Habarini wanajamvi. Tukiweka pembeni chuki, majungu, ubaguzi na maslahi ya udini, ukaskazini na uchaga, matatizo ambayo yanaigharimu CDM, Zitto Kabwe ndiye pekee ataweza kuiondoa CCM ikulu. Najua kuna baadhi ya wavuta bhangi humu watakuja na mapovu midomoni na kunipa kila aina ya kashfa, kejeli ama matusi na kudai nimetumwa. Sijatumwa isipokuwa nikipima busara ya Zitto kwa kulinganisha na Mbowe na Slaa nabaini Zitto ana busara. Wakati Zitto ni mvumilivu dhidi ya changamoto za kisiasa, Slaa na Mbowe si wavumilivu wamejawa na jazba na visasi-sifa za viongozi madikteta. Zitto ana uwezo wa kujenga hoja na kuiwasilisha kwa umakini na ushawishi wakati Mbowe na Slaa wana hoja za uzushi zinazowasilishwa kwa maguvu na jazba, wako tayari kutengeneza uzandiki alimradi kutimiza matakwa yao. Zitto anao uwezo binafsi-hakubali kuburuzwa na hoja zenye maslahi binafsi, ni muungwana anayeweza kukiri mafanikio ya chama cha mapinduzi na kukosoa kwa dhati kwa nia ya kujenga. Slaa na Mbowe wameamua kupinga kila kitu hata isivyostahili. Zitto anaikwepa mikakati halamu ya chama chake ambayo haiangalii athari za kubomoka kwa utaifa wetu endapo itatekelezwa. Muda mwingi unaotumiwa na Mbowe na Slaa kupanga mikakati ya kumdhoofisha ZITTO kisiasa ni wazi wanamhofia na its true Zitto anakubalika kwa dhati wakati Slaa na Mbowe wanakubalika kiushabiki tu. Ninaishauri CDM kumsimamisha Zitto kugombea urais na ushindi utakuwa wazi kwani Zitto ni kete ya ushindi CDM. Karibuni kwa michango yenye busara, Note:matusi ni sifa ya mpumbavu.