Penye ukweli pasi na kujali kambi ni heri kuusema. Vinginevyo tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu milele.
Hongereni CCM Kwa kushinda chaguzi zenu na kama mabwege yakiendelea kulaza damu kazeni uzi hapo hapo.
Kwani malengo ya chama cha siasa nini? Si walisema "the end justifies the means?" Wacha walie lie mkiona yamelala au yako kihasara hasara nyie endeleeni kupita na kura kama vipi, zote kabisa!
Kwa hakika aliyelala usimwamshe.
Kwani nani aliwaambia CCM ni charity organization au hata kuwa ni watangaza dini?
Kutwa kucha wanalia wameibiwa chaguzi. 2024 na hata 2025 kama 2029 na 2030 watalia hivyo hivyo kama wamerogwa tu.
Nani ajuaye labda wao ni wapinzani wa kudumu. Kwamba walishajikatia tamaa au labda ndiyo iliyo core business yao?
Kwani hata wanachukua hatua zipi za maana kuona kuwa sasa au kesho wanaweza kushinda vipi? Kwamba iko wapi mikakati yao ya ushindi? Kwamba wako kusherehekea nyomi mikutanoni mwao, zisizotafsirika kwenye uwanda wowote wa maamuzi?
Kama ndivyo nini tofauti ya vyama hivi na kina TLP, CHAUMA, CUF, au hata na DP ya leo?
Kwenye uwanja wa mapambano mbinu zote dhidi ya adui ni halali. Yaani mbinu safi na hata chafu (overt and covert) zote ruksa. Kumbe sisi tunategemea kushinda kwa kudra za Mola? Kama ndivyo ni heri tukajisajili rasmi kwa akina Mwamposa, Lusekelo au hata kina Mwaipopo huko. Kwa mtaji huo tukawe tayari kupokea vibao shavu moja baada ya jingine bila ya kunung'unika.
Hivi huwa tunajihoji sawa sawa ndani kwa ndani au hata nje kwa nje? Kutambua tuko kamili na kweli tumedhamiria? Tunajua hii ni vita, siyo lelemama? Ya kwamba kama ilivyo kwa kumwua nyani hatupaswi kumwangalia usoni?
Bravo: TAL, Mwabukusi, Dkt. Slaa, Dkt. Nshala, Kamanda Mdude na nyote mliodhamiria kweli kweli.
Kwa hakika mlipo tupo!
Pumzika kwa amani Rev. Christopher Mtikila kama wale hukupata kupoa.