Mkjj,
Unaona vipi kama miongozo ya uchaguzi ibadilishwe kidogo kuhusiana na hili hili swala... Ya kwamba, pale ambapo vyama vingine vinaposhindwa kusimamisha mgombea mwenza, basi chama ambacho kimepata mgombea pekee katika jimbo husika kiruhusu mgombea aliyekuwa wa pili katika kura za maoni za kupitisha wagombea wa chama hicho aruhusiwe kugombea ubunge kama mpinzani aliyepita kwa kura zaidi (au baada ya kuteuliwa), japokuwa ni ndani ya chama kile kile.
Steve Dii
Safi kabisa ...sasa kila kitu kiko wazi ni juu yao waamue cha kufanya!!!!!!!!!!!
Ahsante Mzee Mwanakijji. Hapa sasa ndipo anatakiwa mtu kama Mtikilla, kufungua kesi mahakamani, hawa watu wasiingie bungeni mpaka wachaguliwe, huku kwetu watu wamechukia sana huyu mbunge wetu ambaye kwa njama tu ametangazwa kupita bila kupingwa na matokeo yake mabango ya Chagua Kikwete yamechanwa chanwa, na hii inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mwanakijiji,
Action point ya hii mada ni nini mkuu?
Say word?
Unataka kuniambia candidates "waliopita bila kupingwa" hawapigiwi kura?
Hata Ally Mwinyi na Nyerere tuliwapigia kura za "NDIYO" au "HAPANA".
Say word?
Unataka kuniambia candidates "waliopita bila kupingwa" hawapigiwi kura?
Hata Ally Mwinyi na Nyerere tuliwapigia kura za "NDIYO" au "HAPANA".
mzee.. si ndo maana wanaitwa "wamepita bila kupingwa"? LOL
Wamepita bila kupingwa huko kwenye party politics, hawajapita bila kupingwa kwa wananchi, ni lazima wapigiwe kura.
Hata kama mgombea ni mmoja tu watu wapate nafasi hata ya kupiga kura ya "NDIYO" au "HAPANA". Ama sivyo tutaanza kuona electioneering mpya ambapo wagombea wananunuliwa, wagombea wengine "wanapita bila kupingwa" na wananchi wanaachwa solemba.
Siamini kwamba wagombea "waliopita bila kupingwa" wataingia bungeni kama wabunge bila kupigiwa kura na wananchi, where do you get this idea Mwanakijiji ? This is a genuine question, not a rhetoric one, I would like to know where this nonsense is steming from.
Au unatoa a precautionary note in the style of "tahadhari kabla ya hatari" ?
well.. wameshapita bila kupingwa wanasubiri kuapishwa tu. Hiyo ndiyo sheria yetu. Madiwani na Wabunge.. sijui kwa rais ikoje kwani kwa rais inaonesha bado rais atapigiwa kura.