Kurudishiwa nauli baada ya basi kusitisha safari

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
31,275
31,404
Leo basi la Shabib VIP la saa 8 toka Dar (Shekilango) kwenda Dodoma, abiria walitakiwa wabadirishiwe basi na walitakiwa walifuate Stendi ya Magufuli, Mbezi. Sijui kama walifanikiwa kusafiri au la. Ila mkatisha tiketi (mdada) pale Shekilango alikiona cha moto.

Jana, basi la Buti la Zungu la saa 8 mchana toka Mtwara kwenda Dar nalo, kwa sababu ya uchche wa abiria, mmiliki aliamua kutoruhusu basi na maamuzi yakawa abiria warudishiwe nauli zao. Baadhi waligoma na mawakala wakawapeleka mnazi mmoja ili wapakiwe kwenye mabasi yatokayo Masasi. Zoezi hili lilishindikana. Baadhi walisafiri kwa magari binafsi yaliyowakuta pale.

Nina maswali haya, kwa mwenye kufahamu;

1. Endapo basi husika halitasafiri kwa sababu yoyote, kurudishiwa nauli pekee kunatosha kumfanya mmiliki awe amemaliza jukumu lake?

2. Kuna abiria huwa wametoka walikotoka kwa nia ya kuunganisha safari siku hiyo, anaporudishiwa nauli, nani anatakiwa abebe gharama za siku za ziada zilizotokana na mmiliki kutoruhusu basi kusafiri?

3. Kubadilishiwa basi, kisheria imekaaje?

Naomba kueleweshwa
 
Tiketi ndiyo mkataba kati ya abiria na msafirishaji.

Sasa tuambie, tiketi inasemaje kuhusu kampuni kusitisha safari?

Kumbuka tiketi ni aina ya mkataba ijulikanayo kama unilateral contract yaani mkataba ambao masharti yake yamewekwa na upande mmoja (mmiliki) na hayana mjadala wala marekebisho. Kwa hiyo ukishalipa nauli na kupewa tiketi maana yake umekubaliana na masharti na vigezo vya kampuni.
 
Ndio maana sipendi sheria, yaani kwenye mkataba mmoja ndio aweke masharti, Sasa mkataba gani unaoegemea upande mmoja
 
Kuna Sheria zingine ambazo zinaweza kukupa haki yako na ukalipwa fidia Ila kufuatilia km wewe pangu pakavu huwezi inabidi ukubari suluba tu, maana hadi ufungue kesi ushachelewa unapokwenda na utaingia gharama kufuatilia kesi na inaweza ikachukua miaka na miaka kutolewa maamuzi, utazungushwa sana kwa kikesi kidogo tu
 
Kama vile ambavyo abiria akihairisha safari yake anakatwa pesa kiasi fulani katika nauli ndivyo inapaswa kwa kampuni pia wakishindwa kusafirisha abiria inabadi wafidie usumbufu huo kwa asilimia fulani.
Seconded
 
Ndio maana sipendi sheria, yaani kwenye mkataba mmoja ndio aweke masharti, Sasa mkataba gani unaoegemea upande mmoja

Ndiyo maana nikasema hiyo ni moja ya aina ya mkataba. Mwenye gari ameandaa masharti(tiketi) na iwapo huafikiani nayo, achana nayo nenda kapande basi lingine.
 
Tunaonewa kwa kutojua sheria, niliwahi pata kadhia nikiwa nasafiri basi likaharibika saa 2 asubuhi, mhudumu(wa kike) na mtoto wa mwenye gari(alijitambulisha baada ya basi kuharibika) wakasepa na gari nyingine kwa ahadi ya kua wanafata spare mjini na watakuja na fundi(sijui ilikuaje gari lilitembea bila fundi in the first place), sijui Hawa wajinga walienda kutiana maana tulikaa mpaka jioni hawajarudi, watu wakamzonga dreva akakomaa kua hata yeye Hana la kufanya maana hawapokei simu zake!!

Tukashirikiana tukapata namba za RTO wa mkoa ule, akaja baada ya kama lisaa na huyu jamaa(mtoto wa mwenye gari) akawa kafika atakua walimsanua kua kimenuka! Kufika huyu mtoto anamuomba RTO waongee pembeni, jamaa akagoma akamwambia ongea hapa hapa wakuskie na Hawa, hapo ishakua kama saa Moja!

RTO: "umewapa abiria wako breakfast na lunch kipindi wanasubiri mnatafuta spare?"

Jamaa: "hapana"

RTO: " sheria inasemaje? "

Jamaa: kimyaa...

RTO:" sasa bwana, hebu tafuta usafiri mpaka mji wa karibu kwa gharama zako, tukifika tunaenda hotel abiria wote wale watakachotaka kwa gharama zako, afu wataftie gari mbadala iwapaleke huko waendako ntawaandikia kibali, ukikosa gari ntawapeleka lodge hata kama ni 5 wote watalala kwa gharama zako mpaka asubuhi utapowatafutia usafiri"

Aisee asikuambie mtu, chini ya escort ya yule RTO tulipata gari mpaka mjini tukaenda hotel Moja watu wakaogelea kuku na soft drinks bila kulipa chochote(mwenye gari alilipa) na jamaa alitafuta gari tukasafiri tukafika asubuhi

Nilijifunza kitu, sheria za kuwabana zipo na ni nzuri tu ila shida ni mbili tu
1) Rushwa.. wanaosimamia sheria wakipewa chochote wanawatetea wenye magari... Kongole sana yule RTO I hope umepanda hata cheo maana sio kwa msimamo ule
2) Abiria wengi hatujui haki zetu
 
Mkuu hii sio rocket science, na hakuna sheria hapo iliyowasaidia hapo, msaada hapo ulitoka ka RTO na sio wa kisheria ILA wa wenye bus kuogopa mamlaka (Tanzania ndivyo ilivyo, tunaogopa watu wenye mamlaka na sio sheria),asingetokea huyu RTO, mngekiona cha moto, next time wenzetu wanafanya push back 🔙, choma moto hilo bus, ujumbe utawafikia wenye mabus wote
 
Tiketi ndiyo mkataba kati ya abiria na msafirishaji.

Sasa tuambie, tiketi inasemaje kuhusu kampuni kusitisha safari?

Kumbuka tiketi ni aina ya mkataba ijulikanayo kama unilateral contract yaani mkataba ambao masharti yake yamewekwa na upande mmoja (mmiliki) na hayana mjadala wala marekebisho. Kwa hiyo ukishalipa nauli na kupewa tiketi maana yake umekubaliana na masharti na vigezo vya kampuni.
watu kama nyiyi ndio tunao wataka hapa jf
 
Back
Top Bottom