Kusajili mshambuliaji kutoka mali ni sawa na kuingia msituni kuvua samaki!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
14,205
Reaction score
19,142
Tuliambiwa tumesajili Doumbia wa ukweli kutoka ligi kuu ya Mali, tena alikuwa mfungaji bora kwenye ligi hiyo. Hiyo ni taarifa ya kweli.
Lakini ligi kuu ya mali si chochote kitu, si miongoni mwa kumi bora katika mkeka wa ubora wa ligi kuu hapa Afrika. Mkeka huo huu hapa:

Top 10 African Football Leagues.
1. Egypt– Egyptian Premier League
  • 2. Morocco – Botola Pro
  • 3. Algeria – Ligue Professionnelle 1
  • 4. South Africa – Premier Soccer League (PSL) / Betway Premiership
  • 5. Tunisia – Ligue Professionnelle 1
  • 5. Tanzania – NBC Premier League (Ligi Kuu Bara)
  • 6. Angola – Girabola
  • 7. DR Congo – Linafoot Ligue 1
  • 8. Sudan – Sudan Premier League
  • 9. Ivory Coast – Ligue 1 Lonaci
  • 10. Libya – Premier League
Kamati ya usajili ya simba walijitoa ufahamu wakaamua kuingia msituni kuvua samaki. Tukaletewa tumbili kukaaminishwa kuwa anajua kuogelea balaa!!

Huwezi kuwa na malengo ya kutwaa ubingwa wa Afrika halafu unaenda kusajili mshambuliaji kwenye ligi chovu kama ya mali ambayo haiko kwenye ligi 10 bora barani Afrika. Lazima uvamie kwenye ligi zilizo juu yako kwenye msimamo na kusajili huko yaani Misri, morocco, Algeria, Afrika ya kusini na DRC mwisho!!

Vinginevyo hizo ngonjera za kutuambia malengo ya kufika fainali au kutwaa ubingwa wa Afrika ZIKOME!!
 
Kipindi cha usajili ni kipindi cha upigaji wa wajanja!! Huyo Doumbia ndiyo wa kutuvusha champions league Afrika kweli? Tuache masihara!
 
kwani hamna timu zingine za kushabikia, au kwanini usiwe na timu yako mwenyewe?
 
George Weah asingesajiliwa ulaya kama vigezo vya usajili ndio hivyo unavyoweka.
Ungeongelea qualitu ya mchezaji kwani Diara ametoka wapi.
 
Usichokifahamu mtoa mada ni kitu kimoja tu!
Yule Ibrahim Doumbia ni Osimhen mtupu. Hadi semaji letu la CAF lilituthibitishia jambo hili ile siku ya simba day.
 
kwani hamna timu zingine za kushabikia, au kwanini usiwe na timu yako mwenyewe?
Hapa bongo kuna timu moja tu bora nayo ni SIMBA! NAdiyo maana inatuuma kusajili toka
George Weah asingesajiliwa ulaya kama vigezo vya usajili ndio hivyo unavyoweka.
Ungeongelea qualitu ya mchezaji kwani Diara ametoka wapi.
Sasa Diarra naye mchezaji wa kusema ni mchezaji? Diarra na Doumbia wako daraja moja tu! Ndio maana nilisema labda Doumbia angewafaa wananchi maana wana sampling yake na wameridhika naye!! Kwa Simba lazima apate thank you asubuhi na mapema!
 
Tuliambiwa tumesajili Doumbia wa ukweli kutoka ligi kuu ya Mali, tena alikuwa mfungaji bora kwenye ligi hiyo. Hiyo ni taarifa ya kweli.
Lakini ligi kuu ya mali si chochote kitu, si miongoni mwa kumi bora katika mkeka wa ubora wa ligi kuu hapa Afrika. Mkeka huo huu hapa:

Top 10 African Football Leagues.
1. Egypt– Egyptian Premier League
  • 2. Morocco – Botola Pro
  • 3. Algeria – Ligue Professionnelle 1
  • 4. South Africa – Premier Soccer League (PSL) / Betway Premiership
  • 5. Tunisia – Ligue Professionnelle 1
  • 5. Tanzania – NBC Premier League (Ligi Kuu Bara)
  • 6. Angola – Girabola
  • 7. DR Congo – Linafoot Ligue 1
  • 8. Sudan – Sudan Premier League
  • 9. Ivory Coast – Ligue 1 Lonaci
  • 10. Libya – Premier League
Kamati ya usajili ya simba walijitoa ufahamu wakaamua kuingia msituni kuvua samaki. Tukaletewa tumbili kukaaminishwa kuwa anajua kuogelea balaa!!

Huwezi kuwa na malengo ya kutwaa ubingwa wa Afrika halafu unaenda kusajili mshambuliaji kwenye ligi chovu kama ya mali ambayo haiko kwenye ligi 10 bora barani Afrika. Lazima uvamie kwenye ligi zilizo juu yako kwenye msimamo na kusajili huko yaani Misri, morocco, Algeria, Afrika ya kusini na DRC mwisho!!

Vinginevyo hizo ngonjera za kutuambia malengo ya kufika fainali au kutwaa ubingwa wa Afrika ZIKOME!!
Unawafahamu Fredrick Kanoute na Pascal Feindouno?
 
Back
Top Bottom