafuta.

3. Sijawahi kuona Kusikia wala kusoma mahali kwamba blueband hutumika katika kuchoma popcorn.
 
Mahindi naweka saizi ya kikombe kidogo cha chai,mafuta nimeka,nilijatibu kuweka kidogo,yakaungia,nikafanya tena nikaweka mengi bado yakaungua hivyohivyo
Punguza mkuu weka nusu kikombe mahindi uone matokeo yake, kisha ukishakuwa mzoefu wa mashine hata hiko kikombe kidogo cha chai unachoma vizuri tu. Hizo bisi nyeupe ni rahisi mno kuzichoma.
 
nyeupe tu
😆😆😆 mkuu bisi nyeupe ni rahisi mno kuzichoma, mimi naweza kuzichoma hata ikiwa nimefumba macho.

Shughuli ni bisi za rangi, wakati najifunza niliwahi kuziunguza zinafika hata beseni mbili wanakijiji walikuwa wanashangilia tu, maana walikaa hapo hapo kwenye mashine zikitoka zimeungua wanazizoa na kuzila, nilipata hasira hadi nikatamani kuachana kabisa na hizo bisi za rangi.
 
Sasa mimi zinashinda nyeupe ila natengeza kwa ajili kula tu hapa nyumbani
 
Sasa mimi zinashinda nyeupe ila natengeza kwa ajili kula tu hapa nyumbani
Kumbe sio za biashara, halafu sasa ukiweka mafuta mengi halafu mahindi yakawa kidogo sana, kitakacho tokea ni kwamba mahindi yatapasuka na kuruka ila zile za mwisho ambazo hubaki kwenye sufuria hadi uzimimine, zitakuwa na mafuta mengi kiasi cha kutokupendeza kuliwa. Ila ikiwa ni za biashara haiwi shida kwa sababu huchomwa kwa wingi hivyo zenye makosa hupotelea kwenye nyingi nzuri.
 
Nasoma sasa kesho ntajaribu tena kwa kufuata maoni niliyopata na nitarejesha mrejesho hapa
 
Back
Top Bottom