Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,141
Ni jirani yetu huko nyumbani kwetu, pia kuna kaurafiki kwa mbali baina yetu. Likizo sometimes tulikuwa tunajisomea pamoja kwakuwa tulikuwa darasa moja.

Jamaa akawa teacher wa Serikali baadaye. Sasa nasikia walimu wana miiko mingi kutokana na mazingira yao ya kazi, sometimes wanakuwa walezi.

Sasa jamaa hakuacha sunnah ya Mtume akafuga ndevu vizuri. Mkuu wa shule akamwambia Mr nyoa hizo ndevu hii shule ni secular, jamaa akakataa.

Alipoona anazidi kuhimizwa kunyoa uchebe na sometimes kutishiwa kufutwa ajira akamwahi boss wake akaandika 24 hrs resignation letter, mkuu wa shule akaipitisha, na Mkurugenzi akamaliza kazi.

Jamaa sasa kwa moyo mweupe analima kijijini. Kaka yake aliyemsomesha wamegombana baada ya jamaa kupiga kalamu chini lakini anasema hawezi kurudi.
 
Ni jirani yetu huko nyumbani kwetu, pia kuna kaurafiki kwa mbali baina yetu. Likizo sometimes tulikuwa tunajisomea pamoja kwakuwa tulikuwa darasa moja.

Jamaa akawa teacher wa serikali baadaye. Sasa nasikia walimu wana miiko mingi kutokana na mazingira yao ya kazi, sometimes wanakuwa walezi.

Sasa jamaa hakuacha sunnah ya Mtume akafuga ndevu vizuri. Mkuu wa shule akamwambia Mr nyoa hizo ndevu hii shule ni secular, jamaa akakataa.

Alipoona anazidi kuhimizwa kunyoa uchebe na sometimes kutishiwa kufutwa ajira akamwahi boss wake akaandika 24 hrs resignation letter, mkuu wa shule akaipitisha, na Mkurugenzi akamaliza kazi.

Jamaa sasa kwa moyo mweupe analima kijijini. Kaka yake aliyemsomesha wamegombana baada ya jamaa kupiga kalamu chini lakini anasema hawezi kurudi.
Nenda Znz huko watoto wanakazaniwa Madrasa kuliko shule.
 
Back
Top Bottom