Naxria abdalla
Senior Member
- Feb 28, 2025
- 178
- 311
Habari zenu wana jamvi leo nimekuja kwa unyenyekevu mkubwa ndugu yenu naumwa hlf sijui nini kinanisumbua najua itawashangaza ila na huu ukubwa nilonao sijui naumwa nini ni vile najiskia vibaya mwili unakosa nguvu mda mwengine viungo vinauma tu mda mwengine kama nataka kutapika inafika mwezi wa 4 nikienda hosptal za serikali wananipima tu malaria wananipa dawa hakuna afadhali ninayopata,sasa nimeamua kwenda hosptal za binafsi ila kabla sijaenda nataka ushauri vipimo gani niombe kufanya au doctor nikimuelezea ataelewa nini anipime?mana nateseka mno