Kusaidia ukweni ni hiyari, sio lazima

Kusaidia ukweni ni hiyari, sio lazima

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,547
Reaction score
139,883
Napenda kuwaachia ujumbe huu wake/wapenzi wetu,wakwe na mashemeji kwamba kusaidia ukweni hususani mume kusaidia upande wa mwanamke ni kitendo cha hiyari na sio lazima

Kitendo hiki cha hiyari ni katika namna ya kujenga mahusiano ya karibu katika shida na raha nimekuwa kikichukuliwa na baadhi yetu kwamba ni wajibu kwa mwanaume kuchangia shida za ukweni.

Ni dhahiri kuwa mimi kama kijana niliyemuoa binti yenu ninawajibika kulipia mahali na kumtunza vyema binti yenu,mambo mengine ya ukweni ni mambo ya hiyari kadri ninavyoguswa na ukubwa au unyeti wa tatizo. Nimeamua kusisitiza hili kutokana na sisi mabraza kukutana na kesi nyingi za wadada kulazimisha mabwana wasaidie kila kitu kwa wazazi na wadogo wake. Unakuwa umewekewa mpaka bajeti za ada za shule za wadogo zake mke. Hii haikubaliki hasa kutokana na hali ya Magufuli.

Mimi kama mume ninawajibika kwa familia yangu na wazazi wangu pekee.

Karibu ni kwa maoni
 
Halafu mashemeji na mawifi wanaoombaga bila aibu kana kwamba ni lazima huwa wananiacha hoi. Ila kama mwanamke ana kipato akiwatumia kiasi sio mbaya na isiwe ndo kuelekeza pesa yote huko.

Ila tatizo likiwa kubwa linalohitaji msaada sio mbaya.
 
Mnaambiwa muishi na wake zenu kwa wema.
Sawa sio lazma kuhudumia kwao Ila ni katika vtu vitakuongezea mapenzi kwa mkeo kuona unaijali familia yake!

Utajiskiaje siku unamsifia mama yako kavaa gauni zuri afu akakwambia mkeo ndo alinipa hiki kitenge?!!..au ukaona mama yako kimya haombi hela mwezi huu kumbe mkeo ndo amesababisha?!!!

Basi na unapomfanyia mkeo,mapenzi yake juu yako yanaongezeka Mara dufu
 
msaidie pote kwa kadii ya uwezo wenu mkuu.
umeanza vizuri lkn suala la kumalizia utasaidia wazazi wako tu linatengua umoja wenu.
First priority ni familia zetu(baba,mama na watoto), wazazi wa pande zote pia tunawasaidia kwa kadili ya uwezo bila upendeleo ila sio lazima.
 
Mnaambiwa muishi na wake zenu kwa wema.
Sawa sio lazma kuhudumia kwao Ila ni katika vtu vitakuongezea mapenzi kwa mkeo kuona unaijali familia yake!

Utajiskiaje siku unamsifia mama yako kavaa gauni zuri afu akakwambia mkeo ndo alinipa hiki kitenge?!!..au ukaona mama yako kimya haombi hela mwezi huu kumbe mkeo ndo amesababisha?!!!

Basi na unapomfanyia mkeo,mapenzi yake juu yako yanaongezeka Mara dufu


Umeandika vyema sana.
Pokea like mubashara. Ningekupa likes 1000+ tatizo kitufe kinatoa like moja tu kwenye kila member.
 
Ewaaaaah, haaa haaa Haaa teeeh teeeh teeeh
Hahaaa. Teh teh teeh

Ila saa nyingine vinashangaza. Eti shemeji kama wewe dada akisema kuna ndugu ana shida huwezi kumsaidia?.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndoa ni zaidi ya muunganiko wa mwili mmoja yani mme na mke ila ni muunganiko wa familia ya mume na mke matatizo ni yenu wote kama uwezo unao saidia tu
 
Mmmmh kwani wewe umwlazimishwa kusaidia ukweni
 
Napenda kuwaachia ujumbe huu wake/wapenzi wetu,wakwe na mashemeji kwamba kusaidia ukweni hususani mume kusaidia upande wa mwanamke ni kitendo cha hiyari na sio lazima

Kitendo hiki cha hiyari ni katika namna ya kujenga mahusiano ya karibu katika shida na raha nimekuwa kikichukuliwa na baadhi yetu kwamba ni wajibu kwa mwanaume kuchangia shida za ukweni.

Ni dhahiri kuwa mimi kama kijana niliyemuoa binti yenu ninawajibika kulipia mahali na kumtunza vyema binti yenu,mambo mengine ya ukweni ni mambo ya hiyari kadri ninavyoguswa na ukubwa au unyeti wa tatizo. Nimeamua kusisitiza hili kutokana na sisi mabraza kukutana na kesi nyingi za wadada kulazimisha mabwana wasaidie kila kitu kwa wazazi na wadogo wake. Unakuwa umewekewa mpaka bajeti za ada za shule za wadogo zake mke. Hii haikubaliki hasa kutokana na hali ya Magufuli.

Mimi kama mume ninawajibika kwa familia yangu na wazazi wangu pekee.

Karibu ni kwa maoni
Kumbe ndo maana unampinga JPM bado
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom