Kurekebishana: Lema badilika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kurekebishana: Lema badilika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Jul 2, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Mimi ni kijana ambaye kwa sasa nina makazi nje ya nchi lakini ni kijana niliyekulia Arusha. Nilipoenda Arusha mwezi wa tatu kuna vitu ambavyo sijafurahia. Kwanza ni kile kitendo cha Lema kuwaambia watu sokoni wafanye wanachotaka na hivyo kufanya watu kuanza kuuza vitu barabarani bila utaratibu wa mji.

  Pamoja na kuwa na demokrasia haina maana watu wa mipango ya mji wapuuzwe ni lazima kuwe na utaratibu wa kufanya biashara na kufungua vigenge. Vilevile kuhusu sehemu nyingine za maandeleo kama sehemu za kujenga masoko ya kisasa na miji ya kisasa. Ni kweli kwamba kama mbunge Lema anatakiwa kuhakikisha hakuna kufukuzwa watu kwenye maeneo lakini ni lazima vilevile Lema ahakikishe ujenzi na maendeleo ya mji wa kitalii Arusha unafanyika.

  Malalamiko ya wananchi ni muhimu lakini huwezi kufurahisha kila mtu mmoja mmoja utakiwa uangalie Project na manufaa ya Arusha kwa ujumla. Vilevile Lema unatakiwa ujihusishe zaidi kwenye kutangaza Arusha nje ya nchi, kwenye balozi, na kufanya kazi na wizara ya utalii maana wana zile contact za groups za kifaifa za wageni lakini sijawahi kukusikia unafanya chochote. Kwenye Meeting ya Diaspora ya Marekani na uingereza ungekuja kutangaza Arusha maana wewe ni mbunge wa mji ambao unategemea utalii lakini sijakuona mwaka jana pale Virginia ingawa kulikuwa na watu wengi wa kampuni ya utalii.

  Sijawahi kusikia Lema unafanya mkutano na wafanyabishara wote wa Utalii na biashara nyinginge Arusha na kuwauliza shida zao ni zipi Arusha ni mji wa biashara hivyo huwezi kuongelea chadema pekee.

  Pamoja na ukweli kwamba umefanya kazi nzuri ya kueneza chama Arusha ni wakati wa kuongea biashara na kusaidia kuleta maendeleo Arusha.
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Angefanya mkutano na wafanya biashara si mgesema ana wambia wasilipe kodi!?

  Mmefanya mtakavyo kaondoka sasa hivi unalalamika.

  Umefanya uchunguzi gani ukagundua Lema ndio amewambia wapange bidhaa barabarani?

  Lete ushahidi kiduchu basi kuthibitisha maneno yako!
   
 3. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Eti "mimi ni kijana ninaekaa nje ya Nchi" Si ndio maana uko nje ya Nchi Usituchefue! Kabla hatujakutukana unyamaze! Maana watu Dhaifu kama wewe hatuwataki humu. LIWALO NA LIWE!!
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa atakua ndio kati ya wale wakimbizi waliokimbilia Summer Camp!
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  wewe foreigner hiyo kazi kama wameshindwa wakusanya kodi(wizara ya utalii)unataka aifanye lema aliyekuwa anahujumiwa kila siku..come back home acha blahblah ukiwa unacheza snow fight na mkeo/mmeo huko ughaibuni,..nchi inahitaji ukombozi hii
   
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Popularity stunt! Ulikuwa wapi kusema kipindi kile mpaka baada ya miezi mitatu ndo unajitokeza,unatafta umaarufu?
   
 7. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao huwa hawaguswi ni wateule
   
 8. m

  massai JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hoja dhaifu sana, unakaa nje ya nchi nani anataja kujua unakaa wapi? Hao wachuuzi waende wakafanye shughuli zao wapi?maeneo yote yameuzwa kinyemela.

  Makampuni yote makubwa yakitalii ni ya hao wezi walioko serekalini unategemea lema ataenda kubadili nini pale,anyway alikua na mipango mizuri sana kugusu mji wa arachuga alakini baba mwanaasha kwa udhaifu wa uongozi wake akaona hapana lema hafai.

  Kwa taarifa yako arachuga hata ukiweka soksi ya jeykei na lema au hata na mtu yeyote pale Arusha ni chadema tu.eti uko nje ya nchi acha zakizamani hizo, watu pasport zimechafuka lakini tupo nyuti wala hatuna mbwembwe hizo za kizamani.
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Unamrekebisha kama mb au mjumbe wa halmashauri kuu CDM?
   
 10. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hiyo nchi unayoishi labda ni Somalia...
   
 11. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  we kazi ya lema kabla ajawa mbunge unaijua? Then hata mimi ningekua yeye ningewaruhusu coz nch wanaendesha kihun wenye nacho wanapewa kipaumbele
   
 12. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hoja zingine ni mfu.
   
 13. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kamundu endelea kutetea magamba, si unaona mwenzio Kanyasu kaukwaa UDC Ngara?
   
 14. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Na kweli upo nje ya nchi na sii ajabu unajua raisi wa tz ni nyerere. Ila siku nyingine kabla ya kutoa malalamiko yako uliza kwanza wakubwa wako hoja yako kama ipo sawa lema sio mb wa arusha kwa sasa na kama yeye ndio aliwaambia wafanyie biashara barabarani kwanini uongozi wa mji umewaacha.usipende kulalamika bila kufanya uchunguzi wa jambo kama yule aliyetoa hotuba jana jioni.
   
 15. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,204
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mkuu unajitia aibu bure hata kazi za mbunge huzijui pamoja unaishi ngambo kama unahitaji mambo aliyoyafanya lema Arusha omba utapata humu jamvini watu wapo up to date kila wakati.
   
 16. d

  dandabo JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  mod rudisha post yangu! Acha uonevu
   
 17. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  unatafuta tukujibu mbovu mtun'goe kucha sio!
   
 18. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kamanda

  Ama hujui baadhi ya vitu ulivyoviandika au umefanya makusudi kwa nia ya kupotosha kwa malengo unayoyafahamu. With reservation ya baadhi ya maeneo ambayo umeonesha kiasi fulani constructive criticism...kati ya maeneo ya muhimu sana wambayo Watanzania tunapaswa tujue katika elimu ya mpiga kura na elimu ya uraia (note ni vitu viwili vinavyotofautiana na kufanana na kutegemeana wakati mwingi), ni pmoja na majukumu ya mbunge na nini hasa mpiga kura anapaswa atarajie kutoka kwa mwakilishi au mbunge wake.

  Ni mbunge mjinga tu ambaye anaweza kukubali kuona akina mama/vijana wanaofanya biashara katika eneo fulani kama sehemu yao muhimu to make the ends meet, wanaondolewa na serikali kwa nguvu bila kwanza serikali hiyo hiyo kuwa imewajibika kwanza kutenga eneo ambalo ni suitable kufanya kazi zile zile kwa ajili ya manufaa ya wananchi hao.

  Sasa ni suala la kusikitisha tu kuwa hata watu wanaokaa nje kama wewe ulivyojitambulisha hapa unnecessrily, wanalazimika kupewa elimu ya uraia/mpiga kura ndogo kama hii, kuwa serikali ndiyo inapaswa kuhakikisha kuwa mipango miji inakaa vizuri, kuhakikisha hayo yote uliyoyasema yanakuwa attended. Kazi ya Mbunge ni....waweza kujaza nafasi iliyo wazi.

  Lakini pia anachopigania Lema tangu akiwa bado Mbunge wa Arusha Mjini na hivi sasa ni course ambayo hatimaye itamnufaisha kila mmoja, kuanzia hao unaowaita wafanyabishara wa utalii mpaka mama ntilie na baba ntilie wa kijijini.

  It is a fight or rather a struggle for justice, dignity and humanity. Kukishakuwa na masuala muhimu kama haya, hasa utolewaji wa haki, wafanyabishara wako hao watafanya kazi zao vyema kabisa na kujiongezea kipato kadri ya uwezo wao, halikadhalika wale wa pale Kilombero nao watafanya kazi zao na kusomesha watoto wao, kulisha na kuwatibu inapohitajika, bila tatizo lolote.

  Vitu vingine umezungumza hapa trivial kabisa, eti kwa sababu kulikuwa na kampuni nyingi za utalii, basi ulitaka na mbunge awepo!!! Ulikuwa wakati huo, je hakukuwa na majukumu mengine, je angeenda kama nani, je aliombwa/alikwa akakataa, je wanaopaswa kufanya kazi hiyo ya kuitangaza Tanzania, not only Arusha (na wanakula mishahara kwa kazi hiyo), katika masuala ya utalii wamesaidiaje so far mpaka sasa hapa ambapo bado tunagombania Mlima Kilimanjaro na wenzetu wa Kenya, huko nje ya nchi. Miaka 50 baada ya uhuru!

  Hivi miaka 50 baada ya uhuru Tanzania bado ni taifa ambalo serikali yake haikuwahi kufikiria miaka mingine hamsini masoko yatakuwa wapi, huduma zingine za msingi za kijamii zitakuwa wapi, hata barabara hawakujua kama zitahitajika kupanuliwa n.k,n.k,n.k. Magamba bwana. Fanyeni kazi zenu. Timizeni wajibu, wachenio kulia lia na kusumbuliwa na CHADEMA-phobia.

  Tulitegemea ungehoji kwa nini Lema alishindwa kuisimamia, kuiagiza na kuishauri serikali kwa muda wote aliokuwa mbunge, badala yake unahamisha wajibu kutoka kwa serikali kwenda kwa mbunge! Lakini pia yapo anayopaswa kufanya mbunge na yeye aliyafanya kwa capacity yake na kama sehemu ya kuwajibika na kutumika kwa jamii. Uliza Arusha watakuambia maana wewe umesema ni mkazi wa huko uliye diaspora. Wasalimie.
   
 19. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  tufanye alisema, enhe kwa hiyo unasemaje?
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  CHADEMA hawakosoleki...
   
Loading...