Kutapeliwa

Kutapeliwa

Wakuu habari yenu, jana kuna kitu nlimuuzia jamaa fulani hv. Yeye alisema yuko mkoani, so ikabidi tufanye arrangements ili tukutane na ndugu yake alieko Dar uko, ili nimpe mzigo wake.

Baada ya yule ndugu yake kuuona na kuridhika, ikabidi ampigie mteja wangu kwamba mzigo uko vizuri. Nikawa nimeongea nae akasema atanitumia kwenye number ya airtel iko kiasi tulichokua tumekubaliana. Kwa kua mimi sina number ya airtel ikabidi nimwambie rafiki yangu kuwa kuna muamala utatumiwa kwenye simu yake maana yeye ana line ya airtel.

Basi, kama baada ya dakika nane yule rafiki yangu anaetumia line ya Airtel akanambia ameona pesa imeingia kutokea NMB. Mimi nikasema sawa, nikamkabidhi yule ndugu yake mzigo tukaachama pale.

Ile message inaonekana imetokea NMB, kwamba katumia huduma ile ya benki mkononi kunitumia hela. Basi, kwa kua ilikua ni jioni sana hata mabenki yalikua yamefungwa nikasema asubuhi ya leo nitawahi bank nikaihangaikie. Cha ajabu nafika bank wananiambia hakuna muamala wa dzain hiyo kwa benki yao. Sikukata tamaa ikabidi niwacheki pia kwa mitandao yao ya kijamii (instagram) ila majibu yakawa ni yale yale.

Mteja wangu nliefanya naye biashara, wakati niko bank nilikuwa najaribu kumpigia ila hakupatikana, ila dakika 20 kabla ya kuanza kuandika huu uzi nlijaribu kumpigia akasema ngoja amcheki wakala ambae alimtumia kunitumia hiyo hela. Ndo niko namskilizia hapa.

Naombeni ushauri kama kuna mtu anaweza kuwa na idea na hiki kitu au anaeweza kuwa na wazo lingine anisaidie wakubwa.

Natanguliza shukrani.

View attachment 1488552View attachment 1488553
Nitumie Hyo screenshot kwa wasap 0683226931.
 
Mkuu pole sana umeshapigwa hela hapo,daah nilipigwa lake 3,nikaona nyingi kwa mtindo huo kumbe kuna watu wanapigwa mpk milioni.kua makini siku nyingine mkuu. Matapeli mjini ni wengi na husiamini mtu siku hizi
ulipigwa kwa mtindo huu huu kama wa mtoa maada?
 
Mkuu pole hapo umepigwa. Wametumia bulk SMS na kwenye jina la sender wameweka (NMB.)
Next time hakikisha salio linasoma ndo utoe bidhaa. Yaani kufanya hivyo naandika script ya mistari michache sana ya Python + Bulk SMS API yoyote faster kitu kinatumwa
vipi umeshawahi kupigwa nini?
 
Asante kwa kutambua ujinga wangu Kuhusu kumpa account, Soma vizuri tena boss. Ilikua jioni, so banks pia zilikua zishafungwa. Na pia nisingekubali aje akanitumie labda kesho yake. Ingekua ngumu ndugu yangu
Kwani kutumiwa kwenye ac hadi mtu aende bank? Si anatumia sim banking!!
 
Ngoja nikusaidie kidogo ndugu yangu..

Kuna kampuni nyingi sana zikiwemo za nje ya nchi zina huduma ya bulk sms. Kumbuka pia hii huduma inakupa option ya kutuma sms kwa mtu mmoja mmoja kwa kutumia id ya sender name yako

Mimi pia nina hiyo huduma, hichi nikwambiacho ndicho...

Kilichofanyika, huyo Jamaa ana hiyo huduma, sasa hizo huduma zina option ya kusajili sender name kwa namba uitakayo.

Mitandao mingi wapo very restricted kwenye usajili wa sender name, isipokuwa Airtel pekee.. hata mimi nime sajili sender name ya business name yangu via Airtel.

So, huyu jamaa na yeye amesajili sender name kwa kutumia namba ya Airtel. Ili kuepusha mfanano na NMB original, ameamua kuongeza hiyo nukta hapo.

Nahisi umepata picha nini kimetokea..
 
Yaani akutumie pesa kwenye namba ya simu ila pesa ukachukulie bank!!! Kuna huduma ya hivyo kweli?

Pole we!
Hiyo huduma ya Jamaa ambayo kimsingi ni kama geresha ina shabihina na huduma ya "NMB CARDLESS" ambapo pesa unaenda kutoa moja kwa moja toka ATM kwa kuingiza namba ya aliyekutumia, hizo code kisha kiasi.

Sasa hatari yake, kama huo muamala uko valid, watu wameshachomoa pesa, maana Jamaa ka expose kila kitu..
 
Hawa jamaa....kuna dada yangu nae walimtumia sms kama hiyo ya shs 1,400,000/=...aka n forwadia niicheki kama n pesa kweli ili ampatie mteja wake mzigo wa simu ilikuwa mida ya usiku...nilivyo icheki nikamwambia chonde chonde usitoe mzigo mpaka ufike bank kesho asubuhi...kufika bank asubuh kaambiwa amna muamala kama huo ndo ikawa pona yake.
 
Asante ndugu, Na mimi pia ndo wasiwasi wangu ukianzia hapo. Nilijaribu kuangalia hata message za tigo pesa ila sikuona hiyo nukta kwa mbele. Ikaniongezea mashaka zaidi

Duuuuh na nyakatiii hizi ? Pole sana
 
Ngoja nikusaidie kidogo ndugu yangu..

Kuna kampuni nyingi sana zikiwemo za nje ya nchi zina huduma ya bulk sms.

Mimi pia nina hiyo huduma, hichi nikwambiacho ndicho...

Kilichofanyika, huyo Jamaa ana hiyo huduma, sasa hizo huduma zina option ya kusajili sender name kwa namba uitakayo.

Mitandao mingi wapo very restricted kwenye usajili wa sender name, isipokuwa Airtel pekee.. hata mimi nime sajili sender name ya business name yangu via Airtel.

So, huyu jamaa na yeye amesajili sender name kwa kutumia namba ya Airtel. Ili kuepusha mfanano na NMB original, ameamua kuongeza hiyo nukta hapo.

Nahisi umepata picha ninu kimetokea..

Daaaaaaaaah
 
Muombe sana MUNGU usije fanya maamuzi
Magumu.
Pesa zinatafutwa..
Umejifunza naamini..
Maduka makubwa yote kule kariakoo kama sio mteja wao hawataki ulipe kwa tigo pesa n.k
Wanakwambia lipia BENKI au uje na cash.
siku hizi binadamu ana akili sana kumshinda nyuki.
 
Pole sana ndugu. Kwa mada yako nimejifunza kitu. Hiyo mbinu kama ni mara ya kwanza lazma upigwe.
 
Kila kukicha wajinga wanazaliwa.

............pesa ndefu kama hiyo kwanini hukumpa akaunti namba akadeposit huko?
Braza hamna ujinga hapo...hiyo sms ukikutana nayo mara ya kwanza lazima uingiee mkenge.
 
Hiyo huduma ya Jamaa ambayo kimsingi ni kama geresha ina shabihina na huduma ya "NMB CARDLESS" ambapo pesa unaenda kutoa moja kwa moja toka ATM kwa kuingiza namba ya aliyekutumia, hizo code kisha kiasi.

Sasa hatari yake, kama huo muamala uko valid, watu wameshachomoa pesa, maana Jamaa ka expose kila kitu..
Oooh!! Kumbe kuna huduma ya hivyo!
 
Pole sana mkuu ni juzi tu km wiki tena tapeli huyo kaona bidhaa humu JF nilipost uzi huu
hapaComputer4Sale - HP probook 8 GB ram laptop inauzwa bei poa
nauza laptop akataka nikutane na jamaa yake SINZA KIJIWENI yeye yupo mkoani ARUSHA
Hivyo kwa uzi wako sasa nimeelewa nini kilitaka kunitokea na kipi kilichoniokoa
Akasema anatuma pesa toka bank akang'ang'ania sana Atume aitel 7bu alijua me sina laini hiyo sikutaka mabishano sana fresh nikamtumia namba ya jamaa yangu baada kufanya miamala akasema ishatumwa fresh
Kumuuliza jamaa yangu kasema imeingia pesa toka NMB 255000/=
sasa mm huwa na kawaida 1 nikifanya biashara mtandaoni na mtu hata kama tupo pamoja ukinitumia pesa km malipo hiyo pesa papo hapo kabla sijakukabidhi mali nami lazima niamishe kwenye namba nyingne tena huu utaratibu nautumia miaka mingi sana kabla hata huu utaratibu wa kutuma mitandao mingne haujaanza

nikamuambia jamaa yangu nitumie hiyo pesa kwenye namba yangu jamaa akituma anaambiwa salio halitoshi kila akipunguza wapi ikabidi acheck salio akakuta ipo pesa yake tu haijaongezeka
Nikamuambia pesa huyu jamaa ambaye anakagua mzigo nimkabidhi yeye amtumie jamaa yake pesa haijaingia kwenye AIRTEL MONAYE

Akampigia jamaa yake wakaongea kisha akanigeukia akaniambia jamaa katuma pesa ila NMB wameuishikilia hivyo hiyo Biashara tutafanya kesho atanitumia mm nitakupa CASH akadai km itaingia nimjulishe pia nifanye uungwana
Nikasema poa lkn hiyo kesho mpk sasa wiki na nusu hawajanitafuta na namba zao hazipatikani wote
 
Back
Top Bottom