Ushauri kuelekea tamasha kubwa kabisa nchini SIMBA DAY August 6 Mambo ya Muhimu kuzingatia

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
Tamasha bora la mpira wa miguu kuelekea msimu mpya linapaswa kuwa tukio la kusisimua na la kuvutia kwa mashabiki wa mpira wa miguu na ambao si mashabiki wa mpira wa Miguu kuvutika na kuwa WANACHAMA na wapenzi WA TIMU husika simba

. Hapa kuna mambo kadhaa yanayoweza kufanywa ili kufanikisha tamasha kuwa Bora zaidi Katika siku ya Simba Day.

1. Tamasha linatakiwa liwe na viingolio Rafiki kwa watazamaji.
Kujua uwezo WA watazamaji kiuchumi kunaweza kusaidia ubora wa Tamasha.
Wepesi WA kuingia Viwanjani.
KUEPUKA misusururu na mistari mirefu.

2. Kuwa na washehereheshaji wenye UWEZO Mkubwa na mzuri WA KUTANGAZA kwa Lugha ya kiingereza, kifaransa na kiingeleza.
Sio Kila MC Kutaka kushika Mike HASWA wakati WA UTAMBULISHO WA wachezaji.

3 . Usanifu wa Tamasha: Tamasha linapaswa kuwa na usanifu mzuri na mipango madhubuti ili kuhakikisha kuwa linawavutia na kuwaburudisha mashabiki a)michezo ya burudani,
b) WASANII WAKUBWA WA MUZIKI.
c) wacheza shoo wazuri, na d)maonyesho ya sarakasi,
e)farasi
f) NGOMA nk

4 . Kuialika Timu nzuri Katika siku ya tamasha, Timu yenye Ushindani Mzuri : Kuandaa mechi za kirafiki kati ya timu maarufu na zenye ushindani ni njia nzuri ya kuanza msimu mpya. Mechi hizi zinavutia mashabiki na pia hutoa fursa kwa timu kujiandaa kwa msimu ujao.

5 . Uwepo wa makampuni ya vinywaji na chakula.
CLABU kuingia ubia na makampuni kama COCACOLA, TBL, ENEGY, AZAM NK.
Kuweza kuuza ndani ya Tamasha kwa UTARATIBU maalum

6 . Mipango ya Soka la vijana
Soka: Kuandaa academy za soka kwa vijana ni njia nzuri ya kukuza vipaji na kujenga hamasa miongoni mwa wachezaji chipukizi.hizi zinaweza kuhusisha wachezaji na makocha maarufu ambao wanaweza kutoa mafunzo na ushauri kwa vijana.

7 . Mikataba na Wadhamini: Kuvutia wadhamini na kampuni za kimataifa kunaweza kusaidia katika kufadhili tamasha hilo na kuboresha ubora wake. Wadhamini wanaweza kusaidia katika kutoa tuzo, vifaa vya michezo, na ufadhili wa matangazo nk

8 . Maonyesho ya Teknolojia: Kutumia teknolojia katika tamasha kunaweza kuongeza uzoefu wa mashabiki. Inaweza kujumuisha matumizi ya skrini kubwa za video, teknolojia ya ukweli halisi (AR) au ukweli uliodhabitiwa (VR) ili kutoa hisia za kipekee kwa watazamaji.
Mfano kuwasha tv pale uwanjani, na maeneo kama msimbazi kumshuhudia mashabiki wakifuatilia.

9 . Hafla za Jamii: Kuunganisha tamasha na jamii inaweza kuwa njia nzuri ya kuhamasisha na kutoa mchango kwa jamii, mfano DAMU, yatima , misaada nk.

10 . KUPIGA MNADA WA VIBEGI.
Kuwa na Wauzaji maalumu WA vifaa vya timu kama mabanda ya kuuza jersey, scaff, Bukta, t-shirt,SOCs sweta nk.

N. B
KUMTAMBULISHA BANGALA NA KUMUACHA KRAMO, ONANA AU PHILI KWA MKOPO.

# UNYAMA NI MWINGI.
 
1. Kiingilio tayari kinafahamika. 5000 tu.
2. Wasanii wakubwa watakuwepo. Akina Zuchu, Tundaman, nk.
3. Timu inayokuja ni Power Dyanamos
4. MC ni Ahmed Ally
5. Hiyo NB yako itabakia tu kuwa ndoto ya mchana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom