Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
hadi imerudishwa baada ya kulalamika sana
 
Hakuna hata mmoja anayefaa kati ya hao bora Mnyika anawazidi wote, yupo composed, objective na very reasonable.
 
subiri uone udini wa chadema watakavyomrukia ZITTO. wanajua zitto ni kichwa kupita hata huyo slaa lakini slaa wanampenda kwa kuwa ni PADRI.

wewe utakuwa umetumwa cdm hakunaga udini pale, kama unataka udini nenda cuf. Kama ulishuhudia mkutano wao wa jana na kuona vibarakashia kibao, halafu mbaya zaidi mkutano walifunguwa kwa sara baada ya pastor kuanza kusali wakawa wanamzomea.
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.

Ningelimteua Dr Slaa
1. Uzoefu wake katika mambo magumu ya uongozi
2. Anamwelekeo wa kuikomboa nchi
3. ni mzalendo halisi
4. Ni Mtu mwenye uchungu na Raslimali za nchi yetu kidhati
 
Acha kumfananisha MESSI(Dr Slaa) na Mrisho Ngassa(Zito Kabwe).

Yaani mmekosa kazi ya kufanya CDM? Si mlisema Mnamsubiri Sitta aje ili mumweke awe rais? Zitto ni mtoto sana Atamwongoza nani? juzi amemaliza chuo leo hii Rais, hakika kazi ipo! Yaani nyie cdm ndo bado wengi mnaishi kwenye nyumba za kupanga leo hii mkipewa nchi ndo mnaanza kununua viwanja na kujenga na wala sio kuongoza nchi, Naona mna chezea psychologia za watanzania, Slaa na uzee huu anapamabana na kesi za ndoa, atafanya nini IKULU? THINK TWICE!
 
Ukatae ukubali....ukweli utabaki palepale ZITTO KABWE NI JEMBE huwezi kumfananisha na huyo mzee!siku si nyingi mlikuwa mnamsifu?mmeona anawapa ukweli mmeamua kumharibia....huyo mzee hana lolote mropokaji tu!usidanganyike na makelele tya mikutanoni...angalia FACTS!kwanza hata hizo asilimia hapo juu ni uongo tuuuuu!
 
Kweli Tukiruhusu AKILI NDOGO kutawala akili kubwa tumekwisha.Badala ya Kumpigia Kura Zitto wako unabishana na ICT? Kwa hiyo JF wanamuongezea Dr. Slaa? Naona mnakuja na Singo mpya ya "Uongozi wa Bakwata", maana zifuatazo zimechuja:
1. Mahakama ya Kadhi
2. NECTA na Matokeo tata
3. Mgomo wa Sensa
4. Uamsho
5.Hatuutaki Uongozi wa Bakwata new!!!

All the Best Makubazi Jazz band:spy:
 
wote ni wazuri lkn kwa ulimwengu wa ss zito anafaa kimamabano kwa vijana wa leo wanaotaka mapinduzi ya kweli ya kupambana kufa na kupona!!!
 
Zitto ni kijana shupavu, naweza kusema ni chachu ya vijana walioleta changamoto nzuri sana bungeni hata leo, sasa bunge limetambua wajibu wake badala ya kukubali kila kitu cha serikali. Ikumbukwe kuwa enzi za mzee wa urambo Zitto aliwahi kufukuzwa bungeni na kufungiwa kuhudhuria baadhi ya vikao kwa maslahi ya uhuru wa kutoa mawazo. Hakuna shaka Watanzania baada ya kuona umahiri wa Zitto hawakusita kuongeza wabunge wengine wa upinzani na hasa CDM. Idadi kubwa ya wabunge wa CDM bungeni imechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na mwenendo wa Zitto bungeni.Kwa hili la kugombea Urais, simpendekezi Zitto kuwa mgombea wa CDM kwa sababu zifuatazo:1. Ni mpenda fedha mno kiasi kwamba akisikia harufu ya noti hukosa amani, hutamani kusaliti hata watu walio karibu naye ili mradi apate fedha.2. Ni mchanga mno katika siasa kiasi cha kupewa urais wa nchi hii, aendelee kugombea ubunge ili aimarishe upinzani bungeni.3. Ni mpenda madaraka hivyo hatawatumikia Watanzania kwa haki atafanya kazi kwa sifa ili awafurahishe watu fulani fulani. 4. Ni Mtanzania mwenye asili ya Burundi (sisemi kwamba siyo raia wa Tanzania), kwa tabia ya Warundi huwa hawasahau kwao. Kule Burundi kuna uhaba wa ardhi, akiwa rais ataitoa Kigoma kwa Burundi na kuifanya makazi yao hata kama ni kwa siri.Kwa upande wa Daktari Slaa simpendekezi pia kuwa rais kwa sababu zifuatazo:1. Ana uchu wa mapenzi, aliacha kazi ya upadri ili aoe. Tabia hii itamfanya ashindwe kuwatumikia Watanzania badala yake anaweza kuanzisha ligi ya kuoa vidocho akishindana na King Mswati.2. Ni mpenda fedha, hakutaka kuacha ubunge kwa hiari ili agombee urais hadi CDM walipomhakikishia kuwa hata akishindwa urais ataendelea kupokea posho sawa na mshahara wake wa ubunge. Hapa hakuwa na nia ya dhati ya kuwatumikia Watanzania bali maslahi mbele. Nyerere aliacha mshahara wa ualimu na kuchagua kuimarisha TANU bila malipo ya mshahara wala posho.3. Ni mshindani asiyekubali kushindwa. Katika uchaguzi uliopita alisusia hafla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa kura zilichakachuliwa. Maalim Seif alikubali mara zote kushindwa huko Zanzibar hata pale ilipoaminika (haikuthibitika) kuwa kura zilichakachuliwa; mtakumbuka enzi za Komandoo Salmin Amour v Maalim Seif (mara moja), Daktari Karume v Maalim Seif (mara mbili) na Daktari Shein v Maalim Seif (mara moja).4. Ni mdini sana, aliwahi kuwa padri na katibu mkuu wa TEC, akipewa nchi bila shaka ataiongoza kwa sera za Kivatikani au Kisayuni.Kwa maoni yangu wote hawa wawili viz. Zitto na Slaa hawatufai kuwa viongozi katika nafasi ya urais. Naomba uletwe mpambao mwingine.Inawezakana kabisa CDM ikashinda kiti cha urais 2015 lakini rais ajaye si mmoja wa viongozi waliopo ngazi za juu ndani ya CDM. 'Salvation shall come from the hills, the man shall rise and save the people at their hour of need' (Ngugi wa Thiong'o in the River between).
 
Hii ni aibu kwa Zitto na ccm, haikupaswa kushindanishwa na Dr Slaa, si size yake atall
 
Kiongozi yeyote anaye faa ni yule anayeonekana na wananchi tena kwa utendaji wke wa kazi lakini sio hawa wanajiweka kimbele mbele kuomba madaraka, madaraka ni kuwajibika si kujua kuongea sana na kupiga makelele.
 
Zitto ni kijana shupavu, naweza kusema ni chachu ya vijana walioleta changamoto nzuri sana bungeni hata leo, sasa bunge limetambua wajibu wake badala ya kukubali kila kitu cha serikali. Ikumbukwe kuwa enzi za mzee wa urambo Zitto aliwahi kufukuzwa bungeni na kufungiwa kuhudhuria baadhi ya vikao kwa maslahi ya uhuru wa kutoa mawazo. Hakuna shaka Watanzania baada ya kuona umahiri wa Zitto hawakusita kuongeza wabunge wengine wa upinzani na hasa CDM. Idadi kubwa ya wabunge wa CDM bungeni imechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na mwenendo wa Zitto bungeni.Kwa hili la kugombea Urais, simpendekezi Zitto kuwa mgombea wa CDM kwa sababu zifuatazo:1. Ni mpenda fedha mno kiasi kwamba akisikia harufu ya noti hukosa amani, hutamani kusaliti hata watu walio karibu naye ili mradi apate fedha.2. Ni mchanga mno katika siasa kiasi cha kupewa urais wa nchi hii, aendelee kugombea ubunge ili aimarishe upinzani bungeni.3. Ni mpenda madaraka hivyo hatawatumikia Watanzania kwa haki atafanya kazi kwa sifa ili awafurahishe watu fulani fulani. 4. Ni Mtanzania mwenye asili ya Burundi (sisemi kwamba siyo raia wa Tanzania), kwa tabia ya Warundi huwa hawasahau kwao. Kule Burundi kuna uhaba wa ardhi, akiwa rais ataitoa Kigoma kwa Burundi na kuifanya makazi yao hata kama ni kwa siri.Kwa upande wa Daktari Slaa simpendekezi pia kuwa rais kwa sababu zifuatazo:1. Ana uchu wa mapenzi, aliacha kazi ya upadri ili aoe. Tabia hii itamfanya ashindwe kuwatumikia Watanzania badala yake anaweza kuanzisha ligi ya kuoa vidocho akishindana na King Mswati.2. Ni mpenda fedha, hakutaka kuacha ubunge kwa hiari ili agombee urais hadi CDM walipomhakikishia kuwa hata akishindwa urais ataendelea kupokea posho sawa na mshahara wake wa ubunge. Hapa hakuwa na nia ya dhati ya kuwatumikia Watanzania bali maslahi mbele. Nyerere aliacha mshahara wa ualimu na kuchagua kuimarisha TANU bila malipo ya mshahara wala posho.3. Ni mshindani asiyekubali kushindwa. Katika uchaguzi uliopita alisusia hafla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa kura zilichakachuliwa. Maalim Seif alikubali mara zote kushindwa huko Zanzibar hata pale ilipoaminika (haikuthibitika) kuwa kura zilichakachuliwa; mtakumbuka enzi za Komandoo Salmin Amour v Maalim Seif (mara moja), Daktari Karume v Maalim Seif (mara mbili) na Daktari Shein v Maalim Seif (mara moja).4. Ni mdini sana, aliwahi kuwa padri na katibu mkuu wa TEC, akipewa nchi bila shaka ataiongoza kwa sera za Kivatikani au Kisayuni.Kwa maoni yangu wote hawa wawili viz. Zitto na Slaa hawatufai kuwa viongozi katika nafasi ya urais. Naomba uletwe mpambao mwingine.Inawezakana kabisa CDM ikashinda kiti cha urais 2015 lakini rais ajaye si mmoja wa viongozi waliopo ngazi za juu ndani ya CDM. 'Salvation shall come from the hills, the man shall rise and save the people at their hour of need' (Ngugi wa Thiong'o in the River between).

Maneno yote uliyoandika umepoteza muda tu kwani ni ujinga mtupu na kujidhalilisha kwa kuonyesha uwezo wako wa kufikiri
 
too emotional topic, dr Slaa ana rekodi nzuri ya uongozi kuliko zito kabwe,

Dr. W.Slaa
1.kwanza alishinda Urais mwaka 2010, tume ya uchaguzi haijawahi kukunusha haya madai, na bado hawana takwimu sahihi kwa sababu walivurugu utaratibu il mtu wao ashinde
2.ni kiongozi makini aliyekipa chama mvuto na mchango wake mkubwa umepelekea kupatikana wabunge 22,
3.ameendelea kusimamia umoja na uadilifu ndani ya chama
4.ni mzalendo wa kweli. ukimtazama
5.anaaminika sana na watu makini hata ndani ya CCM
6.ana ushawishi mkubwa hata nje ya nchi,
7.si mdini hata kama aliwahi kuwa padri

zitto Kabwe
i. ni kijana machachari mjenga hoja.anahitaji kujifunza zaidi siasa tumpe miaka kama 20,ijayo atakuwa ameiva
Tatizo amaetoka Kigoma tu.Watu wa Kigoma hawaaminiki ni wanafiki.
 
wewe jamaa kilaza kweli kweli, unadhani nchi inaongozwa kwa sababu mtu ni Tajiri, aliyehitimu digrii siku nyiingi, au mwenye majumba ya kifisadi? anahitajika mtu mwenye fikra pevu, huruma ya uzalendo na anayeweza kuileta Tanzania huru, utawala thabiti kwa maendeleo yetu sote. naye ni ZITO ZUBERI K!
 
kwani Ikulu kuna kazi ya kupiga kinanda,jibu ni ndio basi Mimi namchagua Mzee Mzima Slaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom