Habari zenu wakuu,
Mwaka jana tulikuwa tumesafiri kwenda nyanda za juu kusini wakati wa kurudi tulisimama wilaya fulani mjini kwa ajili ya kuongeza maji bahati mbaya tulisahau kufunga mfuniko wa rejeta, baada ya kutembea kilometa kadhaa gari ikawa inaishiwa nguvu kwenda kuangalia maji yote yamemwagika japo tulijaribu kuongeza mengine haikusaidia ikabidi turudi kwenye ule mji tulioupita kwa kuvuta gari tuliwaomba hawa jamaa wa it.
Tulivyorudi garage ikaonekana tatizo sio la kuisha muda ule kwani silinda head imepinda na wahindi wanaonyoosha hawafanyikazi J2 basi tukaazimia kulala kesho yake J3 tushughulikie na kuanza safari, wakati naenda duka fulani kununua vocha kuwataarifu ndugu na jamaa mkasa uliotukuta nikakutana na demu fulani tuliosoma naye primary yeye alivyofeli la saba alikuja mjini kumsaidia dada yake kwenye mgahawa, basi baada ya mawili matatu nikampa namba ya simu kama baadae ataweza kuja tupige pige stori.
Kufupisha habari usiku kama wa SAA 4 hivi nikaona meseji upo chumba gani sababu nilijua ni yeye tu nikamwelekeza na kumfungilia mlango, baada ya stori za maisha za hapa na pale ukafika mda wa kula tunda kusema kweli alinifariji machungu ya safari na mkasa wa uzembe ule ambao kwa kiasi ulitugharimu pesa sana nakumbuka nilipiga bao3 tu kwa usiku ule ila zilikua za ufundi haswa.
KISA CHENYEWE.
Baada ya kupotezana kwa muda bila mawasiliano na huyu mwanamke jana nimeona meseji yake ananisalimia anasema aliibiwa simu hata hivyo alikuwa anaumwa kwa mwonekano wa picha yake huwezi bisha kuwa anaumwa sana nikajaribu kumdadisi nini kinamsibu akanimbia wazi ameathirika na ushahidi akanionyesha na akaomba samahani kama amaeniambukiza kwani ana uhakika aliyemwambukiza ni mzazi mwenziye anayefanya biashara ya mbao na alikuwa naye kabla hata mimi sijatembea naye, kweli nimemtoa hofu kuwa mimi niko mzima na nimemwahidi kumsaidia kama itabidi kwani nimepima mara nyingi tu na niko -ve. Sasa nimefikiria kama bao 3 hazikutosha kunipa VVU huu ugonjwa ni selective sana au sio rahisi kuupata wajuvi nisaidieni.