Namna ya kumshawishi Mfadhili akuandikie Hundi

Feb 5, 2022
31
48
1687785585109.png
Takwimu ulimwenguni zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 70 ya fedha zinazoenda kwa Asasi za Kiraia kama ruzuku hutolewa na mtu mmoja mmoja yaani "individual supporters" . Kufanikiwa kwa Taasisi katika upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuendesha miradi na programu (fund development) hutegemea sana uwepo wa wafadhili wa namna hii. Taasisi inapaswa kuwa na utaratibu wa kutafuta na kusajili mfadhili mmoja mmoja (donor cultivation) kwa ajili ya kufadhili utekelezaji wa miradi na program pia hata gharama za uendeshaji wa Taasisi.
Kwa Taasisi ambazo zina utaratibu huu, hugawa wafadhili wao katika makundi makuu matatu mpaka manne; mfano; wafadhili wadogo, wafadhili wa kati na wafadhili wakubwa.

Kumshawishi mfadhili (individual supporter) akuandikie hundi kwa ajili ya uendeshaji wa miradi na programu za Taasisi inahitaji muda na mkakati; ili kumshawishi kwa mafanikio zingatia yafuatayo;
  • Mhusika(mfadhili) asiwe mtu mgeni kwako au kwa Taasisi yako, au awe ameonyesha shauku juu ya kile ambacho Taasisi yako inafanya au juu ya mradi unaotaka kuufanya.
  • Hakikisha kiasi cha pesa unachomuomba kipo ndani ya uwezo wake.
  • Mshawishi kinagaubaga kwa kumueleza kwanini pesa yake ni muhimu kwa Taasisi/mradi, na itatumikaje pia matokeo yanayotarajiwa ni yapi
KUMBUKA: Inaweza ikaichukua Taasisi zaidi ya mwaka kumshawishi mtu na kuwa mfadhili wa Taasisi.

OMAR MSONGA (BA. PPM &CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom