Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,999
Moyo ukija kupenda, wenda ukidundadunda,
Mtu aanza kukonda, anapomkosa nyonda,
Alalama kama konda, mwenzenu kumbe kapenda,
Mtu akiisha kupenda, huogopa kuvurunda
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Ukishampenda mtu, moyo usipate kutu
Roho yako iwe kwatu, usilie mimi mbwitu
Usilete katukatu, kwa kusikia ya watu
Mwisho wajikuta fyatu, na penzi likawa butu,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nilimpenda fulani, yule binti wa jirani,
Kaniingia moyoni, penzi hadi mifupani,
Leo kanuna jamani, amepata kisirani
Kosa langu miye nini, najiuliza watani,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
Kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
Nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
Hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nikimgusa aruka, kumbusu anangaka,
Nyonda mbona washtuka, wanitatiza hakika,
Lipi limevurugika, nambie wangu wa shoka,
Ni vipi umekwazika, nitonye nikatonyeka,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Siku zikapitiliza, maswali najiuliza,
Kuliza ameniliza, na majonzi kanijaza,
Najikunyata nawaza, hadi nimepitiliza,
Ni dogo amelikuza, au nikubwa sijaliwaza
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Nabaki nasubiria, nyonda kunihurumia,
Na aje kuniambia, ni wapi nimechapia,
Mwenzako ninaumia, ninavyokufikiria
Fanya hima kunijia, kosa sitalirudia,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nilichokuandikia, ni kweli nakuambia,
Tafadhali fikiria, jibu nalisubiria
Mikono nimeachia, niweze kukumbatia
Ni mbali tumeanzia, si tayari kuachia
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nafunga ninafungana, ya leo siyo ya jana,
Na wewe nafungamana, ee nyonda wangu mwanana,
Zikongine zafanana, penzi tulilopeana,
Fanya hima kuonana, nina hamu kukuona,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)