Msemaji wa Wizara ya Biashara ya Marekani Matthew Miller amedai kuwa, marufuku hiyo imewekwa bila ya msingi, na itavuruga soko la chip za kampyuta. Lakini, kwa kweli, katika miaka ya hivi karibuni, kutoka Huawei hadi TikTok, Marekani imeweka vikwazo dhidi ya kampuni zaidi ya 800 za China kwa kisingizio cha “usalama wa kitaifa”. Katika mkutano na waandishi wa habari, mwanahabari mmoja alimuuliza Miller, ni kwa nini Marekani inaweza kupiga marufuku kampuni za China kutokana na usalama wa taifa, lakini China haiwezi? Miller alijibu kwa kusitasita, kwamba sababu ni kuwa China imesema inafungua mlango wake kwa kampuni za nje. Jibu hilo liliamsha swali lingine kutoka kwa mwanahabari huyo, ambaye aliuliza, je, si Marekani pia imesema inafungua mlango kwa wafanyabiashara?
Ingawa alichouliza mwanahabari huyo wa Marekani kilikuwa ni sawa, lakini hakufahamu vizuri madhumuni ya China, na kuchukulia kuwa China inataka kulipiza kisasi dhidi ya Marekani. Ukweli ni kwamba, hivi sasa Marekani ina wasiwasi mkubwa, kuwa licha ya Micron, China itaadhibu kampuni nyingine nyingi za Marekani, na hii inatokana na vitendo vibaya ambavyo nchi iefanya dhidi ya kampuni za China kwa kisingizio cha “usalama wa taifa”.
Hata hivyo, tofauti na vitendo viovu vya Marekani, hatua ya China dhidi ya Micron inatokana na uchunguzi wa wiki 7 uliofanywa na Idara Kuu ya Forodha ya China, pamoja na Ofisi ya Usalama wa Mtandao ya China. Uchunguzi huo uligundua kuwa, bidhaa za Micron zina hatari kubwa kwa usalama wa mtandao nchini China, haswa katika miundombinu muhimu ya habari. Kulingana na Sheria ya Usalama wa Mtandao na sheria nyingine husika za China, kampuni zinazoshughulikia miundombinu muhimu nchini China zinapaswa kuacha kununua bidhaa za Micron.
Micron sio kampuni ya kwanza iliyofanyiwa ukaguzi wa usalama nchini China, na ile kauli inayosema hatua ya China inalenga kampuni za Marekani haina msingi wowote. Jambo pekee ambalo tukio hilo linathibitisha ni kwamba, baada ya kukamilika kwa mfumo wa sheria wa China, shughuli zozote za kibiashara ni lazima zifuate sheria, na haziwezi kutishia usalama wa taifa la China.