Kupenda kunaniponza

Kupenda kunaniponza

Wimbo Ulio Bora:2:7:

-Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
 
Habari wana jamvi,

Its almost a year sasa nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume kwa mara ya kwanza. Hali iliyopo sasa nahisi kufa kwa mawazo, ninashinda nalia peke yangu, sometimes siwezi kula naona niko peke yangu duniani.

Tumekuwa na migogoro ya hapa na pale chanzo kila mmoja akimwona mwenzie msaliti, Binafsi kuna vitu niliviona, sikupenda kabsa though aliaribu kunielekeza but sikutaka kuelewa because niliona havimake sense, at the same time alikuwa anaongea maneno fulan kama vile namsaliti ivi nilichukulia kama utani coz sio kweli.

Finally tuliamua kila mtu ashike 90 zake, binafsi napata shida sana nateseka sana, uwepo wake nahitaji lakini pia sipendi kusalitiwa, naogopa kumwonyesha kiasi gani namuhitaji.
nimejaribu kujkeep busy kufanya vitu tofauti lakini hali iko palepale.

Naombeni msaada wa ushauri nifanye nini niwe katika hali ya kawaida.
hivi kweli wewe na akili yako unawezaje kulipenda limtu umekutanalo ukubwani bhana si bora umpende mama yako aliyekubeba tumboni miezi tisa.
 
Kama imefika hatua unaona hamuwezi kuendelea kuvumiliana Ni bora ukajitahidi kwa namna yoyote kua nae mbali. Naamini kabisa ukidhamiria kumsahau unaweza mana hilo liko ndani ya uwezo wako. Vinginevo ukijiendekeza na kusema huwezi msahau ni kuendelea kujipalilia matatizo.
 
binti njoo kwangu. mimi ni kijana mwenzako na yaliyokukuta wewe na mimi muhanga. Nakuomba saaana njoo pm tuanze mazungumzo. Mimi ni mcheshi sana, mawazo yako yooote yatafika mwisho.
 
Fanya hivi Tutsi gl;

- tembelea sana jukwaa la siasa, intelligence, ujasiriamali na mengine yafananayo na hayo. MAANA YANGU: jiepushe na mazungumzo ya mahusiano na mapenzi kwa sasa.

- ANDIKA (PUT IT ON PAPER): Wanasema wataalamu, ukiweza kuandika hisia zako kwenye karatasi utaweza kuzisahau haraka. Kama sio mwandishi nihaditihie tu mkasa wako tuandike wote itakuwa bonge la hadithi.

- JIFUNZE KITU KIPYA: kuna filamu moja niliangalia, mwanaume alikuwa na shida katika mahusiano yake akachukua jukumu la kujifunza lugha mpya. Mimi hujifunza kozi mpya! Yaani lengo ni kuipa akili yako kitu kipya cha kufurahia kufanya ( @nyaningabu utanisamehe niongee kiingereza hapa)..'something that makes you look forward to..'. Kwa kuanzia pitia hizi sites: www.coursera.org na www.en.duolingo.com - ni bure na utajifunza mambo mengi ya 'fields' tofauti tofauti ikiwemo lugha yeyote mpya bure.

Nadhani tuanzie hapo...!
Duh..

Ts been a year sasa...

Tutsi gl tupe mrejesho tafadhali.
 
Habari wana jamvi,

Its almost a year sasa nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume kwa mara ya kwanza. Hali iliyopo sasa nahisi kufa kwa mawazo, ninashinda nalia peke yangu, sometimes siwezi kula naona niko peke yangu duniani.

Tumekuwa na migogoro ya hapa na pale chanzo kila mmoja akimwona mwenzie msaliti, Binafsi kuna vitu niliviona, sikupenda kabsa though aliaribu kunielekeza but sikutaka kuelewa because niliona havimake sense, at the same time alikuwa anaongea maneno fulan kama vile namsaliti ivi nilichukulia kama utani coz sio kweli.

Finally tuliamua kila mtu ashike 90 zake, binafsi napata shida sana nateseka sana, uwepo wake nahitaji lakini pia sipendi kusalitiwa, naogopa kumwonyesha kiasi gani namuhitaji.
nimejaribu kujkeep busy kufanya vitu tofauti lakini hali iko palepale.

Naombeni msaada wa ushauri nifanye nini niwe katika hali ya kawaida.

mi nimegundua we ndo unamatatizo sana ..et unateseka sana .we huyo umezaliwa naye kwani si ulimkuta tuu kwenye huu mchafuko wa dunia .Yan umeshindwa kabisa kufanya maamuzi hapo?
 
Pole mpendwa kwa sasa jaribu kufuta kumbukumbu zake zote kama pics na msgs zote. pia jaribu kukwepa uwepo wake karibu nawe.

Wanasema kumsahau mtu unaempenda ni kama kumkumbuka mtu ambaye humjui.

But God is always good, wapendwa wetu wanatutoka duniani na bado Mungu anatupa uwezo wa kusahau yale maumivu.

Jipe moyo mdogo angu na ujue furaha ya moyo wako unayo wewe mwenyewe.
Good advice jje's !

Majibu na ushauri wa hivi ndiyo unaozidi kuifanya Jamii Forums kuwa "Home of Great Thinkers".Hongera kwa kwa hilo ila, please nikushauri jambo! Kwenye maneno "Mdogo angu" katika aya/paragraph ya mwisho usipende sana kuyatumia unless unamfahamu mhusika kiumri.Kumradhi kwa hili.

Barikiwa sana.
 
Mapenzi ni chombo cha moto, yanahitaji lesseni kama vile za udereva, pikipiki, ndege n.k

Wazee na mafundisho ya imani yako sahihi kabisa, tungepunguza matatizo mengi sana kama tungesubiri hadi ndoa na kuwa waaminifu kwa wenza wetu baada ya ndoa.

Utakaa sawa tu baada ya muda, binadamu tumejaliwa kusahau mambo baada ya kipindi kupita.
Good Thinking Samaritan !

Baadhi yetu humu Jamii Forums tumejaaliwa majibu ya hovyo sana ila majibu yako huwa yana busara, Hekima na na tafakuri za kina kitu ambacho ni bidhaa adhimu sana katika jamii zetu.

Hongera sana Mkuu, pia Mungu azidi kukubariki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom