Kupwaya kwa vipindi Clouds tv

Kupwaya kwa vipindi Clouds tv

Clouds Tv vipindi vyao
Shilawadu
Habari
Take one
Mahusiano
360
Kambi popote
Sizikitaa
Swali tv ilo hewani masaa 24 baadhi ya vipindi hapo kwa wiki kipo mala moja je mda mwingine huwa kuna nini

Jibu: clouds bado hawajajipanga vizuri kwenye vipindi
 
Tena hii channel yao Mpya ya clouds plus ndio ya hovyo kabisa..signal ziko chini..ina scratch balaa..mbaya zaidi sijaona jipya zaidi ya kurudia bongo movie..sasa sielewi ile channel ya sinema zetu ya kazi gani...labda nieleweshwe hapo
 
Wanazingua aisee kipindi kinafanyiwa marudio zaidi ya Mara tano!
Mfano kambi popote
 
Clouds ni TV ya showbiz...

Sema tu wanajichanganya.

Ni kituo cha infotainment... Formality ya NEWS wawachie wengine..
 
Dhima ya clouds TV ni nini?

Habari?

Burudani?

Documentary?

Tamthiliya?

Mi Naona bado wanasafari Na wanapiga hatua... Kama nanyoona kwa ongezeko la clouds TV plus..

Maudhui yanapokuwa mengi inabidi uanzishe TV nyingine iyabebe hayo maudhui..

Sishangai siku clouds wakizidi ongeza channels zaidi Na kila channel ibebe maudhui yake., Kama ni Habari Na makala iwe channel yake, muziki, tamthiliya, Sinema , michezo..

Hili lipo hata kwa vituo vingine, channel moja inataka ibebe contents zote..

Hili aliishii kwa luninga tu, hata redio pia.. Siku sishangai nione clouds FM 1 , 2, 3, 4 etc...

Kuna vingi vinaachwa kwasababu vinabebwa Na channel moja.
 
Ile ni entertainment television so music is everything vipindi baadae, kama unataka vipindi nenda TBC
 
Kuna tatizo la dominance ya kipindi kimoja kinaitwa 360. Hicho kipindi ndo kitaiua clouds.... Kama wanaweza wafanye regulation haraka sana. Kwa mfano ili uonekane kuwa umehojiwa na ukahojika ni lazima uhojiwe na Hassan, au babie... Na siku hizi wanamuongeza masoud.

Ni mbaya kwa televisio inayotazamwa siku nzima kutegemea kipindi kimoja. Naona sasa hivi hata matukio ya kitaifa yanayofanyika Muda ambao sio wa 360, bado yana rushwa na haohao watangazaji wa 360....

"......kufilisika kunaanza baada ya kupata ziada"
 
Mmetumwa na Bashite? kumbukeni hiyo ndio Tv inayoangaliwa na amiri jeshi mkuu
 
mnataka vipindi vyote vioneshwe na clouds hizo chaneli nyingine zinafanya nini??
 
Kuna tatizo la dominance ya kipindi kimoja kinaitwa 360. Hicho kipindi ndo kitaiua clouds.... Kama wanaweza wafanye regulation haraka sana. Kwa mfano ili uonekane kuwa umehojiwa na ukahojika ni lazima uhojiwe na Hassan, au babie... Na siku hizi wanamuongeza masoud.

Ni mbaya kwa televisio inayotazamwa siku nzima kutegemea kipindi kimoja. Naona sasa hivi hata matukio ya kitaifa yanayofanyika Muda ambao sio wa 360, bado yana rushwa na haohao watangazaji wa 360....

"......kufilisika kunaanza baada ya kupata ziada"
ulitaka watu wa shilawadu ndio wakaripoti matukio ya namna hiyo?
 
Clouds hawana kipindi cha maana zaidi ya taarifa ya habari nayo baada ya kuanza kutangaza kwa mtimbo wa kughani ngonjera basi kipindi kizuri kilicho baki ni tangazo la coca cola la kunywa hapa hapa

Kweli kabisa Mkuu kwa upande wa taarifa ya habari wamekosa kabisa watangazaji mahili mtu anatangaza na mikono anachezesha kama anaelekeza mkandarasi wa kichina
 
Hapana watengeneze vipindi,Kuna Muda mwingi kunakuwa hakuna vipindi inabidi waweke tu miziki
Clouds in general wamejikita zaidi katika burudani ya mziki ndiyo maana clouds tv haiwezi kuwa kama itv maana target ya audience wao ni tofauti kabisa.
So msoforce wafanane
 
Back
Top Bottom