Kura za Rais kutangazwa majimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura za Rais kutangazwa majimboni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa matokeo ya Rais yatatangazwa kwenye majimbo badala ya kusubiriwa kutangazwa na NEC...

  Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

  Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuondoa hofu kwa wananchi wanaosubiri kujua matokeo.

  Kiravu alisema kuwa NEC imeanza maandalizi ya uchaguzi ujao kwa kujipanga kikamilifu ili kuwepo na uwazi na haki sawa kwa mujibu wa sheria.

  Alisema kwa sasa NEC inaboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura ili iweze kupanga vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi mkuu.

  Alisema kwa mwaka huu vituo vitaongezeka kufikia vituo 55,000 kutoka 47,000 vya mwaka 2005.

  Mkurugenzi huyo alisema asasi za kiraia zikiwemo za walemavu zina wajibu wa pekee wa kuelimisha umma hususan masuala muhimu yanayohusu uchaguzi.

  Kwa mujibu wa Kiravu, uelimishaji huo ni ule unaolenga kumpa uelewa mpiga kura kuhusiana na namna ya kupiga kura, thamani ya kupiga kura, umihimu wa kutunza kadi ya kupigia kura na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

  Alisema walemavu watapewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni watu kama watu wengine na wana haki za msingi na watapatiwa elimu kuhusu namna ya kushiriki katika uchaguzi huo.

  Mkuu wa Mradi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Oscar Harnam, alisema kuwa wamejitolea kwa ajili ya kuwasaidia walemavu kwenye uchaguzi na kuwapatia mahitaji watakayoyahitaji wakati wa uchaguzi.

  Alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 8.2 ni watu wenye ulemavu ambao ni sawa na watu zaidi ya milioni 3 hivyo wanapaswa kushiriki.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kukumbushia tu.. wasije wakabadili mawazo!
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawawezi mkuu Hiki ni kibano toka kwa wafadhili na kilikuwepo toka siku nyingi. Inadaiwa kuwa eti vurugu za kenya zilisababishwa na ucheleweshaji wa kutangaza matokeo.
   
 4. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  First Step to Victory; unbelievable!!
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Kama vile naota!!!!

  Mwaka huu JK atakufa kwa presha

  Kwa hiyo Miraji Kikwete na wahindi wake wanapauka bure??
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hapana wanachojaribu kufanya ni kuwa matokeo yatakapotoka mikoani yakitangazwa yanatangaza mshindi tu wa kura kwenye jimbo hilo.. lakini wakati huo huo lazima yatumwe kwa NEC ambapo yatajumlishwa na jumla rasmi itakapotolewa. Sasa endapo wakijikuta kuwa hali inakuwa ngumu kama jimbo wametangaza kuwa Kikwete kapata 1000 halafu tume ikajumlisha 10000 na kutokana na mahesabu hayo ya tume kikwete akashinda na wakamtangaza basi ndio itakuwa hivyo hakuna mahakama itakayoingilia kati..
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,695
  Trophy Points: 280
  [QUOTE
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa matokeo ya Rais yatatangazwa kwenye majimbo badala ya kusubiriwa kutangazwa na NEC...

  Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

  Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuondoa hofu kwa wananchi wanaosubiri kujua matokeo.][/QUOTE]

  Lililobaki ni kwa NEC kuturuhusu wapigakura kuwathibiti mashushu kwenye vituo vya kupiga kura. Waturuhusu kubaki mita 200 kutoka kwenye vituo vya kuhesabia kura.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahaha.. natamani kingekuwa ni kibano cha wapinzani.. but will take it
   
 9. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Na ikiwa hivyo, kazi ya ukombozi ni rahisi
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hili likifanyika itasaidia sana kupunguza utata katika kutangaza matokeo.
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Ni kweli mbinu zilizotumika Kenya zilianza kwa KUSIMAMISHA utangazaji wa matokeo. Sasa kama kwetu watatangaza majimboni, hiyo ni PLUS. Ila jumuisho la matokeo toka majimbo mbali mbali na kusema nani anaongoza KITAIFA litafanyikaje, na hakuna atakayeweza kusimamisha utangazaji wake? Maana ukisikia wamesimamisha utangazaji wa matokeo ujue kuna wizi.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii imenichekesha sana!!!!!!!!! of course nikicombine na ile ya matokeo ya uraisi kutoka ndani ya siku moja inanipa shida kidogo kuamini na huu sasa ndiyo mtego wa NEC. Inawezekana Kikwete alikubaliana na haya mabo kwa kudhania ushindani kwa kiti chake hautakuwepo kabisa!
   
 13. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii safi sana, itapunguza ile presha kwamba matokea YATACHAKACHULIWA.. labda tusibiri visingizio vingine,,,
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Pamoja na shinikizo la wafadhili, NEC wanajivua lawama mapema.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  TAtizo litakuja baada ya matokeo ya Ubunge yanapotangazwa kwernye majimbona kuwa katikajimbo fulani Dr. Slaa kashinda.. matokeo hayo yakianza kujumlishwa na mtu huru italazimisha Tume kusitisha kwani watu wataanza kusherehekea.... na wakianza kusherehekea guess what will happen? serikali itatuma mapolisi kuwazuia and the rest will be history!
   
 16. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MM,

  Jimbo likitangaza 1000, NEC wakatangaza 10,000 Mahakama zina uwezo wa kutengua maamuzi hayo ikiwa kuna uthibitisho. Na uthibitisho utakuwepo kwa kuwa kura za majimboni zitakuwa zinafahamika hadharani. Unless uniambie maamuzi ya NEC ndo yako juu ya sheria. Sheria inazuia kumshitaki rais lakini inaweza kutengua ushindi wa "Rais."
   
 17. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Nadhani sheria ya uchaguzi inasema matokeo ya urais yakiishatangazwa na tume ya uchaguzi, hayawezi kuwa challenged kwenye chombo kingine kile (hata mahakama)
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Apa kuna kitu CCM wamekubali ilo.
  Basi utakuta wana mikakati mizito ya kuiba kura vituoni.
  TUWE MAKINI VITUONI
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  LAkini pesa za kuwalipa mawakala wasiopungua elfu 55 zipo kwa Vyama hivi ukiondoa CCM? Tupate wapi wazalendo watakao kubali kuwa mawakala hata kama hakuna malipo?
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kwamba hilo la kutangazwa ni hatua muhimu, naona wengi mmeruka kitu kingine ambacho ni cha umuhimu pia na kimedokezwa hapo juu. Nacho ni hii idadi:

  Nadhani NEC wameandika na kuiweka mwisho makusudi kwenye mawasiliano yao, ili ukisoma unakuwa excited na habari ya kuhesabu na kusahau umuhimu wa hili by the time unafika mwisho wa kusoma.

  Tujiulize:

  -- Je, hii idadi ni ya kweli? Je, ina reflect national averages za walemavu hapa nchini?
  -- Je, ni watu wangapi wataongozana na walemavu katika kuwasaidia wafanikishe kupiga kura kwenye vituo?
  -- Je, watu hao nao watakuwa wanapiga kura wakati huo huo?

  Kwasababu Katiba yetu ya Tanzania haielezei aina za ulemavu na kugawa katika makundi bali kijumlajumla tu, je yule aliye mlemavu wa miguu au mikono atapata wasaidizi sawa na yule aliye na ulemavu wa macho?

  Naonesha kusita na hii idadi maana naona inaonekana kukinzana na hali halisi baada ya taarifa za watu zaidi ya millioni tatu kuongezeka kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Hatuchelewi kukuta walemavu waliojiandikisha kupiga kura Tanzania hawazidi laki 6. Ila kuna millioni 3 za watu hewa ambao wametayarishiwa kura tayari na wataingia kama wasaidizi wa walemavu kwenye vituo vya kura, hivyo kuifanya idadi iwe hiyo tunayoambiwa ni 19.6 millioni.

  Tarehe 23-9-2010 Ronald Salanzu (mjumbe anayewakilisha watu wenye ulemavu na mahitaji maalum) na Miriam Ndesanguo ambaye ni mmoja wa wahusika wakubwa katika kuwezesha hili waliongea na BBC Swahili kuhusu hili swala, I wish wangelitaja idadi ya walemavu wakati huo. Inabidi kuwabana nao watoe ufafanuzi zaidi achilia mbali NEC.
   
Loading...