Kurithishana Chuki katika Jamii Yetu..

Kurithishana Chuki katika Jamii Yetu..

Nawaacha kivyao..
Dawa ni kujiweka mbali nao wamalizane wenyewe.
Sasa Mimi mtu hajanikosea lolote naanzaje kumchukia na kumfanya adui yangu?
Nimchukie kisa wewe unamchukia?
Sawa kabisa mkuu,nadhani tunapaswa kuachana na hii tabia
 
Hisia za chuki zina madhara makubwa sana kwenye afya yako, Pia unahitaji kazi kubwa kudumisha chuki. Upendo ni rahisi kuudumisha na bado hisia zake zina faida kubwa kwenye mwili. Chuki mara nyingi huwa inasababishwa na hofu . Maisha yalivyo mafupi kuna haja ya kupoteza muda kwenye hisia hasi zisizo na faida yeyote .
 
Hivi unaanzaje kumchukia mtu ambaye hajakukwaza?!
Adui wa mtu hawezi kuwa adui yangu kamwe, kilichowafanya wagombane hilo halinihusu kabisa!
Halafu mtu huwa unajisikiaje kuishi siku zote huna amani kisa mtu fulani, pataneni muishi kwa amani!
Hilo linafahamika kabisa mkuu,shida inakuja pale Baba hapatani na baba Mkubwa halafu asikie unaenda msalimia,anaona kama unauza siri ya kambi kwa mpinzani...Kwa hali kama hiyo unafanyaje
 
Hisia za chuki zina madhara makubwa sana kwenye afya yako, Pia unahitaji kazi kubwa kudumisha chuki. Upendo ni rahisi kuudumisha na bado hisia zake zina faida kubwa kwenye mwili. Chuki mara nyingi huwa inasababishwa na hofu . Maisha yalivyo mafupi kuna haja ya kupoteza muda kwenye hisia hasi zisizo na faida yeyote .
Chuki umuumiza anayeihifadhi ndani yake....
 
mimi huwa sinunui ugomvi wa mtu au kuongeza maadui na watu ambao hawajanikosea. Cha msingi ni kujitahidi kujua ni nani mwenye makosa katika ugomvi huo na ujue jinsi ya kwenda nae maana huwezi jua ni lini upepo utakugeukia. SIWEZI NUNUA UGOMVI WA MTU, KAMA ALIUANZA BHASI ATAJUA JINSI YA KUUMALIZA BILA YA KUTEGEMEA CHUKI NA SUPPORT ZA WATU WENGINE.
 
Hii tabia anayo dada yangu yaani inanikera balaa, bora ugomvi wenyewe uwe wa maana basi. Mbaya zaidi huyo anayetaka na wewe umchukie utakuta ni ndugu yenu wa karibu
Huyo kweli ni sadist
 
ZINGATIA HII
Rafiki wa adui yako ni adui yako,
Adui wa adui yako ni rafiki yako,
Rafiki wa rafiki yako ni rafiki yako,
Adui wa rafiki yako ni adui yako.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kipindi cha cold war marekani alikuwa na ugomvi na urusi basi kila mmoja akakusanya washirika wake ili wachukiane vizuri
Hiyo hali ndo iliyopo kwenye jamii sasa,tena Marekani ni mfano hai kabisa pale anapokuwa na ugomvi na taifa Fulani......
 
Naongelea hali halisi.hapa nnavotype bifu linaendelea.A akisikia nipo kwa B anachukia...
B akisikia nipo kwa A anachukia
Kuhusu watamalizana lini watajua wenyewe,maana wao ndo wanajua vema waligomban kisa nini.mradi mi sijiweki upande wowote..nakua neutral.
Unajua watamalizana lini?
 
ZINGATIA HII
Rafiki wa adui yako ni adui yako,
Adui wa adui yako ni rafiki yako,
Rafiki wa rafiki yako ni rafiki yako,
Adui wa rafiki yako ni adui yako.

hizi ndio zile za solidarity na kuitana blood kwenye mambo ya kipuuzi ila ukitangaza njaa, hao blood wote wanakukimbia. Dunia ya sasa imejaa unafki sana na ukienda kwa kufuata upepo unapoelekea UTAPOTEA. Cha msingi ni kuwa kama Marekani, Hakuna permanent friends or enemies ila permanent interests, Umezeshwe chuki na kuanza kumchukia mtu ambaye hujui kwenye future mtakutana wapi !!!!... mimi siwezi
 
Back
Top Bottom