Kurithishana Chuki katika Jamii Yetu..

Kurithishana Chuki katika Jamii Yetu..

Hii tabia inaathiri sana mahusiano kwenye familia.tubadilike.
Kila mtu abebe furushi lake,una ugomvi na mwafulani ubebe mwenyewe,siwezi mchukia kisa wewe humpendi au una bifu nae.nami ukiongea na adui yangu sina shida mradi haina madhara.lakini kama inaleta madhara nakuweka mbali.
 
ZINGATIA HII
Rafiki wa adui yako ni adui yako,
Adui wa adui yako ni rafiki yako,
Rafiki wa rafiki yako ni rafiki yako,
Adui wa rafiki yako ni adui yako.
Sasa mkuu,ina maana utakuwa unafuata hiyo kanuni bila kujua chanzo cha huo uadui....
 
Hii tabia inaathiri sana mahusiano kwenye familia.tubadilike.
Kila mtu abebe furushi lake,una ugomvi na mwafulani ubebe mwenyewe,siwezi mchukia kisa wewe humpendi au una bifu nae.nami ukiongea na adui yangu sina shida mradi haina madhara.lakini kama inaleta madhara nakuweka mbali.
Upo sahihi kabisa mkuu, shida inakuwaga pale upande mmoja unashinikiza wewe usiyehusika uungane nae...
 
tangu lini mtu akakosea kumchukia mtu??
Mfano mdogo mkuu,demu wako kakopa sehem hakukuambia sasa kwenye kudaiwa hataki kulipa wakaanza gombana na mdai wake,ina maana na wewe hutoelewana na huyo mtu? Maana utakuwa hujajua sababu we utamchukia tu kisa demu wako anamchukia
 
Nawaacha kivyao..
Dawa ni kujiweka mbali nao wamalizane wenyewe.
Sasa Mimi mtu hajanikosea lolote naanzaje kumchukia na kumfanya adui yangu?
Nimchukie kisa wewe unamchukia?
Upo sahihi kabisa mkuu, shida inakuwaga pale upande mmoja unashinikiza wewe usiyehusika uungane nae...
 
Hivi unaanzaje kumchukia mtu ambaye hajakukwaza?!

Adui wa mtu hawezi kuwa adui yangu kamwe, kilichowafanya wagombane hilo halinihusu kabisa!

Halafu mtu huwa unajisikiaje kuishi siku zote huna amani kisa mtu fulani, pataneni muishi kwa amani!
 
Back
Top Bottom