Mimi ni kijana ambaye kwa sasa nina makazi nje ya nchi lakini ni kijana niliyekulia Arusha. Nilipoenda Arusha mwezi wa tatu kuna vitu ambavyo sijafurahia. Kwanza ni kile kitendo cha Lema kuwaambia watu sokoni wafanye wanachotaka na hivyo kufanya watu kuanza kuuza vitu barabarani bila utaratibu wa mji.
Pamoja na kuwa na demokrasia haina maana watu wa mipango ya mji wapuuzwe ni lazima kuwe na utaratibu wa kufanya biashara na kufungua vigenge. Vilevile kuhusu sehemu nyingine za maandeleo kama sehemu za kujenga masoko ya kisasa na miji ya kisasa. Ni kweli kwamba kama mbunge Lema anatakiwa kuhakikisha hakuna kufukuzwa watu kwenye maeneo lakini ni lazima vilevile Lema ahakikishe ujenzi na maendeleo ya mji wa kitalii Arusha unafanyika.
Malalamiko ya wananchi ni muhimu lakini huwezi kufurahisha kila mtu mmoja mmoja utakiwa uangalie Project na manufaa ya Arusha kwa ujumla. Vilevile Lema unatakiwa ujihusishe zaidi kwenye kutangaza Arusha nje ya nchi, kwenye balozi, na kufanya kazi na wizara ya utalii maana wana zile contact za groups za kifaifa za wageni lakini sijawahi kukusikia unafanya chochote. Kwenye Meeting ya Diaspora ya Marekani na uingereza ungekuja kutangaza Arusha maana wewe ni mbunge wa mji ambao unategemea utalii lakini sijakuona mwaka jana pale Virginia ingawa kulikuwa na watu wengi wa kampuni ya utalii.
Sijawahi kusikia Lema unafanya mkutano na wafanyabishara wote wa Utalii na biashara nyinginge Arusha na kuwauliza shida zao ni zipi Arusha ni mji wa biashara hivyo huwezi kuongelea chadema pekee.
Pamoja na ukweli kwamba umefanya kazi nzuri ya kueneza chama Arusha ni wakati wa kuongea biashara na kusaidia kuleta maendeleo Arusha.
Tumewazoea ninyi, mnafikiri mnajua kila kitu.Kamanda
Ama hujui baadhi ya vitu ulivyoviandika au umefanya makusudi kwa nia ya kupotosha kwa malengo unayoyafahamu. With reservation ya baadhi ya maeneo ambayo umeonesha kiasi fulani constructive criticism...kati ya maeneo ya muhimu sana wambayo Watanzania tunapaswa tujue katika elimu ya mpiga kura na elimu ya uraia (note ni vitu viwili vinavyotofautiana na kufanana na kutegemeana wakati mwingi), ni pmoja na majukumu ya mbunge na nini hasa mpiga kura anapaswa atarajie kutoka kwa mwakilishi au mbunge wake.
Ni mbunge mjinga tu ambaye anaweza kukubali kuona akina mama/vijana wanaofanya biashara katika eneo fulani kama sehemu yao muhimu to make the ends meet, wanaondolewa na serikali kwa nguvu bila kwanza serikali hiyo hiyo kuwa imewajibika kwanza kutenga eneo ambalo ni suitable kufanya kazi zile zile kwa ajili ya manufaa ya wananchi hao.
Sasa ni suala la kusikitisha tu kuwa hata watu wanaokaa nje kama wewe ulivyojitambulisha hapa unnecessrily, wanalazimika kupewa elimu ya uraia/mpiga kura ndogo kama hii, kuwa serikali ndiyo inapaswa kuhakikisha kuwa mipango miji inakaa vizuri, kuhakikisha hayo yote uliyoyasema yanakuwa attended. Kazi ya Mbunge ni....waweza kujaza nafasi iliyo wazi.
Lakini pia anachopigania Lema tangu akiwa bado Mbunge wa Arusha Mjini na hivi sasa ni course ambayo hatimaye itamnufaisha kila mmoja, kuanzia hao unaowaita wafanyabishara wa utalii mpaka mama ntilie na baba ntilie wa kijijini.
It is a fight or rather a struggle for justice, dignity and humanity. Kukishakuwa na masuala muhimu kama haya, hasa utolewaji wa haki, wafanyabishara wako hao watafanya kazi zao vyema kabisa na kujiongezea kipato kadri ya uwezo wao, halikadhalika wale wa pale Kilombero nao watafanya kazi zao na kusomesha watoto wao, kulisha na kuwatibu inapohitajika, bila tatizo lolote.
Vitu vingine umezungumza hapa trivial kabisa, eti kwa sababu kulikuwa na kampuni nyingi za utalii, basi ulitaka na mbunge awepo!!! Ulikuwa wakati huo, je hakukuwa na majukumu mengine, je angeenda kama nani, je aliombwa/alikwa akakataa, je wanaopaswa kufanya kazi hiyo ya kuitangaza Tanzania, not only Arusha (na wanakula mishahara kwa kazi hiyo), katika masuala ya utalii wamesaidiaje so far mpaka sasa hapa ambapo bado tunagombania Mlima Kilimanjaro na wenzetu wa Kenya, huko nje ya nchi. Miaka 50 baada ya uhuru!
Hivi miaka 50 baada ya uhuru Tanzania bado ni taifa ambalo serikali yake haikuwahi kufikiria miaka mingine hamsini masoko yatakuwa wapi, huduma zingine za msingi za kijamii zitakuwa wapi, hata barabara hawakujua kama zitahitajika kupanuliwa n.k,n.k,n.k. Magamba bwana. Fanyeni kazi zenu. Timizeni wajibu, wachenio kulia lia na kusumbuliwa na CHADEMA-phobia.
Tulitegemea ungehoji kwa nini Lema alishindwa kuisimamia, kuiagiza na kuishauri serikali kwa muda wote aliokuwa mbunge, badala yake unahamisha wajibu kutoka kwa serikali kwenda kwa mbunge! Lakini pia yapo anayopaswa kufanya mbunge na yeye aliyafanya kwa capacity yake na kama sehemu ya kuwajibika na kutumika kwa jamii. Uliza Arusha watakuambia maana wewe umesema ni mkazi wa huko uliye diaspora. Wasalimie.
Sasa wewe ulitaka lema aende america akaongee kichaga? mtu hana elimu, anajua nini kuhusu uchumi wakati yeye kapitia biashara za panya road. We hukuona ile picha alivyo chanua kwenye bonet ya gari? Itafute ndio utajua akili yake iko wapi.
Mimi ni kijana ambaye kwa sasa nina makazi nje ya nchi lakini ni kijana niliyekulia Arusha. Nilipoenda Arusha mwezi wa tatu kuna vitu ambavyo sijafurahia. Kwanza ni kile kitendo cha Lema kuwaambia watu sokoni wafanye wanachotaka na hivyo kufanya watu kuanza kuuza vitu barabarani bila utaratibu wa mji.
Pamoja na kuwa na demokrasia haina maana watu wa mipango ya mji wapuuzwe ni lazima kuwe na utaratibu wa kufanya biashara na kufungua vigenge. Vilevile kuhusu sehemu nyingine za maandeleo kama sehemu za kujenga masoko ya kisasa na miji ya kisasa. Ni kweli kwamba kama mbunge Lema anatakiwa kuhakikisha hakuna kufukuzwa watu kwenye maeneo lakini ni lazima vilevile Lema ahakikishe ujenzi na maendeleo ya mji wa kitalii Arusha unafanyika.
Malalamiko ya wananchi ni muhimu lakini huwezi kufurahisha kila mtu mmoja mmoja utakiwa uangalie Project na manufaa ya Arusha kwa ujumla. Vilevile Lema unatakiwa ujihusishe zaidi kwenye kutangaza Arusha nje ya nchi, kwenye balozi, na kufanya kazi na wizara ya utalii maana wana zile contact za groups za kifaifa za wageni lakini sijawahi kukusikia unafanya chochote. Kwenye Meeting ya Diaspora ya Marekani na uingereza ungekuja kutangaza Arusha maana wewe ni mbunge wa mji ambao unategemea utalii lakini sijakuona mwaka jana pale Virginia ingawa kulikuwa na watu wengi wa kampuni ya utalii.
Sijawahi kusikia Lema unafanya mkutano na wafanyabishara wote wa Utalii na biashara nyinginge Arusha na kuwauliza shida zao ni zipi Arusha ni mji wa biashara hivyo huwezi kuongelea chadema pekee.
Pamoja na ukweli kwamba umefanya kazi nzuri ya kueneza chama Arusha ni wakati wa kuongea biashara na kusaidia kuleta maendeleo Arusha.
Ushauri wa kijinga tu
Mkuu hao huwa hawaguswi ni wateule