Nilipotea siku 3 porini wakati nipo darasa la tano, kisa ka mbwa tu...home wakaweka tanga siku ya 3 na mm nikaingia usiku wake *****, sitosahau, zaidi ya saa 72 nimekwama eneo ambalo naona nimezingukwa na mto mm nipo kati kati na mbwa wangu wa3, mto umetengeneza duara alafu mto una ngema za maana, siku nakuja pata akili ya kutoka pale ni siku ya tatu alfajiri, hapo nishakula sana majani na matunda pori silijui hata moja, mbwa wamekonda, wamekuwa wapole, mm tumbo limeingia ndani, dah hii siwezi sahau kabisa, ule ulikuwa ni ulimwengu mwingine kabisa. Ilikuwa ni kama maono tu, sababu nilishaanza kukata tamaa lakini kuna sauti ndani yangu ilikuwa ikiniambia siwezi kufa ki rahisi namna ile tena ikiniambia nikishindwa kuweza kutoka pale nitapotea jumla, aisee, nilitoka pale siku hiyo ya tatu, alfajiri kama saa 10 hivi ndio napata wazo kwamba nijaribu kubadili nguo zangu na viatu ( nje ndani ) na viatu pia unavigeuza cha kudhoto unavaa kulia. ( Nakumbuka ile siku nilivaa viatu vile vitokanavyo na matairi ya magari, ( nikaanza safari bila ya kuuona tena ule mto, hakuna mto wala nini, mpaka inafika saa 7 ndio nikaanza kuona moshi kwa mbaaali nikaanza ufuata kuufikia ilikuwa saa 9, nikakuta mashamba ya miwa, sasa akili ikaanza kurudi kwamba nipo wapi, hapo nilipokuwa na nilikuwa nikiwasikia kaka zangu huwa wanaenda kuwinda karibu na mashamba ya miwa, basi nikatembea pembezoni nikiwa nayafuata mpaka nikafika kwenye barabara za kwenye lile shamba, nikaifuata mpaka nikakutana na barabara ambayo sasa naifahamu, kutoka nilipotokea mpaka kufika kijiji chetu kulikuwa na kilometer 7, nikaanza safar ya kuelekea home huku nguvu zikizidi niisha, mbwa ile barabara haikuwa ngeni kwao wakaniacha pale wao wakatangulia nyumbani, sasa wale waliokuwa kwenye matanga pale nyumbani walipowaona wale mbwa watatu wamerudi, na nilionfoka nao siku 3 zilizopita ikabidi watumwe watu wafuatilie ile njia ambayo mbwa wametokea, ndipo waliponikuta mbele mbele huko sasa kutembea tena siwezi yaani nalisikia tumbo kama limegusa uti wa mgongo, nimekaa tu, natafuna majani pembeni ya barabara ili nipate japo nguvu ya kudogea, nikachukuliwa pale kwenye baiskeli, kufika home, vilio vikaanza upyaaa, wazee wa kijiji wote wapo home, kabla ya kuingizwaa ndani kuna tamaduni zilifanyika pale...sitosahau
Kila nikikumbuka kilichonitoa nyumbani roho huwa inaniuma sana,
Ka mbwa tu, kalikatiza alafu kamekonda kishenzi sasa mm nilikuwa nawalisha chakula mbwa wa home, walipokaona kale ka mbwa wakanizidi nguvu wakaanza kukafukuzia, ndio ikabidi na mimi niwaungie maana wale mbwa hawakutakiwa kuwa wamefunguliwa muda ule, ilikuwa ni kesi kwangu kumbe ndio nakimbilia majanga.