Kama atarisiti mwambie aache mchezo kabisaa, mimi ni mfano hai. Nilipata Credit moja ya Kiswahili 2010, nikarisiti masomo 3 mwaka 2011 kutafuta Credit 2. Huwez kufaulu kama hujui sababu iliyofanya ufeli. Nilijua sababu ilofanya nifeli nikaiacha nikawa busy na kitabu. Nilisoma zaidi ya kusoma na wakati huo nasoma masomo ya Form 5 huku narisiti (Yaani unasoma Form 5 huku unarisiti ili ukipata credit unaunga kidato cha 6 lakn usipopata credit safari inaishia hapo hakun kwend form 6). Ratiba yangu ilikuw hivi; Saa 1:00 nipo shule ndani ya geti nazama maktaba napiga msuli mpaka wanapofunga maktaba 12:30Jion hapo sijala napiga tu maji ya kunywa. Nikrud nyumban nakula ikifika 2:00 msul mpaka 5 naingia kulala naamka saa9 napga msuli hadi saa11:30 nalala kisha saa 12:30 najiandaa kwend shule. Hapo pote napitia Past Papers za nyuma kwa umakini mkubwa mno na kupiga test za shule. Mungu saidia nikapata Credit 2 kati ya masomo 3 niliyorisiti na sasa nimehitimu Chuo Kikuu.