Kurudishwa payroll ya Serikali

ulanzi mtamu: Nijibu maswali yafuatayo ndio nikusaidie.

1.Wakati unaondoka

(a)Uliaga? Au kupewa ruhusa na mwajiri wako?..na document ya kuthibisha hilo unayo?

(b) Kama hapo (a) hukufanya hayo;- je uliendelea kulipwa mshahara wako wakati haupo kazini??

2. Unabarua yeyote ya taarifa juu ya kuachishwa kazi na mwajiri wako au kuondolewa kwenye payroll?

Jibu kisha niendelee kukupa mbinu za kupata haki zako.

Koz binafsi niliondoka kazini na nimerudi bila wasiwasi...wao ndio hawakufuata sheria na taratibu. Nilipotea kwa siku zaidi ya 4000.

Toa majibu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Ni ngumu kweli kweli ina mchakamchaka wake ni hatari sana nahitaji moyo. Sema labda kwa waalimu kwa kuwa mnahitajika. Kwa fani nyingine yaani ni nyodo kwa kwenda mbele. Jaribu bahati yako.
 
Toa majibu mkuu.

1. a/ Mwaka 2007 niliajiriwa wilaya ya kongwa kama mwalimu wa leseni,mwaka 2009 nikaomba kwenda kusoma diploma ya ualimu,ila mie nikaenda kusoma advanced diploma ya ugavi pale TIA.
b/Nimelipwa mishahara yangu mpaka nilipomaliza masomo yangu na kurudi kazi na mkuu wangu wa shule akanipokea ila afisa elimu na afisa utumishi wakaniambia mie mtoro kazini.
2.Sina taarifa yoyote ya kuachishwa kazi na mwajiri na zaidi ya hapo documents zote zimenyofolewa kwenye file la afisa utumishi na yeye anasema ni mgeni, yule wa mwanzo alisha hama..
 
Ni ngumu kweli kweli ina mchakamchaka wake ni hatari sana nahitaji moyo. Sema labda kwa waalimu kwa kuwa mnahitajika. Kwa fani nyingine yaani ni nyodo kwa kwenda mbele. Jaribu bahati yako.

nimeenda mpaka nimechoka na ajira mpya inaonyesha wanakataa, wanadai tayari nimeshaajiriwa.
 
cha kufanya rudi halmashauri ulipokuwa unafanya kazi onana na afisa utumishi ongea nae mweleze black and white course cku hzi issue ya kumrejesha mtumishi kwenye payrol lina complication fulani kwani ma approver PO-PSM wanasumbua sana tofauti na zamamini but ikishindikana kukurejesha nenda sehemu uliyopata kaz ongea na afira utumisg kuna naona ya kufanya atakusaidia
 
nimeenda mpaka nimechoka na ajira mpya inaonyesha wanakataa, wanadai tayari nimeshaajiriwa.
Hakika utachoka. Nakuambia kuna ndugu yangu alikuwa ameajiriwa na serikali akaacha kazi na akaingia taasisi nyingine ya serikali. Imagine kurudisha ile check number yake wamekataa. Wanataka kibali toka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Wanasema ili urudi ni lazima uwe na rare profession kitu ambacho si rahisi. Wanadai ulipoondoka nafasi yako ilishajazwa. Pole sana. Ila kama inawezekana waambie wwakupe mkataba ila nako ni tabu maana kuna waraka wa serikali wa mwaka 2009 unakataza ajira za mkataba kwa walio chini ya miaka 45.
 
cha kufanya rudi halmashauri ulipokuwa unafanya kazi onana na afisa utumishi ongea nae mweleze black and white course cku hzi issue ya kumrejesha mtumishi kwenye payrol lina complication fulani kwani ma approver PO-PSM wanasumbua sana tofauti na zamamini but ikishindikana kukurejesha nenda sehemu uliyopata kaz ongea na afira utumisg kuna naona ya kufanya atakusaidia

Asante sana buso kwa ushauri,ila wana katisha sana tamaa kwa maana urasimu ni mwingi na wengi wetu hiyo pesa ya nauli ni ishu kuipata, MUNGU ATUONGOZE kwa maana kumwona katibu mkuu kiongozi pale ikulu ni ishu labda kutuma barua...
 
hata issue za secondment ni kazi kweli unaweza pewa ruhusa ya bila malipo na mwajiri wako kwa ajili ya kwenda kufanya kazi ya mkataba kwingine lkn kurudishwa kazini itategemea kama nafasi yako bado ipo wazi, kama imejazwa na mtu inakula kwako.
 
Ila huna ujanja zaidi ya kuongea na Afisa utumishi wa huko ulikokuwa ili ufanikishe mambo yako.
 
ulanzi mtamu: Sheria ya Utumishi inasema, mwajiriwa akipotea kazini kwa muda wa siku tano mfululizo bila taarifa anatakiwa afukuzwe kazi.

Lakini kufukuzwa kazi huko kunaenda kisheria sio kufukuzwa tu kama ulivyofukuzwa wewe.

Sheria zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kufukuzwa.

1. Kuandikiwa Charge sheet (Hati ya mashtaka ya utoro kazini)..ambayo inatakiwa wakuandikie immediately baada ya hizo 5days za utoro wako. Hiyo ni kwaajili ya kujitetea ulikua wapi....kisha wanaunda kamati isiyozidi watu wanne wenye vyeo vikubwa zaidi yako, wanakuita na kukuhoji kama unakosa au la.

Nb: hati ya mashtaka lazima ikupate na sharti watumie njia sahihi ambayo ni lazima uipate.

Mfano wakati upo chuo, wangemtumia mkuu wa chuo then unaitwa na kukabidhiwa. Hua inakua inform of confidential.

Aaah..nimechoka kuandika...nitaendelea badae kukupa hints....utashida bro ukikomaa. Simple sana kesi yake.
 
Last edited by a moderator:
Wadau mimi tangu 2007 nimeajiriwa katika halmashauri ya Biharamulo kama mwalimu.2012 niliamua kuondoka kituoni na nkaenda shule ya private hapa Mwanza,mwaka jana kuna kazi ya ualimu katika mojawapo ya shule za mashirika ya umma ilitangazwa na tume ya ajira nikaomba na nimepata kazi.

Tatizo walipoenda kuniingiza kwenye system ikaonekana nshaajiriwa serikali.Kwahyo natakiwa kurudi Biharamulo na kuomba nirudishwe payroll na nihamishe datasheet.

Je wadau ni njia gani nyepesi nitumie ili nifanikiwe katika hili na ukizingatia niliondka kazin kwa kukimbia mazingira magumu.
Siku nyingine ili kuepuka matatizo kama haya muwe mnaaga tu kisheria, msitoroke. Utaratibu ni kuandika barua ya kuacha kazi mwezi mmoja kabla au kama ni 24 hrs unaacha mshahara wako wa mwezi mmoja basi, unatolewa kwenye system zao. Ikiwa baadaye utaajiriwa tena serikalini kunakuwa hakuna tatizo kurudi kwenye payroll.
 
duuh kazi kweli kweli, mimi niliacha huko 2006 nipo kwenye mishe mishe zangu binafsi, nina mpango wa kurudi GOVERNMENT 2016 sijui kama watakuwa na kumbukumbu zozote!
 
2006 uko safe...kuna sheria ilipitishwa 2010 ndio inatutesa.

Sure mkuu, ila pia kama alikuwa na check number itakuwaje? Maana kama atatumia jina lile lile wakienda katika system ya payroll na mengine itasoma japo itakuwa haiku active. Ila hakika kwa sasa wanabana sana.
 
We Zogwale utakua na matatizo ya akili.Nahisi Utakua umemeza kitu chenye ncha kali....kina kusumbua kukitoa matakoni.

Ushauri wangu: Usitumie nguvu kujibu hoja. Unajua maana ya Shame on??

Nadhani bnyanya hakukosea kukwambia " we utakua na minyoo si bure!!!"

Acha kuharibu threads za watu kwa upuuzi wako na mambo yako ya kitoto.

Vitu vyenyewe unavyochangia kwanza ni pointless. Pumba tu!!!

We utakua na minyoo si bure...Bwahahahahhahaha
 
Next .....................thread za watu nilizoharibu ni zipi? Wenye thread zao waje hapa waniulize. Ninaamini wewe ni bnyanya uko kivingine. Karibu sana poromosha matusi ya nguvu. Fanya haraka unachelewa. Huwezi kushindana na mimi kwa hoja. Katafute wa matusi wenzako vijiweni mkatukanane!!! Kwangu umepotea njia. Poromosha, ruksa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom