holy spirit
JF-Expert Member
- Nov 30, 2020
- 698
- 1,039
Habarini members, natumaini mnaendelea vyema na majukumu ya kujenga taifa.
Ningependa kupata msaada wa mawazo kutoka kwenu ni jinsi gani naweza kushughulikia swala hili. Mimi binafsi sio mtu mwenye roho mbaya, mambo ya chuki na wivu naweza kuongea kwa kujiamini kabisa kwamba sina kabisa. Napenda sana kuwa independent, kuna nyakati najichanganya na watu lakini muda mwingi huwa nautumia kukaa peke yangu. Hata nikiwa kwenye kundi la watu naweza kuchangia mada kidogo muda mwingine nanyamaza hadi niulizwe.
Shida kubwa inayonikumba kutokana na kupenda kwangu kukaa mwenyewe kunafanya asilimia kubwa ya watu wanaonizunguka waone siwapendi au siwathamini. Hii hali naona sasa inawaingia hata watu wangu wa karibu ndugu pamoja na wazazi. Napata maneno kama vile "we utakuwa mtu wa aina gani huwezi ata kukaa na mzazi wako mkaongea ukija nyumbani kusalimia ni kujifungia chumbani tu". Wazazi nawathamini pamoja na ndugu pia ila ndo nilivyo yani napenda kukaa mwenyewe nisome vitabu, social media n.k. nikionana na mtu tunajuliana hali tunaongea dakika kumi au kumi tano kila mtu anaendelea na mambo yake. Hata chuoni sikuwa mtu wa kupenda discussion nilikuwa nasoma mwenyewe tu hii ilikuwa inafanya watu waone najikuta genius huku mi wa kawaida tu.
Kubadilika ni ngumu kidogo ila tatizo langu ni kwamba nawezaje kuwaondoa watu hayo mawazo ya kwamba mimi siwathamini au nawachukia sababu nayaona hayo mawazo kupitia maneno yao huku uhalisia kutoka moyoni mwangu hauko hivyo.
Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app