Uchaguzi 2020 Kutangaza maandamano pekee hakutoshi, kunahitaji maandalizi. Tujiulize kwanini maandamano ya Seif Zanzibar hayakufanikiwa

Kina Mbowe wasanii, pale wanawazuga Mabeberu waliwapa fedha za kampeni ili ionekane baada ya 'kuibiwa kura' walionesha hali ya kutoridhika na walijaribu ku protest

Hakuna wa kuandamana hasa huku bara ndip sababu hata Maalim kawapuuza hakuja japo awali aliahidi kuja
Umeongea points tupu. Huwez kumwamsha mtu akaandamane wakati hajui mwisho wa siku maandamano yanaishia ikulu au Kariakoo sokoni
 
Hukuandamana UKUTA, wala kwa Da'Mange kwa Lissu utajitokeza kweli?
Oooh! Wakati ule sikuwa nimedhulumiwa kama Sasa. Nimetumia hela yangu kufanya kampeni halafu unapora ushindi wangu kibwege tu. Hata mtume ametuamrisha kupambana na dhuluma kwa jihad
 
Mbona karatasi za kura zilizagaa mpaka zikawa zinatumika kufungia maandazi.
Huu wizi uliratibiwa na intelligence officers (TISS).

Hawa waliruhusu begi moja or so likamatwe ili ‘walinda kura’ wawe macho kuhakikisha kura haziingi ndani kutokea nje. Kumbe wizi wenyewe ulikuwa unafanyika ndani

Wale maafisa wa muda wa NEC ndio waliokuwa wanapiga kura za ziada ndani. Bahati nzuri/mbaya walikuwa na namba za wote waliojiandikisha na ilikuwa rahisi tu kutupigia kura sisi tulio busy humu ila kwenda kupiga kura hatutaki.

Bottom line: Kwa NEC hii, hakuna haja ya kushiriki uchaguzi mwingine
 
Jamana printers watakuwa walitengeneza karatasi 12,500,000 zenye kura kwa Magufuli, tuwasusie bidhaa zao wanatuharibia nchi.

Kura za wizi zingekuwa zimejazwa kwa mikono mipango haramu ya CCM ingejulikana siku nyingi.

Maandamano yaanzie Jamana printers kuelekea ofisi za tume.
 
Huu wizi uliratibiwa na intelligence officers (TISS).

Hawa waliruhusu begi moja or so likamatwe ili ‘walinda kura’ wawe macho kuhakikisha kura haziingi ndani kutokea nje. Kumbe wizi wenyewe ulikuwa unafanyika ndani

Wale maafisa wa muda wa NEC ndio waliokuwa wanapiga kura za ziada ndani. Bahati nzuri/mbaya walikuwa na namba za wote waliojiandikisha na ilikuwa rahisi tu kutupigia kura sisi tulio busy humu ila kwenda kupiga kura hatutaki.

Bottom line: Kwa NEC hii, hakuna haja ya kushiriki uchaguzi mwingine
nec hii hii ambayo Mbowe na halima wamekuwa wabunge kwa mihula miwili au hamkumbuki hilo....kususia bunge la corona kumewaharibia sana makamanda!
 
Umeanza lini kumpinga Mbowe?
Kuandaa maandamano ni fani kunahitaji mipango madhubuti, hata kama una ajenda muhimu huwezi kukurupuka na kutangaza leo au kesho kuna maandamano, Seif alikuwa na ajenda lakini hakuwa na mipango madhubuti aliongozwa na mihemuko, hasira na jazba.

Wataalamu wa mipango ya maandamano wanasema ili maandamano yafanikiwe kuna hatua muhimu lazima zizingatiwe.

  1. Lazima kuwe na sababu (issue) inayogusa jamii. Unaweza kutangaza maandamano ukakuta watu hawana interest nayo.
  2. Chagua ‘theme’ kauli mbiu itakayokuwa common kwa wote itakayotoa hamasa mfano, uonevu sasa basi au wimbo wa ujasiri.
  3. Toa taarifa kwa taasisi za misaada kama Red Cross na andaa utaratibu wa misaada ya haraka kwa waandamanaji watakaozidiwa wakati wa maandamano mfano maji na huduma ya kwanza.
  4. Tayarisha eneo mwafaka destination la kutolea matamko yako (open space, ofisi za serikali, nk) usitoe matamko ofisini kwako.
  5. Alika ‘known public speakers’ watakaotoa hotuba fupi fupi zisizochosha mfano viongozi wa dini, wasanii nk.
  6. Andaa mziki na wasanii watakaoburudisha.
  7. Andaa shelters mahema, jukwaa kama kuna ulazima.
  8. Andaa mabango yenye kuvutia na kufikisha ujumbe mfupi (inclusive) usibague kundi lolote la jamii.
  9. Kama lazima pata vibali au toa taarifa kwa mamlaka husika.
  10. Alika vyombo vya habari vya ndani na vya nje ikiwezekana vipe taarifa mapema kwa simu ama maandishi, email nk.
  11. Tumia mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram, You Tube nk kuhamasisha watu.
  12. Ijulishe jamii ya kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na marafiki kusudio lako la kufanya maandamano ya amani ukinukuu vifungu vya sheria vinavyo kusapoti.
  13. Mwisho kabisa hakikisha wafuasi na waandamanaji hawavunji sheria wala kufanya fujo.
 
Back
Top Bottom