Kupenda kumbe ni kazi! .. kunakuja na machozi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupenda kumbe ni kazi! .. kunakuja na machozi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 20, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Moyo ukija kupenda, wenda ukidundadunda,
  Mtu aanza kukonda, anapomkosa nyonda,
  Alalama kama konda, mwenzenu kumbe kapenda,
  Mtu akiisha kupenda, huogopa kuvurunda
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!

  Ukishampenda mtu, moyo usipate kutu
  Roho yako iwe kwatu, usilie mimi ‘mbwitu’
  Usilete katukatu, kwa kusikia ya watu
  Mwisho wajikuta fyatu, na penzi likawa butu,
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!

  Nilimpenda fulani, yule binti wa jirani,
  Kaniingia moyoni, penzi hadi mifupani,
  Leo kanuna jamani, amepata kisirani
  Kosa langu miye nini, najiuliza watani,
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi

  Kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
  Kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
  Nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
  Hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!

  Nikimgusa aruka, kumbusu anan’gaka,
  Nyonda mbona washtuka, wanitatiza hakika,
  Lipi limevurugika, nambie wangu wa shoka,
  Ni vipi umekwazika, nitonye nikatonyeka,
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!

  Siku zikapitiliza, maswali najiuliza,
  Kuliza ameniliza, na majonzi kanijaza,
  Najikunyata nawaza, hadi nimepitiliza,
  Ni dogo amelikuza, au nikubwa sijaliwaza
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi

  Nabaki nasubiria, nyonda kunihurumia,
  Na aje kuniambia, ni wapi nimechapia,
  Mwenzako ninaumia, ninavyokufikiria
  Fanya hima kunijia, kosa sitalirudia,
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.

  Nilichokuandikia, ni kweli nakuambia,
  Tafadhali fikiria, jibu nalisubiria
  Mikono nimeachia, niweze kukumbatia
  Ni mbali tumeanzia, si tayari kuachia
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.

  Nafunga ninafungana, ya leo siyo ya jana,
  Na wewe nafungamana, ee nyonda wangu mwanana,
  Zikongine zafanana, penzi tulilopeana,
  Fanya hima kuonana, nina hamu kukuona,
  Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Pole sana kwa kutoa chozi, pengine kapenda mwingine au umemkosea muulize polepole, kama vipi mpotezee.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280

  sasa kama ni hivi si bora angesema? au ndio haya ya "huku ataka na kule ataka".. ?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Labda amestukia wewe ni mlaji ukishiba waeza tafuta mti mwengineo wenye matunda kesho yake.

  Ushauri: Jaribu
  kutangaza nia.
   
 5. T

  Tall JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.haya ni mapenzi original
  2.mapenzi kama haya ni adimu kuyapata.
  3.usanii kwenye mapenzi hivi sasa ndio unatawala kwa kiasi kikubwa.
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hii inaelekea kufanana na kisa fulani hivi, kweli kupenda ni kazi especially unapokuja kutoa machozi kwa mtu unayempenda halafu yeye haoni hilo ndio maana watu wengi wakiumizwa na mtu fulani kwenye mapenzi na yeye anaamua kuumiza wengi pia ambayo kwangu mimi huwa siaafiki kabisa lakini hayo ndio mapenzi na kupenda ni kazi tegemea lolote kukutokea.
   
 7. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mapenzi ya kwenye Tamthiliya........ shades etc.
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Pole mzeee MM wajua kupenda ni kazi ..wewe waweza penda binti fulani kumbe yeye kapenda kwingine .:confused2:
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MMKJ kweli kupenda kazi na kwaitaji moyo
   
 10. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usipokuwa makini, unaweza kuwa chizi
  Ukipenda kwa undani, utatokwa na machozi
  Unasumbukia nini, si uwaambie wazazi
  Mapenzi yanayo nguvu, tena yashinda mauti,
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,665
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Hapa tupo ukurasa mmoja mkuu inawezekana kabisa hii....:confused2:
   
 12. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kweli kupenda ni kazi,huwa najiuliza kwanini Mungu aliweka upendo wa mapenzi i wish usingekuwepo!! MM hapo penye red ni pagumu sana maana watu wengi ni selfish,full usanii utadhani wote wamepita bagamoyo!
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wenzio walipokubwa na maswahiba kama yako walisema hivi

  si kitu kunipuuza, kwako tamaa sikati
  fikira sitogeuza, moyo wangu madhubuti
  ni lani utavyoweza, naapa sikubanduki


  anaependa kikweli, hachoki kuvumilia
  habadilishi kauli, japo ukimchukua  wajua ninakupenda, ndo mana waniringia
  unanifanyia inda, mapenzi kuyasusia
  baada ya hiki kidonda, na moto unanitia

  anaependa kikweli, hachoki kuvumilia
  habadilishi kauli, japo ukimchukua


  nikimbie japo mwaka, nipo ninakungojea
  ukirudi nakutaka, wala sitoona haya
  ........................,........................


  anaependa kikweli, hachoki kuvumilia
  habadilishi kauli, japo ukimchukua


  Source: nyimbo moja ya zamani sana
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,665
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Uwe na busara kama Wiselady
  Au na upendo kama FirstLady,
  Na ma "passion kama queenKammy
  Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa!

  Na Ukipendwa kama Nyani Ngabu
  Watu hawakosi sababu!
  Ili mradi mapenzi tabu, na
  Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa

  Mfikiriea Zion daughter,
  Kila kitu amepata,
  Naye JS amedata, kisa
  Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa!

  Uwe mkarimu kama bacha
  Au Fidel80 wa kukacha,
  Na The Finest wa kuacha..bado
  Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa

  Ukiwa mtulivu kama Asprin
  Au Mlokole kama Gaijin
  Bado utaikuta Acid! kisa?
  Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa!

  Nilidhani katulia Teamo,
  Kumbe madhila yangalimo!
  Nikamuliza Masanilo! kanambia:
  Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa

  Ni kwako Cheusimangala,
  Je waweza kugangamala?
  Manake hayana muamala,
  Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa

  Alipata kusema Nyamayao,
  'kitusimulia ya kwao
  Kumbe ndio hayo hayo,
  Mapenzi yanatesa 'kiyapatia unatesa....
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kaizer sikujua kama na wewe ni mmalenga ...............:smile-big:
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,665
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  am not, thanks anyways..malenga kuna Mwanakijiji and co bana sio mchezo...
   
 17. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dah nimeipenda hii.....
  Very creative.....
   
 18. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mwanafasihi mzuri sana wewe Kaizer, vipaji mnavyo mnavikalia, au mnataka watu tuwahamasishe kwa campaign za shuka kwa shuka ili mvitoe vipaji vyenu hadharani?
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kweli we kiboko. Ushamtungia mistari yule dada anayempenda NN?
   
 20. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kaizer nitakupeleka kurecord hiyo single, baada ya hapo utafanya featuring na Mwanakijiji so itakuwa full mautamu.Love it, hasa hapo kwa Fidel kukacha nikilinganisha na avatar yake mh,,:becky::eyebrows:
   
Loading...