Kusomesha na kufundisha nani yu sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusomesha na kufundisha nani yu sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by galagaja mtoto, May 30, 2012.

 1. galagaja mtoto

  galagaja mtoto Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wataalam wa lugha hasa wale wanaoketi mbele ya tbc juzi waliniumiza kichwa kwa kusema kuwa neno ''KUFUNDISHA'' lina maana kutoa elimu ya masuala yaufundi(mchundo) lakini yule anayesimama mbele ya darasa kwa shule ya msingi/sekondari inasemwa kuwa ''ANASOMESHA''. Sasa wadau wangu hebu niwekeni sawa je nikisema ''KUJIFUNZA'' hufanyika kwa wanachuo tu nitakosea? kwani ndo wanakopatikana wakufunzi.

  ''kama hujui kitu funga domo lako'' je hii nayo ni sahihi?
   
 2. Catch-22

  Catch-22 Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Binafsi, ninatumia kufundisha na kusomesha kama walivyoeleza wataalamu wa Kiswahili wa huko TBC.

  Nikirudi kwenye suali lako sasa, ninakumbuka kusema "leo tumesomeshwa uadilifu" kwa mfano, nilipokuwa shule ya msingi na sekondari yake, sikuwa nikitumia nimejifunza.

  Kwa ufahamu wangu, kujifunza kunakuja kwenye utaalamu au kwenye ustadi kama kushona, kupika, kufuma, ufundi mchundo na kadhalika. Masomo bila ya vitendo unasoma na hujifunzi.

  Kwa hiyo kwa ufupi jibu la suala lako ni kuwa, hata huko chuo kikuu kuna baadhi wanaoenda kusoma tu na sio kujifunza
  :)
   
 3. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  galagaja mtoto karibu jamvini!
  Mimi nianze kukueleza tangu mwanzo kwamba ni lazima uifahamu tabia ya lugha ya Kiswahili vinginevyo itakuchanganya bure. Vitenzi vya lugha hii vina tabia ya kunyambuka na kuzalisha maneno mengi tu ili kuongeza msamiati wake. Mimi sitadiriki kusema yupi yu sahihi kati ya atumiaye neno 'kufundisha' na yule asemaye 'kusomesha'. Ila nachangia mjadala kwa kukuonesha asili ya maneno yote mawili ili mwenyewe uamue ni neno lipi litakuwa jalabati katika muktadha upi.

  Neno 'Kufundisha' liko kundi moja na maneno ya mnyambuliko kama funda, funza, funzo, fundishika, ufundishaji, mafunzo, kufundishika, wakufunzi, wafundwao, mafundi, wanafunzi...........Kimsingi maneno ni mengi. Lakini ukiyachunguza vizuri maneno yote niliyoyaorodhesha utagundua kama yana mofimu -fun- ambayo ndiyo mzizi.

  Neno 'anasomesha' halikadhalika limo katika kundi moja na maneno ya mnyambuliko kama kusoma, masomo, kisomo, msomi, wasomao, kusomwa, kusomewa, kusomeshwa, kasome, kimesomeka, nimekisoma, somo....... Unaweza kuongeza maneno kadri unavyoweza. Lakini ukiyachunguza maneno yote ya mnyambuliko utaona yana mzizi -som-.

  Mantiki itokanayo na mnyambuliko wa maneno yote mawili inaweza kutubashiria kwa usahihi zao la kila neno. Yaani kutokana na neno 'kufundisha' tutampata fundi na kutokana na neno 'anasomesha' tutampata msomi.

  Ninawasilisha!
   
Loading...