Kura ya Meghji yazua utata mpya

Kura ya Meghji yazua utata mpya

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
meghji-564x272.jpg

Zakia Meghji

Dar es Salaam. Suala la Mjumbe wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Zakia Meghji kupiga kura upande wa Zanzibar wakati wa kupitisha Katiba Inayopendekezwa, limechukua sura mpya baada ya uliokuwa uongozi wa Bunge hilo kusema, "hakuna sehemu yoyote iliyobainisha kwamba alikuwa mjumbe kutoka Bara."

Utata wa kura ya Meghji uliibuliwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba ambaye alisema mjumbe huyo alitakiwa kupiga kura upande wa Bara kutokana na Tangazo la Gazeti la Serikali namba 29 la Februari 7, mwaka huu lililomtambulisha Meghji kama mjumbe kutoka Tanzania Bara lakini katika upigaji kura alipiga upande wa Zanzibar.

Hatua ya mjumbe huyo kupiga kura upande huo wa muungano inachukuliwa na baadhi ya wanaopinga mchakato wa Katiba Mpya kama moja ya mbinu zilizotumiwa na uongozi wa Bunge Maalumu kulazimisha upatikanaji wa theluthi mbili ya kura kutoka visiwani ili kupitisha Katiba.

Hata hivyo, Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk Thomas Kashililah alisema jana kuwa: "Mnajichanganya tu, katika hilo tangazo la Serikali halikubainisha kwamba Meghji ni mjumbe wa Bara sisi tulichoangalia ni originality (asili) yake ni wapi hata kama anaishi Bara," alisema Dk Kashililah na kuongeza: "Kama ndiyo hivyo, mbona Hamad Rashid anaishi Bara lakini asili yake ni Zanzibar? Mbona hilo hamuulizi? Hapo hakuna hoja kama wanatafuta kitu hicho hakipo.

"Katika Bunge hilo kulikuwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wajumbe 201 na wajumbe kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania… ieleweke kwamba mjumbe wa Baraza la Wawakilishi anaweza kuingia Bunge la Jamhuri lakini wa Jamhuri hawezi kuingia Baraza la Wawakilishi."

Muda mrefu ambao Meghji amekaa Bara anaweza kufananishwa na ule ambao Mbunge wa Dole (CCM), Sylivester Maselle Mabumba ameishi Zanzibar lakini wakati akipiga kura kupitisha Katiba, asili ya Mabumba ambayo ni Bara haikuzingatiwa.

Taarifa katika tovuti ya Bunge zinaonyesha kuwa Mabumba alihitimu elimu yake ya msingi katika Shule ya Langoni, Dole – Zanzibar mwaka 1983 na mpaka sasa amekuwa akiishi Visiwani humo licha ya kwamba ni mzaliwa wa Kahama, Shinyanga.

Meghji alipopigiwa simu kuzungumzia suala hili, baada ya mwandishi kujitambulisha kwake alisema: "Unasema unaitwa nani, unasemaje", kisha simu ikakatika na alipopigiwa tena alipokea lakini ilisikika sauti ikisema hasikii na alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakujibu.

Asili yake

Mjumbe huyo ni mmoja wa wabunge wa kuteuliwa na Rais katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na hakuna taarifa zozote zilizoambatana na uteuzi wake kuhusu ni upande upi wa muungano anakotoka. Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa amekuwa akiishi mkoani Kilimanjaro ambako 1990 alikuwa mkuu wa mkoa huo, nafasi ambayo aliipata baada ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi mwishoni mwa miaka ya 1980.

Meghji pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri akiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa miaka tisa, Wizara ya Afya kwa miaka minne na Wizara ya Fedha kwa miaka miwili.
Wizara hizo mara kadhaa zimekuwa zikiongozwa na mawaziri kutoka pande zote mbili za muungano, lakini pia ni nadra kwa kiongozi kutoka Zanzibar kushika wadhifa wa mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya upande wa Bara.

Wasemacho wengine

Mratibu wa Mtandao wa Wanaopigania Haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alisema kitendo kilichofanywa ni kuhalalisha uchakachuaji wa Katiba hiyo.
"Kama mtu ameteuliwa kutoka Bara hata kama ni Mzanzibari atatakiwa kupiga kura kama mtu wa Bara kwani kulikuwa na maana yake kuteuliwa upande mmoja."

Mwanasheria Mwandamizi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema kuna vitu viwili vinatakiwa kutazamwa kwa makini; mosi ni uteuzi wake ulikuwa kutoka wapi na alipiga kura kama mjumbe wa wapi.

"Kama aliteuliwa kama mjumbe wa Tanzania Bara alitakiwa kupiga kura kama mjumbe wa Bara na kama aliteuliwa mjumbe wa Zanzibar angepiga kura kama Mzanzibari na si kuangalia asili yake na hili halina hata haja ya kuumiza kichwa kwani linaeleweka alipoteuliwa ndipo huko atapigia kura," alisema Sungusia.

Chanzo:Mwananchi
 
Huyo katibu wa Bunge ana hoja dhaifu sana na anaonekana mzito kujieleza.

Hivi Hamad Rashid si Mbunge wa Wawi iliyopo Zanzibar? Sasa si lazima angepiga kura kwa Upande wa Zanzibar maana sheria inataka pande mbili za muungano na yeye amekua mjumbe kwa tiketi ya Kuwa Mbunge wa Wawi ya Kule Zanzibar

Huu ni Upuuzi
 
Hawa ndio wale walioongeza idadi ya Wazanzibar toka 210 tuliyotangaziwa awali, mpaka Wazanzibar 219!!!! tuliotangaziwa baada ya kupiga kura

Na bado watajulikana wote, Walivyokuwa Majuha eti wanaangalia "Originality"!!!!!

Kama originality yake ni Zanzibar, Alipataje basi kuwa mkuu wa Wilaya na Mkoa kwa nyakati tofauti ndani ya Ardhi ya TANGANYIKA???? Je huku siko kulalamika tunakolalamika Watanganyika kwamba Wazanzibar pamoja na uchache wao bado wanatutawala na kuchukua Ajira za Watanganyika??

Nasema Maccm Mtatujibu maswali haya muwe mmekufa au mko hai..Hatuwezi kuchezeana akili utafikiri wendawazimu enzi hizi Tunajitambua

Tutaona.......!!!

BACK TANGANYIKA
 
....hapa shida ni nini?,meghji anotoka 201,je jina lake linatoka upande gani wa Tanganyika au Zanzabar,angalieni aliomba kupitia taasisi gani?.Atakamatika tu.....ikija kungundulika kama kamafanya hivyo..duh huyu mkwe atadharaulika na pengine akajipatia maadui wabaya sana.
 
Chezea Intarahamwe wewe!! Hao ndio ccm wamesheheni kila idara. Kwenye ufisadi wamo, ujangili wa maliasili wamo, uuaji wamo, uwizi wa kura wamo, utapeli wamo, uporaji wamo na kila aina ya uchafu unaoujua na usio ujua.
 
....hapa shida ni nini?,meghji anotoka 201,je jina lake linatoka upande gani wa Tanganyika au Zanzabar,angalieni aliomba kupitia taasisi gani?.Atakamatika tu.....ikija kungundulika kama kamafanya hivyo..duh huyu mkwe atadharaulika na pengine akajipatia maadui wabaya sana.

Mkuu huyu mama ni mjumbe toka Wabunge wa Muungano kama sikosei na si kundi la 201

BACK TANGANYIKA
 
Kakke huyo mama ni mzanzibar wa kuzaliwa kama ilivyo kwa wazanzibar wote kuwa wana haki zote za utanzania hivyo anaweza kushika cheo chochote tanzania maana ni mtanzania.

ila kwa mtu wa bara kuwa mznz lazima awe kaishi muda usiozidi 10yrs zanzibar .hapo hakuna utata. sasa huyo mama unasemaje sio mzanzibar kwa vile ameamua kuhamia dar ndio asiwe mznz,wewe uliyehamia huko UK tukuite sio mznz?
au kuna mahali popote kaelezwa kuwa yeye anawakilisha jimbo fulani bara?
hizi hoja za kitoto ndio ccm huwapiga nazo mnabaki mmeduwaa.

AWOTTA: Member: Zakia Hamdani Meghji
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huyu mama ni mjumbe toka Wabunge wa Muungano kama sikosei na si kundi la 201

BACK TANGANYIKA

ni mbunge wa kuteuliwa na rais katika bunge la muungano. ukweli ni kuwa wako waznz wengi tu na wabara wengi wameteuliwa na rais lakini katika uteuzi hasemi kateuwa kutoka wapi wala wapi , sasa kigezo cha anatoka bara au znz kinatoka wapi?
 
Hawa ndio wale walioongeza idadi ya Wazanzibar toka 210 tuliyotangaziwa awali, mpaka Wazanzibar 219!!!! tuliotangaziwa baada ya kupiga kura

Na bado watajulikana wote, Walivyokuwa Majuha eti wanaangalia "Originality"!!!!!

Kama originality yake ni Zanzibar, Alipataje basi kuwa mkuu wa Wilaya na Mkoa kwa nyakati tofauti ndani ya Ardhi ya TANGANYIKA???? Je huku siko kulalamika tunakolalamika Watanganyika kwamba Wazanzibar pamoja na uchache wao bado wanatutawala na kuchukua Ajira za Watanganyika??

Nasema Maccm Mtatujibu maswali haya muwe mmekufa au mko hai..Hatuwezi kuchezeana akili utafikiri wendawazimu enzi hizi Tunajitambua

Tutaona.......!!!

BACK TANGANYIKA

yaani ndugu unaongea kama vile umepagawa au hujitambui. huyu ni mbunge wa kuteuliwa na rais kama alivyo sada mkuya.
 
....hapa shida ni nini?,meghji anotoka 201,je jina lake linatoka upande gani wa Tanganyika au Zanzabar,angalieni aliomba kupitia taasisi gani?.Atakamatika tu.....ikija kungundulika kama kamafanya hivyo..duh huyu mkwe atadharaulika na pengine akajipatia maadui wabaya sana.

Adharaulike mara ngapi mkuu! Keshadharaulika tayari mtu hata kuongea na waandishi wa habari anaona aibu ndo ujue alichofanya sicho anajua ataulizwa maswali amabayo majibu yake utata tupu. Hovyo sana hili limama na walioliteua.
 
....hapa shida ni nini?,meghji anotoka 201,je jina lake linatoka upande gani wa Tanganyika au Zanzabar,angalieni aliomba kupitia taasisi gani?.Atakamatika tu.....ikija kungundulika kama kamafanya hivyo..duh huyu mkwe atadharaulika na pengine akajipatia maadui wabaya sana.

Mkuu, sijakuelewa hapo kwenye Bold, hivi huyu mama sio viti maalumu? Halafu bold No 2, mbona mnamwita mkwe, ni mkwe wa nani kaka?
 
Njia rahisi ya kupata ukweli ni hii.Sikuna ile idadi ya wajumbe wa bunge kutoka bara.Cha kufanya ni kuorodhesha(kuhesabu) majina ya wajumbe hao bila kuingiza jina la Meghji tuone kama ile idadi ya awali ya wajumbe kutoka bara itabaki kama ilivyo.
 
Back
Top Bottom