Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ivunjwe na kuundwa upya

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Kiuhalisia imeshindwa kazi halisi ya yanayopaswa kufanywa na kurugenzi hiyo na kubaki kama idara ya itikadi na uenezi ya chama.

Tukio lililo ikumba nchi kwa siku tatu na kuleta tahayari na utengano lingeweza kuzuiwa kiweledi kama kurugenzi hiyo ingeamua kuilinda Ikulu na mambo ya aina hiyo, badala yake Mkurugenzi Gerson Msigwa anajiingiza naye kwenye mambo ya kivijembe vijembe kama watu wa mtaani.

Badala ya kuwa kitengo cha sifa na mapambio wanaweza kuingia deep zaidi kuisemea Ikulu na Urais kama taasisi kamili na yenye watu wengi muhimu na majukumu tofauti tofauti.

Hawabuni hata vipindi kufundisha vijana nini hasa mpangilio wa kazi ndani ya maeneo ya Ikulu na ofisi zake kiasi cha kuwavutia vijana kuja kufanya kazi Ikulu tofauti na sasa wanajua kuna Rais na kazi ni kuteua na kutumbua tuu.

Wakati huu ni muhimu kufanya mabadiliko kwani Msigwa inaonyesha sio size yake tena
 
Acha wivu mkuu why should Msigwa respond to uzushi wa mafisadi?He is more than that!
Nchi inahitaji maendeleo na uwajibikaji...sio upuuzi wa ushuzi na uzushi.
Gerson Msigwa Relax and act professionally kama unavyofanya.

Achana na majuha kalulu tuhangaishane nao!
 
Wamekusikia ila sizani kama wataufanyia kazi ushauri wako, hata mimi ningekuwa kama wao ningekusikiliza lakini nisingeufanyia kazi ushauri wako, pole sana
 
Sasa kama kila uzushi unautolea maelezo mbona you will loose your focus na adui atakuwa kashinda
 
wewe badala ya kuivunja kurugenzi ya kigogo, iliyotuaminisha rais kalazwa ujerumani, unaongelea ya rais iliyo tunza siri
Nimekuelewa vizuri, ingawa umeogopa kufunguka zaidi kwani utashambuliwa.
Nasisitiza haya yote yamesababishwa na ukimya wa kutokujua wafanyeje. Mbona mambo mengine hawakawii kujibu? Kwani kama aliugua kwa uchovu wangesema kulikuwa na shida gani?
 
Kurugenzi ya ikulu haina kazi ya kujibu kila uzushi wa malofa chadema
Bado unarudi kulekule kuleta uchama kwenye mambo ya maana.
Ungejua kuwa haohao wanaccm ambao ndio wenye nafasi za juu ndio waliokuwa mstari wa mbele kuomba hadithi hii iwe kweli lakini walifunga midomo usinge bwabwaja hata kidogo. Na sababu zao ziko wazi, walio hatarini zaidi kimaslahi ni wanasiasa wa ccm kuliko wengine
 
Kiuhalisia imeshindwa kazi halisi ya yanayopaswa kufanywa na kurugenzi hiyo na kubaki kama idara ya itikadi na uenezi ya chama.

Tukio lililo ikumba nchi kwa siku tatu na kuleta tahayari na utengano lingeweza kuzuiwa kiweledi kama kurugenzi hiyo ingeamua kuilinda Ikulu na mambo ya aina hiyo, badala yake Mkurugenzi Gerson Msigwa anajiingiza naye kwenye mambo ya kivijembe vijembe kama watu wa mtaani.

Badala ya kuwa kitengo cha sifa na mapambio wanaweza kuingia deep zaidi kuisemea Ikulu na Urais kama taasisi kamili na yenye watu wengi muhimu na majukumu tofauti tofauti.

Hawabuni hata vipindi kufundisha vijana nini hasa mpangilio wa kazi ndani ya maeneo ya Ikulu na ofisi zake kiasi cha kuwavutia vijana kuja kufanya kazi Ikulu tofauti na sasa wanajua kuna Rais na kazi ni kuteua na kutumbua tuu.

Wakati huu ni muhimu kufanya mabadiliko kwani Msigwa inaonyesha sio size yake tena

Sio kurugenzi ya kumjibu kigogo ivunje kiss uzushi?
 
We ni mjinga msigwa aanze kuwajibu wale wapuuzi wanaozusha matapishi
Hivi unadhani hayo matapishi hayajaleta athari katika maisha ya kawaida na ya kikazi ya mheshimiwa Rais? Mbona mnajibu kihuni huni wakati hata hotuba yake ya Leo inaonyesha wazi kaathirika?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom