Kusema Rais anashauriwa vibaya ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana akili; naona ni ukosoaji wa kinafiki

Akila za raisi zinamtosha mwenyewe kuvukia barabara
 
Afadhali uwe na Rais angalau mwenye akili kiasi, ukivhanganya na ushauri mambo yanakaa sawa.

Sasa chukua kichwa maji uone kama kuna lolote litatokea
Raisi lazima awe na basic knowledge ya baadhi ya mambo na kufanya utafiti wa hapa na pale sasa wakwetu yeye kila kichwa hawezi halafu ni MVIVU KUPINDUKIA .labda la kununua magoli ya yanga na simba
 
Kwanza kabisa, Samia Suluhu Hassan si accidental president.

Kama unakubali kuwa CCM ilishinda uchaguzi 2020, basi watu walichagua tiketi ya Magufuli/ Samia. Hakuchaguliwa mtu, ni tiketi ya watu wawili, mgombea urais, na mgombea mwenza anayekuja kuwa VP.

Na kuwa VP maana yake ni kwamba you are a heartbeat from the presidency. Watu walikuwa wanatakiwa wajue kwamba rais anaweza kufariki madarakani, na akifariki madarakani, tumempitisha huyu Samia kuwa rais.

Tatizo Watanzania wengi wanakwenda kwa mazoea, walifikiri rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufia madarakani, walifikiri Samia atakuwa pambo tu, afanye kazi cwremonial za kukata tepe, kuzindua majengo na kuwakilisha nchi kwenye misiba.

Sasa Magufuli alivyofariki, ndiyo wanajiona wana accidental president.

Accidental president kivipi wakati katiba imewaeleza kabisa kwamba rais akifariki, makamu wa rais anakuwa rais?

Kitu kinajulikana kabisa na kipo katika katiba, kwa nini mnakiita accident?

Kifo kinajulikana kipo, kwa nini mnakiita accident?

Samia ni rais fair and square, if at all umekubali matokeo, na hata kama hukubali matokeo that is a separate and even bigger issue.

Kuhusu nchi changa na nchi established, hoja yako haina mashiko.

We are nit talking about nuclear reactors here, we are not talking about sending people to tye moon.

Kusema huko nchi changa ni tofauti na nchi zilizoendelea katika hili la ushauri ni makosa, ni kujidogosha tu.

Kwa sababu nimekutolea mfano mzuri sana wa rais J.K Nyerere alivyopewa ushauri mbaya, na alivyoufanyia vetting, akatumia unofficial advisers, akafanya tofauti na alivyoshauriwa na washauri wake rasmi.

Kama Nyerere aliweza kufanya hivyo 1970s, kwa nini rais mwingine yeyote aliyemfuatia ashindwe kufanya hivyo?
 
Yaan wanasiasa wanaiba pesa serikalini anakuja kununua apartment na kujenga mahotel halafu tunafurahia hivi unajua atakuwa ameleta athari kias gani kwa hao maskin ... amna nchi inayoendeshwa hivyo
 
Running the government it is not like family matters
 
Babako Kwa mfano akikosea pakubwa, waeza Sema hadhani kuwa......., Si utanyamaza au kutafuta namna ya kuwasilisha kosa lake,


Tukisema mkubwa hakosei, maana yake ni upande wa pili, kulinda Heshima ya uongozi na KITI.

Bt yapo makosa ambayo hapasi kukosea, mf baba kula mayai ya mama nk nk, haivumiliki.

Miiko ya uongozi ifuatwe. Na viongozi wajiheshimu, wasifanye makosa ambayo hata waongozwa watastuka.
 
Well..so far hapa Kwa mujibu wa mtoa mada hatujadili ushauri wowote aliopewa Samia halafu akakubali...na huo ushauri ukawa sio sahihi...

But twende with assumptions kuwa tunajadili Samia na washauri wake...
Je wewe unamjua hata mshauri mmoja wa Samia official?..
Point yangu hapa ni kuwa kabla hata ya Rais hatujamlaumu Kwa kupokea ushauri ...kwanza tuna uhakika hata wapo hao washauri?na Wana qualify kuitwa washauri?..Kwa sababu Kwa uzoefu wangu huwa inapita miaka kadhaa ndo unakuja kusikia Fulani alikuwa mshauri wa Rais ..mfano Lipumba alipoingia CUF ndo tunaambiwa aliwahi kuwa mshauri wa Rais Mwinyi na Museven kwenye uchumi na wala hatuna namna ya Ku verify alikuwa mshauri Kwa kiwango gani?..

Umezungumza kuhusu Nyerere...Nyerere alitaifisha nyumba na Mali za watu bila kuwepo sheria ya kumruhusu kufanya hivyo....ikaja sheria kupitishwa tayari zoezi limeshapita....yaani kama kipimo ni Nyerere makosa yake ni mengi mno hafai hata kutajwa kama mtu alie heshimu ushauri na washauri..
 
Mkuu,

Kwani wewe unaposikia "washauri wa rais" unafikiri nini?

Unaelewa kuwa kwa kuanzia tu, ukiacha hao wanaoteuliwa kuwa "mshauri wa rais wa ...", unaelewa kuwa cabinet nzima ni washauri wa rais?
 

The buck stops with the President, full stop... the rest is history!​
 
Mkuu,

Kwani wewe unaposikia "washauri wa rais" unafikiri nini?

Unaelewa kuwa kwa kuanzia tu, ukiacha hao wanaoteukiwa kuwa "mshauri wa rais wa ...", unaelewa kuwa cabinet nzima ni washauri wa rais?
The level of dumbness is astounding!!

Yaani kabisa mtu anauliza washauri wa Rais ni akina nani? Hivi Civics waliacha lini kufundishwa mashuleni?

Huu ujuha ni wa kipekee.

Mfano mmoja mrahisi tu wa mshauri wa Rais ni Mwanasheria mkuu



 
Tuna kazi kubwa sana ya kuelimishana hapa.

Tena bila mshahara.
 
Mkuu,

Kwani wewe unaposikia "washauri wa rais" unafikiri nini?

Unaelewa kuwa kwa kuanzia tu, ukiacha hao wanaoteukiwa kuwa "mshauri wa rais wa ...", unaelewa kuwa cabinet nzima ni washauri wa rais?
Nafikiri washauri wapo generally na kuna washauri specific Kwa masuala specifics..
Ndo maana kina Larry Summers wanasifika dunia nzima...wanapata credit Kwa kuokoa nchi zaidi ya moja kiuchumi...wakati ule USA na Mexico baadae...na Hadi akarudi wakati wa Obama.......

So yes cabinet nzima ni ya washauri...
But cabinet inaundwaje?kupitia wabunge...wabunge wanapatikanaje...nayo ni suala lingine kabisa la chaguzi na tume ya uchaguzi...

Lakini wale wanaoteuliwa Kwa kazi moja Tu ya kushauri na katika mfumo rasmi unaotambua wako pale Kwa kushauri masuala specifics... uchumi, international investment,n.k...hao Mimi ndo nimesema wazi mifumo yetu haijakomaa kabisa kuwa na washauri walioshiba sawasawa Kwa maoni yangu....na hata uwepo wao sijui kama ni rasmi
 

Kwani mtu anayeshauriwa ni kwamba ana akili? Je Rais hana washauri? Na kama anao wanakazi gani kama si kumshauri?
 
You are not being clear.

Nchi yetu haijakomaa kivipi?

Hatuna washauri wenye sifa? Hatuna mifumo ya kukubali ushauri?

Elewa core discussion hapa ni kwamba watu wanalaumu washauri na wanamuacha rais.

Sasa washauri na ma Ph.D yao wote hao, serikali ina makabrasha yaliyojaa ushauri wa kila aina, bado unasema nchi yetu haijakomaa?

Haijakomaa kivipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…