Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 31,292
- 31,448
Leo basi la Shabib VIP la saa 8 toka Dar (Shekilango) kwenda Dodoma, abiria walitakiwa wabadirishiwe basi na walitakiwa walifuate Stendi ya Magufuli, Mbezi. Sijui kama walifanikiwa kusafiri au la. Ila mkatisha tiketi (mdada) pale Shekilango alikiona cha moto.
Jana, basi la Buti la Zungu la saa 8 mchana toka Mtwara kwenda Dar nalo, kwa sababu ya uchche wa abiria, mmiliki aliamua kutoruhusu basi na maamuzi yakawa abiria warudishiwe nauli zao. Baadhi waligoma na mawakala wakawapeleka mnazi mmoja ili wapakiwe kwenye mabasi yatokayo Masasi. Zoezi hili lilishindikana. Baadhi walisafiri kwa magari binafsi yaliyowakuta pale.
Nina maswali haya, kwa mwenye kufahamu;
1. Endapo basi husika halitasafiri kwa sababu yoyote, kurudishiwa nauli pekee kunatosha kumfanya mmiliki awe amemaliza jukumu lake?
2. Kuna abiria huwa wametoka walikotoka kwa nia ya kuunganisha safari siku hiyo, anaporudishiwa nauli, nani anatakiwa abebe gharama za siku za ziada zilizotokana na mmiliki kutoruhusu basi kusafiri?
3. Kubadilishiwa basi, kisheria imekaaje?
Naomba kueleweshwa