Kusamehe ni kitu kigumu sana:

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Kusamehe ni kitu kigumu sana ingawaje ni tendo zuri sana kwa upande mwingine .Kwanini ni msamehe mwingine ambaye ananikosea mara kwa mara na wakati mwingine kwa makusudi na wala harudi kuomba msamaha?Kiakili na kwa kutumia busara ya kawaida,unaweza kusema kuwa naweza kumsamehe ndugu yangu huenda akiwa amenikosea mara moja au mara mbilihivi.

Petro alikuwa yuko tayari kusamehe mara saba.Lakini bwana yesu anasema kwamba tusamehe daima,bila kuhesabu ni mara ngapi umekosewa.Kwanini hayao unaweza kujiuliza .Jibu kwamba ndivyo mungu anavyotenda pamoja nasi,yaaani anatusamehe daima,bila mipaka,bila kuhesabu ni mara ngapi tumemkosoea.

Hivyo tunaalikwa kusamehe kama sisi tunavyosamehewa .Kwa upande mwingine kusamehe ni jambo jema kiafya na kisaikolojia au kwa maneno mengine kutokusamehe ni hatari kimwili na kisaikolojia kwa muhusika yaani yule anayebeba kinyongo.Wanasayansi ya jamii wanasema usipo samehe unatengeneza sumu ndani ya mwili wako ambayo inakuteketeza kimwili na kisaikolojia.

Kwa upande mwingine kusamehe nikuishi amri ya mapendo yaani kumpenda mungu na jirani ,ikiwa namaana kwamba kumpenda mwingine hata anapokosa.
 
Sulpha eeee ondoa basi kwanza hiyo avatar maana wengine inatukumbusha miguu ya vistuli viwili bana!
ps: ukishaiondoa ndo ma asenali tutapata nguvu ya kuchangia!
 
Sulpha eeee ondoa basi kwanza hiyo avatar maana wengine inatukumbusha miguu ya vistuli viwili bana!
ps: ukishaiondoa ndo ma asenali tutapata nguvu ya kuchangia!

Bishanga vipi tena lakini kuna timu nyingi za kushabikia sio lazima ubakie Asernal,ok tuache hilo swala la arsenal,maana hali yao bado sio nzuri.
 
Inategemea na tukio au mkasa Mr.rocky maana kuna matukio mengine ni ishu kubwa sana kusahau.

Mkuu hakuna kitu hapa duniani ambacho hakiwezekani
Tukio limeshatokea na limekuathiri kwa namna moja au nyingine na madhara umeyapata
hata usiposamehe huwezi kurudisha kile ambacho kimeshatokea
MNi kama maji yamemwagika kwenye mchanga huwezi kuyachota tena
japo inaumiza sana na mtu unapata maumivu makubwa haswa unapomuona yule aliyekufanyia mabaya bado anaendeela kuwepo ila mkuu kusamehe kupo tuu
 
Red:nakubaliana na wewe.
Swala linakuja je unaweza kusamehe bila kusahau?
 
kusahau ngumu sana
 
Bishanga vipi tena lakini kuna timu nyingi za kushabikia sio lazima ubakie Asernal,ok tuache hilo swala la arsenal,maana hali yao bado sio nzuri.
Mkuu,we can talk now!
Katika ndoa hasa siku za mwanzo huwa kuna tendency ya wanandoa kujaribiana tena wakati mwingine unconsciousily yaani ka vile mmoja ana test zali. Mathalan mmoja anaweza kuchelewa kurudi makusudi aone mwenzie atasemaje,mara mwingine aende mahali bila kuaga ili mradi kupima tu boundaries zinaishia wapi. Tatizo hapa ni mmoja kuugulia ndani bila kusema,mkeo anarudi saa mbili we mama karibu,anarudi saa nne we mama karibu kumbe ndani kifua kinabana.Sasa siku ukija kulipuka atakwambia alaaa sasa kwa nini ulikuwa husemi? Mi naona ndo yale yale ya MJ1 ya ku mark teritory mkioana ni bora muwekeane mipaka mapema kuliko kuumizana pasipo sababu.
 
Red:nakubaliana na wewe.
Swala linakuja je unaweza kusamehe bila kusahau?

Kusahau inakuwa ni ngumu ila kumtakia mtu uliyemsamehe kuwa nimekusamehe ila sitakusahau ni kama hujatekeleza sawa sawa msahama wako
Msamehe na ishi kawaida na lione tukio limepita japo kuna sehem unakumbuka kitu kinakutia machungu ila usimlaani yule mhusika moyoni mwako kuwa bila yeye lisingetokea
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom