Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ivunjwe na kuundwa upya

Nimekuelewa vizuri, ingawa umeogopa kufunguka zaidi kwani utashambuliwa.
Nasisitiza haya yote yamesababishwa na ukimya wa kutokujua wafanyeje. Mbona mambo mengine hawakawii kujibu? Kwani kama aliugua kwa uchovu wangesema kulikuwa na shida gani?
Yaani bega tu linauma au ana mafua inabidi uambiwe? Pambaaf kabisa, subirni tango pori lingine toka kwa kigogo
Maana aliwaambia gavana anatumbuliwa
Mkuu wa mkoa mbeya anatumbuliwa
Makamu wa raisi samia suluhu kakamatwa
Na ujinga kibao tu anawajaza
 
Kiuhalisia imeshindwa kazi halisi ya yanayopaswa kufanywa na kurugenzi hiyo na kubaki kama idara ya itikadi na uenezi ya chama.

Tukio lililo ikumba nchi kwa siku tatu na kuleta tahayari na utengano lingeweza kuzuiwa kiweledi kama kurugenzi hiyo ingeamua kuilinda Ikulu na mambo ya aina hiyo, badala yake Mkurugenzi Gerson Msigwa anajiingiza naye kwenye mambo ya kivijembe vijembe kama watu wa mtaani.

Badala ya kuwa kitengo cha sifa na mapambio wanaweza kuingia deep zaidi kuisemea Ikulu na Urais kama taasisi kamili na yenye watu wengi muhimu na majukumu tofauti tofauti.

Hawabuni hata vipindi kufundisha vijana nini hasa mpangilio wa kazi ndani ya maeneo ya Ikulu na ofisi zake kiasi cha kuwavutia vijana kuja kufanya kazi Ikulu tofauti na sasa wanajua kuna Rais na kazi ni kuteua na kutumbua tuu.

Wakati huu ni muhimu kufanya mabadiliko kwani Msigwa inaonyesha sio size yake tena
Msigwa sio mtanzania mwenzetu.. na yeye kuna watu anawaita nyumbu hivo hana muda wa kihangaika nao..

Shame..
 
Kurugenzi ya ikulu haina kazi ya kujibu kila uzushi wa malofa chadema
Mara baada ya rais kuzungumza na kwenda kupiga picha walijibu kiaina kwa kuweka wimbo fulani hivi wa kidini nadhani ni ule uitwao Hauwezi Kushindana na Mwanadamu wa Goodluck Gozbert. Nilihisi ni majibu na vijembe kwa waeneza uvumi wa "simu ya kifo".
 
Yaani bega tu linauma au ana mafua inabidi uambiwe? Pambaaf kabisa, subirni tango pori lingine toka kwa kigogo
Maana aliwaambia gavana anatumbuliwa
Mkuu wa mkoa mbeya anatumbuliwa
Makamu wa raisi samia suluhu kakamatwa
Na ujinga kibao tu anawajaza
Vijana mnajadili kila jambo kwa mihemko. Nyie mnaona ni ushindi dhidi ya hao walio anzisha taharuki hiyo lakini niwaambie kuwa wao ndio wameshinda.
Kwa sababu Rais Magufuli hawezi kuwa yeye yule wa Jana na juzi tena! Lazima atabadilika sio katika misimamo bali katika tabia. Lazima kutatokea mabadiliko makubwa sana na kama hayatakuwapo basi ni sikio la kufa.
Kibinadamu lazima atajiuliza jee alikuwa sawa kuhusu hatima ya Lissu(akiwa kama Rais), alikuwa sawa juu ya maamuzi ya watumishi wa vyeti nk nk. Jee huo sio ushindi kwa hao walio zusha taarifa hizo na kuleta taharuki?
 
Naona mnahamisha magoli, mkubwa ukivuliwa nguo chutama tantalila hazitobadili ukweli kuwa mnakurupuka.
Tena hili jambo limewaaibisha sana na watu wengi wamepoteza imani na upinzani, Magufuri kawapiga KO mapema
 
Wajumbe naamini hamjambo!
Baada ya kimya cha muda mrefu mimi Mzee wa Anecdote kutoka ukanda wa nyanda za juu kusini nina neno kwa wasaidizi wa Mkulu.

Kule Mwakaleli, Mbeya miaka 62 iliyopita kulikuwa na Mzungu mwenye asili ya Ujerumani aliyebatizwa kwa jina la Mwakapalila ambaye pia ndiye aliezeka kanisa la kilutheri lililopo katika mwambao wa milima ya Livingstone na hilo kanisa linafahamika kwa jina la Mwakaleli KKKT.

Mzungu huyo alikubali kuitwa Mwakapalila na hata kaburi lake ukitembelea eneo hilo la mission limeandikwa hivyo. Alikubali kwa malengo mawili makubwa.
Lengo la kwanza ni kuendana na mila za Wanyakyusa ambao waliamini sana kwenye utamaduni wa majina katika kuonyesha umoja na ushirika wa mtu katika jamii.

Lakini sababu ya pili, ni ile imani kwamba NAMNA HUELEKEZA MWISHO WA MTU.

Mjerumani yule hakuamini kama angekufa angerudishwa Ujerumani bali angezikwa Unyakyusani. Angezikwa na kuoza kama Wanyakyusa wengine licha ya kuwatawala Indirectly. Akakubali kuitwa Mwakapalila na katika ujenzi wa kanisa la KKKT Mwakaleli alipomaliza kuezeka aliteleza kutoka juu ya bati na kuanguka kisha akafa na kuzikwa kwa heshima zote za Kinyakyusa na mpaka leo kaburi lake linapaliliwa na kina mama wa Kinyakyusa na hutembelewa na Wamisionari wa Ulaya.

NAMNA ILIAMUA HATMA YA MWAKAPALILA KWASABABU FAMILIA ILIAFIKI.

Kwa yanayoendelea nchini, Familia ya mkulu haijishughulishi na namna anavyoenenda Mkulu ili kujua hatma ya afya yake.
Mkulu anatoa milioni tatu na kumpa mwanafunzi, kisha anamwambia KAMPE MWALIMU MKUU, UKAMWAMBIE AKILA HIZI HELA NAYE ATALIWA!

Mwanafunzi anafanya hivyo na kushangiliwa na wasio na hekima, WANAFAMILIA (TISS) hawaoni walakini wa kiafya katika kauli hizi?

Mkulu anaendelea na ziara anakutana na Mkurugenzi aliyekuwa akifanya kazi USA kabla ya kuteuliwa, anaambiwa mbele ya kadamnasi WEWE HUU UPUMBAVU NDO ULIKUWA UKIUFANYA MAREKANI?
Wanafamilia hawaoni udhaifu wa kiafya kwa cheo cha Mkulu katika kauli hizi?

Bado Mkulu anaingia kusini na kukutana na wenyeji mara unasikia NINYI NI VILAZA NA HUU UPUMBAVU MNAOUFANYA SIKUBALIANO NAO.KAMA MMEKULA BASI NANYI MTALIWA

Wanafamilia bado tu mnataka daktari awajulishe nini cha kufanya???

You need to be cautious and attentive all the time and you got a single interest...NATIONAL INTEREST!

Nakumbuka marehemu Mzee Apson Mwang'onda aliwahi kuniambia, "wananitizama vibaya wakisema nambeba Mwandosya lakini mie sipigi kura Mkutano mkuu, lakini sichukii ila najifunza kujari tuhuma nilizokuwa sizijali kabla"
Hiyo ilikuwa mwaka 2005 enzi hizo mie nimetoroka masomoni Zanzibar na kurudi Tukuyu kabla ya kutafutiwa chuo kingine bara.

Wanafamilia mnatakiwa mjifunze kujali tuhuma mlizozoea kuzipuuza ili kuepusha taharuki nchini.
Katika suala la usalama tunazingatia kanuni ya John Dewey mwanafalsafa na muasisi wa mfumo wa elimu wa Marekani kwamba, "LET US DOUBT EVERYTHING"

Kupitia mashaka tunajifunza vingi kuliko vile tunavyohisi tunavijua tukiwa na uhakika. Mkiona kauli tatanishi za Mkulu mna nafasi ya kutia shaka ya kiafya na kuelekeza medical check up kabla hajazidiwa.
Najua kuna wanafamili watakuja DM tafadhari soma mara mbili kabla ya kuja!

#THE MEANS JUSTIFIES THE END#
 
Mtakuja na propaganda gani tena baada ya uzushi wenu kufikia mwisho?

Magufuli hajawahi kubadilika toka awe mbunge 1995 labda km umeanza kumfuatilia baada ya kuwa Rais

Magufuli hana maneno ya pwani yale ya kutabasamu huku moyoni unakinyongo
 
Mada zingine zinashawishi kuchangia hasa muanzilishi akiandika kiufundi na staha namna hii, tatizo mara nyingi mada kama hizi husababibisha jina lako liwe ktk orodha(The List).

Sema nini, tumejuwa mjomba bado yupo sana, tuta agua sana kama waganga wa Firauni enzi za Musa. Mwisho wa siku kama Mungu amependa Musa atufikishe nchi ya ahadi tutafika tu hata akija Joshua kumalizia hii Exodus, mradi Musa katuanzishia safari hii nzuri.

Wakati mwingine fatigue inakuwa ni ugonjwa unaoweza kuleta taharuki kwa wapendwa wetu, husababisha hallucinations,na kutoa kauli tata kama hizo hapo juu.

Mjomba nae anajisahau na kukumbuka lugha zetu zile za mtaani kabla ya kupewa uchifu, kumbe ukiwa chifu kila neno na tukio lako linakuwa na ujumbe wenye tafsiri nzito hata kitabibu, bora kupunguza maneno mengi na matukio.

Mjomba jipe muda wa kupumzika kidogo, ulifikishe hili lori salama nchi ya ahadi, ukilala hapa katikati ya kilele na kona kali za Kitonga imekula kwetu tunao kutegemea.
 
Mtakuja na propaganda gani tena baada ya uzushi wenu kufikia mwisho?

Magufuli hajawahi kubadilika toka awe mbunge 1995 labda km umeanza kumfuatilia baada ya kuwa Rais

Magufuli hana maneno ya pwani yale ya kutabasamu huku moyoni unakinyongo
Unajua chochote kuhusu being democratic upon your own opinion?
And the definite meaning of that state of mind?
And the Dos and Donts of top figures during tough moments?

Kuna vitu haijalishi umezaliwa navyo au umejiendekeza at a certain point you must be controlled for the national interest. Na kusaikolojia aina ya maneno yako inatosha kutufanya sisi tukuelekeze ufanye nini tukiwa kama Wanafamilia.

No matter what, mwanafunzi kwenda kumwambia mwalimu wake kwamba UKILA HII HELA BASI NAWE UTALIWA ni walakini.
You don't need to train learners that your trainers aren't innocent out of your orders...
Kama hii angle hauijulii upo kikada zaidi tafadhari pumzisha ubongo kesho uamke na kuunga juhudi!
 
Nimesema sana kuhusu kauli za Magufuli kuwa hazina staha ya kirais.

Watanzania wengi wanaonekana kukubali tu na kuacha standards zianguke, wengine wanapata ruhusa kushusha standards across the board, kwa sababu rais, ambaye ni "model Tanzanian" anaonekana kushusha standards.

Bora na wengine waone na waseme kuhusu hili.

Mengine mtalaumu wasaidizi sana, lakini mtu mzima akijinyea na kujikojolea mwenyewe wasaidizi mtawaonea tu.
 
Back
Top Bottom