Kupotea bila kujijua

hata mama namuuliza hapa anasema kipindi cha masika. na mvua iliwanyeshea masaa ma5 ,walitembea mpaka mto fulani watu Masasi wanaujua unaitwa Myesi
Kama ni ule mto Mhesi km kadhaa ukitoka tunduru basi nami naufahamu japo si mwenyeji wa huko
Mto huo wenyeji wanasema unatabia ya kuua mtu kila mwaka na kweli mmoja kati ya watu tuliokuwa kule tulikuwa tunautumia kuoga mana maji yalikuwa ni shida(ilikuwa kiangazi)mwenzetu mmoja akachotwa kiajabu na tukaja kumpata baada ya siku tatu,ikabidi na utafiti wetu tusitishe kabisa
Mwaka huu wameenda wengine tena
 
Ukijua sana muda mwingine ni matatizo, hivi unahisi alipagawa? Sikuwahi kumsikia kumtokea jambo hilo na lilitokea siku moja na halijamtokea tena. Kwenye hii dunia kuna mengine hutoyajua mpaka yakukute, naishia hapa.
Tatizo liko hapo unaposema "ukijua sana muda mwingine nitatizo".

Siombei iwe hivyo, lakini pengine mzee ana early onset Alzheimer or dementia. Haya ni magonjwa ya akiliyanayohusiana na utu uzima na ukiyawahi kuna dawa za kusaida kuyakabili/ kuyapunguza/ kuyasogeza yasidhuru sana mapema.

Ukisema "ukijua sana muda mwingine ni matatizo" unaweza kuwa sawa kulinganana mana yako, lakini unawezakuwa unalifumbia macho tatizo badala ya kujaribu kulitatua.

10 Early Signs and Symptoms of Alzheimer's
 
Hizo ni perceptions zako tu hana tatizo lolote.
 
Thibitisha habari zako, zaidi ya hapo huwezi kuepuka kuambiwa unaleta ngano tu.
 
Mi nilishawahi kupoteza baiskeli porini sikuiona kwa miaka minne mwaka wa tano nilikuja kuiona palepale haikuguswa wala kusogezwa mpk Leo siamini niliota au lakini ndio ukweli
 
Kwahiyo mkuu ulizurula si mchezo
Sasa hawa wanaopotea kutwa?
Yalikuwa masi
Hata kwa sasa ukimgusa Jiwe tu utapotea hivyo hivyo, so inawezekana hayo utokea
 
Hizo ni perceptions zako tu hana tatizo lolote.
Hana tatizo lolote wakati kapotea kurudi kwake hivyo na so far tunaona hajafanyiwa hata tests za cognitive ability?

Are you in denial?
 
Mzee baba tusilishane matango bana... Musoma kwetu pia
 
Safi sana, wengi tumeshindwa kufikiri nje ya box ila pia tu wavivu wa kusoma. Mpaka vijana wa le bado kila kitu wanakihusisha na mambo ya giza
 
Akili yako haiko sawa
Kumradhi, nia ya akili hii isiyo sawa ilikuwa kumtakia mema mzazi wako na kama kuna namna ya kumuagua mapema kabla pengine matatizo makubwa zaidi hayajamfika, itafutwe.

Lakini naona tunatoka dunia mbili tofauti.

Akili yangu haiko sawa katika dunia yako mkuu.

Kila la heri kwako wewe na familia yako.

Kwa heshima na taadhima.
 
Safi sana, wengi tumeshindwa kufikiri nje ya box ila pia tu wavivu wa kusoma. Mpaka vijana wa le bado kila kitu wanakihusisha na mambo ya giza
Vitu vingine ni Natural mkuu.
sio mambo ya giza wala sayansi.
Duniani kila kitu ni maajabu ila tu yanatofautiana. huoni ajabu kupanda mbegu ukaota mti ,sio mysterio hayo?
kwahiyo hayo mambo yapo ni natural ukifanya hiki kitatokea hiki, ndio maana kuna vitu vinaitwa najisi....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…