Kupokea simu asubuhi ukiwa umelala na mpenzi wako.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Ukiwa na mpenzi au mwenza wako kwenye marital bed, ni busara kuweka simu kwenye vibration. Mihangaiko ya mchana kutwa inachosha, na usingizi ni njia pekee Mwenyezi Mungu alituwekea kupunguza uchovu bure bila gharama.

Kuna wale wanaotegemea simu za biashara ya kazi na nyingine huingia hata saa 11 alfajiri. Inawezekana ni kijana wa duka anakufahamisha ana dharura hawezi kufungua duka saa moja asubuhi. Inawezekana ni ndugu amepata ajali au hata taarifa umeshida bahati nasibu ya Taifa.

Unapopokea simu alfajiri, mfikirie mwenza wako, si ajabu hakupata usingizi wa kheri usiku na usingizi umemfika alfajiri. Sasa wewe unaanza, mzigo umeingia! Hakikisha mimi ninakua wakwanza kuangalia viatu na mawigi. Ikibidi kupokea simu nenda nje ya chumba taratibu.

Ni vitu vidogo lakini vinakera, na kama mnaaminiana wala mwenza hatakua na shaka huyo uliyeenda kuongea nae ni nani.

Ijumaa Njema.
 
Siku unakamatwa anakwambia weka Loudspeaker halafu ni simu ya Mcheps 😅 ndio utajua hujui
 
Mimi ninalia na mtu mzima mwenye akili zake timamu anayempigia simu mwanandoa usiku halafu anaanza kupiga story saa nzima.Hivi wewe mwanandoa mwenzangu hujui kuwa huo ndo muda wa kuboost ndoa? Mnakera sana watu wa namna hii.
 
Back
Top Bottom