Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Zitto jamani saizi yake ni ubunge tu kwa sasa. Sijaona kukomaa kwake kunakoweza kupelekea aingie urais. Ila kwa sababu ya demokrasia agombee tu, halafu wanachama tutaamua.
 
ZITTO, ndio shujaa hao wote kina slaa walikuwa CCM , baada ya kushinwa ndo wakahama.sifa gani aliyonayo huyo BABU, ZITTO hana? . msimuonee wivu zitto kwa kipaji chake . lakini sio bure mnaomkashifu zitto wote mmepandikizwa. Sehemu za siri wakubwa nyie. aah aah aah.
 
Zito Kabwe, kweli ana haki ya kugombea urais lakini anatakiwa apime hali halisi iliyopo, sababu bado amezungukwa sana na mazonge ya kutoaminiwa na wana-CHADEMA(wazalendo wa taifa hili). Ajipe muda labda baada ya mwaka 2015!
 
Hawa wote wanafaa sana kuwa wapinzani tu. Kwani umaarufu wao ni kusema ya wenzao. Sasa kutenda kazi ni tofauti sana na kusema ya wenzao. Yeyote anaweza kuwa raisi ila ategemee hakuna jipya atakalolileta zaidi ya kujinufaisha yeye na familia yake na wapambe wake tu.
 
Wote wanafaa ila kwa sasa Dr. Slaa aendelee kupeperusha bendera ya urais
 
zitto atapata kura nyingi akigombea urais kuliko slaa,Slaa ni mzee kwa sasa.

Hatuangalii uzee bali utendaji. CDM ilipofika hapo ni mchango mkubwa sana wa Dr. Slaa hasa baada ya kuwa katibu mkuu
1. Slaa ni mchapa kazi kwelikweli
2. Halali kwa ajili ya watanzania na chama chake
3. Ana mvuto mkubwa sana kwa Watanzania
4. Anaheshimika na watanzania wengi sana na hasa katika chama chake
5. Ni msimamizi mzuri sana kwa watu wa chini yake. hili tunaliona ndani ya chama chake! na hata alipokuwa bungeni
6. Ni mtoaji maamuzi, hababaiki hata kidogo
7. si mwoga, atatusaidia sana kurudisha mali za uma zilizochakachuliwa na kukamata mafisadi wote na waalioua kuwafikisha mahakamani ili sheria iwapatie haki yao
 
wewe utakuwa umetumwa cdm hakunaga udini pale, kama unataka udini nenda cuf. Kama ulishuhudia mkutano wao wa jana na kuona vibarakashia kibao, halafu mbaya zaidi mkutano walifunguwa kwa sara baada ya pastor kuanza kusali wakawa wanamzomea.

Huyo jamaa bila shaka ni CCM, mara udini, ukanda, ukabila, uvurugu vyote vimegonga mwamba. Kama ni udini na anajua kuchungulia majawabu aangalie ndani ya serikali ya CCm halafu atanyamaza mwenyewe, Raisi wa TZ ni dini gani, Makamu wa raisi wa TZ ni dini gani? Raisi wa Zenj ni dini gani? je makamu wake? achungulia katika baraza la mawaziri la TZ na Zenj. aangalie viongozi wa chama cha CCM udini ulivyokolea. aangalie nafasi nyeti za kazi, ni aibu tupu. Tuwapongeze wakristu kwa kulipuuza hilo, wao huwa hawaongei ni kitabu na maendeleo ya nchi kwa kwenda mbele
 
Babu ana busara kuliko baba na pia huwezi kumfananisha baba na mtoto.kama kigezo ni elimu ,kutoka,kukubalika,uzoefu mbona hata haja ya kuomba maoni hamna .jibu unalo
 
ZITTO, ndio shujaa hao wote kina slaa walikuwa CCM , baada ya kushinwa ndo wakahama.sifa gani aliyonayo huyo BABU, ZITTO hana? . msimuonee wivu zitto kwa kipaji chake . lakini sio bure mnaomkashifu zitto wote mmepandikizwa. Sehemu za siri wakubwa nyie. aah aah aah.
Kama wewe ndio mtetezi wa Zitto basi jamaa yako asahau Urais wa nchi hii maana huna tofauti na CCM. Kichwa chako unafugia nywele tu basi
 
Watu wa Moshi na Arusha wanampenda Slaa kwa sababu ya kabila lake
Kwa hiyo zile 26& alipata Moshi na Arusha tu? Wewe unaishi kuzimu nini maana mtu aliyepo hapa Tanzania anajua ukweli. Mnaoleta ukabila na udini wote ni Wana CCM hata kama mnavaa kombati
 
Comment deleted... (name calling)
Paw
Wewe ndio una ufinyu wa mawazo, huoni aibu tangu 2009 post 5 tu?. Hujui hata sheria za JF kwamba hutakiwi kutaja jina lamtu humu. Mods please mtendeeni haki huyu au vipi Mkuu Paw?
 
watanzania tunapotea sasa, mda mwingi siku hizi tunaongelea siasa tunaacha kufanya personal reasearch kwa nini nchi masikini tunapoteza mda kwa ujinga lets be serious guys this is totally idiot. kila mtu sasa hivi kasoma sheria, account, administration fikirieni hili wote mnataka kukaa kwa office mnaacha wazungu/wachina wanafanya proffessional halafu mnakaa ooooooh Zitto vs slaa nani zaidi encourage people to learn technology/ innovation/technical/engineering hili tutoke hapa tulipo hata hiyo europe+america now asia 1800 huko hakuwa na huu ujinga tuliokuwa nao sisi masikini wa akili. BE SERIOUS GUYS.
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
A%20S%20465.gif
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom