Lighton
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 2,185
- 3,659
Wakuu Habari za mchana huu
Binafsi niseme, mimi kwa upande wangu kusamehe siyo shida na huwa inachukua muda kufungua moyo, inategemea na ukubwa kosa lenyewe. Naweza kudondosha visa viwili muhimu.........
1. Kisa cha kwanza; Kipindi nipo primary niliwahi kushuhudia matendo ya chuki ya baadhi wafanyabiashara ambao walikuwa wanafanya biashara aina moja na mzee.
Mzee wangu alikuwa na bahati sana kwenye biashara, kwahiyo akawa anapiga sana pesa, hapo jirazi zake wakaanza kuleta noma, shutuma za hapa na pale, yaani kiufupi mambo yalikuwa mengi.
Mpaka ilifikia hatua wakapanga njama za kumpoteza, rafiki zake wa karibu ndo walikuja kumsanua, mzee alivyojua nayeye akaenda kuwapiga mkwara. Nilikuwa nawafahamu kwasababu watoto wao walikuwa rafiki zangu.
Ajabu ni kwamba mimi na watoto wao hatukuwahi kuwa maadui mpaka leo, ilichukua muda kuwasamehe kwa kupanga njama mbaya za kutaka kumpoteza mzee wangu lakini baada ya muda kupita nilifungua moyo wangu na mambo yakaendelea kama kawaida.
2. Kisa cha pili ni cha Mshikaji wangu,pamoja na demu, Hapa sina stori nyingi ila jamaa alinizunguka kwa demu wangu, jamaa alikuwa anaruka na demu wangu kisirisiri na demu wangu nae alikuwa anaruka na mshkaji wangu yaani both team to score anyway nilishawasamehe wote nikaamua kumove on.
Nakumbuka matukio, ila nilishasamehe, wakuu kusahau ni ngumu.