Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,368
Hata sijui swali lako linaegemea wapi, umenisoma na kunielewa?It means jua au mwez ukipatwa mawimbi huongezeka??
Ngoja nikuandikie tena tena niende kitoto kabisa ukinielewa
1: Maji kupwa na kujaa kunasababishwa na mzunguko wa Mwezi kuizunguka Dunia, hapa kunakuwa na Gravitational force ambayo inayafuta maji yaliyopo Duniani kuelekea Mwezi ulipo,
sasa tuanzie hapa
1: Mwezi ukiwa Kaskazini ya Dunia, basi maji yatajaa Kaskazini na Kusini mwa dunia, na Maji yatakupwa Mashashiri na Magharibi ya Dunia,
Kumbuka mwezi unazunguka kutoka Mashariki kwenda Magharibi, hivyo basi
2: Mwezi ukizunguka na Kufika Kaz-Mag, basi maji yatajaa Kaz-Mag na Kus-Mas na kupwa Kaz-Mas na Kus-Mag
Kwa hiyo kila Mwezi utakapokuwepo kuelekea uso wa Dunia utasababisha maji kujaa kwenye uelekeo huo
Nimejaribu kukuelezea kitoto zaidi