Uchaguzi 2020 Kutangaza maandamano pekee hakutoshi, kunahitaji maandalizi. Tujiulize kwanini maandamano ya Seif Zanzibar hayakufanikiwa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,272
Kuandaa maandamano ni fani kunahitaji mipango madhubuti, hata kama una ajenda muhimu huwezi kukurupuka na kutangaza leo au kesho kuna maandamano, Seif alikuwa na ajenda lakini hakuwa na mipango madhubuti aliongozwa na mihemuko, hasira na jazba.

Wataalamu wa mipango ya maandamano wanasema ili maandamano yafanikiwe kuna hatua muhimu lazima zizingatiwe.

  1. Lazima kuwe na sababu (issue) inayogusa jamii. Unaweza kutangaza maandamano ukakuta watu hawana interest nayo.
  2. Chagua ‘theme’ kauli mbiu itakayokuwa common kwa wote itakayotoa hamasa mfano, uonevu sasa basi au wimbo wa ujasiri.
  3. Toa taarifa kwa taasisi za misaada kama Red Cross na andaa utaratibu wa misaada ya haraka kwa waandamanaji watakaozidiwa wakati wa maandamano mfano maji na huduma ya kwanza.
  4. Tayarisha eneo mwafaka destination la kutolea matamko yako (open space, ofisi za serikali, nk) usitoe matamko ofisini kwako.
  5. Alika ‘known public speakers’ watakaotoa hotuba fupi fupi zisizochosha mfano viongozi wa dini, wasanii nk.
  6. Andaa mziki na wasanii watakaoburudisha.
  7. Andaa shelters mahema, jukwaa kama kuna ulazima.
  8. Andaa mabango yenye kuvutia na kufikisha ujumbe mfupi (inclusive) usibague kundi lolote la jamii.
  9. Kama lazima pata vibali au toa taarifa kwa mamlaka husika.
  10. Alika vyombo vya habari vya ndani na vya nje ikiwezekana vipe taarifa mapema kwa simu ama maandishi, email nk.
  11. Tumia mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram, You Tube nk kuhamasisha watu.
  12. Ijulishe jamii ya kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na marafiki kusudio lako la kufanya maandamano ya amani ukinukuu vifungu vya sheria vinavyo kusapoti.
  13. Mwisho kabisa hakikisha wafuasi na waandamanaji hawavunji sheria wala kufanya fujo.
 
Lengo huenda lilikuwa zuri ila organisation hakuna na hiyo Jumatatu most likely kusitokee kitu

46AD3BC5-4AF8-4E9E-B705-47741824CE14.jpeg

Maandamano kwenye kata yataelekea ofisi za wasimamizi wa Uchaguzi kutokea wapi? Nani anaongoza? Saa ngapi? Waandamanaji wakifika huko wanapaswa kufanya nini?

Siera Leone upinzani walikinukisha siku 7 kabla ya uchaguzi na kura zimepigwa leo. Incumbent President keshaanza kuomba poo na huenda asiibe sana
 
Hizo ni gharama kubwa kuliko za kuweka mawakala vituoni.

Ili yafanikiwe inabidi yaanzie kusini usiku.
 
Back
Top Bottom