barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,944
Kila ifikapo usiku Anna na Lucy huchangia kitanda kimoja na mpenzi wao Ben,ambaye wanaamini anawapenda wote kwa usawa.Anna na Lucy ni mapacha waliopishana dakika moja tu wakati wa kuzaliwa,hapo nyuma kila mtu alikuwa na mpenzi wake lakini wakaja kuona ni kama hajakamalika kwa kuwa na mpenzi tofauti hivyo wakaamua kuwa na Ben kwa wakati mmoja.Hali hii imewaletea umaarufu sana katika mji wanaoishi na katika mitandao ya kijamii
Mapacha hawa hawachangii tu mpenzi,bali wanachangia hata namna ya kuvaa,huvaa nguo sare,wamefanyiwa upasuaji wa pamoja kubadilisha muonekano wao,wanakula chakula sawa cha ujazo sawa wa "calories" kila siku,na hufanya mazoezi kwa muda sawa na urefu sawa.Lucy na Anna wanasema wana uwezo wa kufikiri sawa na kutenda sawa,yaani kila mtu ana uwezo wa kujuwa mwenzake anawaza nini.Hata mmoja anapopata maumivu ya mwili au hisia,mwenzake pia hujisikia hivyo.Kifupi ni kuwa wana kila kitu chenye ufanano.