Kurithishana Chuki katika Jamii Yetu..

Kurithishana Chuki katika Jamii Yetu..

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2015
Posts
4,507
Reaction score
5,742
Imezoeleka kwenye jamii zetu kwamba mfano baba, mama au rafiki yako akiwa hana maelewano na mtu Fulani basi hutaka hata watu wake wa karibu wasiwe na ukaribu pia na mtu huyo ambaye hana maelewano nae hata kama hawahusiki na ugomvi wao, Je hii hali au tabia ni sahihi? na kama si sahihi utakabiliana nayo vipi ikikutokea au kama ilishawahi kukutokea ulikabaliana nayo vipi....Nakaribisha michango na mawazo yenu.
 
Attachments

  • lexonart-20190322-0006.jpg
    lexonart-20190322-0006.jpg
    79.5 KB · Views: 29
Hii hali ipo sana, kikubwa me naangalia nafasi ya huyo mtu, kwa mfano kama una ugomvi na mama yangu, basi hata kama my mother is wrong I will publicly side with her lakini may be privately ntamwambia.

Kama ni rafiki tu basi itategemea na suala lenyewe wanalogombania. Ilimradi ni hali ipo na inatutokea mara kwa mara.
 
Hii tabia anayo dada yangu yaani inanikera balaa, bora ugomvi wenyewe uwe wa maana basi. Mbaya zaidi huyo anayetaka na wewe umchukie utakuta ni ndugu yenu wa karibu
 
Ni jambo linaloleta changamoto sana,katika jamii yetu
 
Hii tabia anayo dada yangu yaani inanikera balaa, bora ugomvi wenyewe uwe wa maana basi. Mbaya zaidi huyo anayetaka na wewe umchukie utakuta ni ndugu yenu wa karibu
Pole sana mkuu, sasa unakabiliana nayo vipi hiyo hali
 
Me nawaachiaga ugomvi wao me simchukii mtu sababu chuki huleta stress
Unadhani upande mmoja utajisikiaje pale unapoona upo karibu na adui yake,let's say mpenzi wako kagombana na mtu Fulani halafu unaendelea kucheka na huyo mtu.....
 
Inabidi ujiweke mbali mkuu, kwa sababu ni utanuniwa, utasemwa na kuambiwa maneno mazito mpaka ulie. I love my sister ila hii shida yake inanitia wazimu
Unajiweka mbali kwa kujifanya kiziwi na kipofu au hahaa
 
Back
Top Bottom