Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!

Mfano kontena zimekamatwa, scanner zimeonyesha kilichomo, ndani, mhusika mwenye kontena ametafutwa, amepatikana na amekamatwa yuko kwenye selo ya polisi, contena zimefunguliwa mbele yake kujiridhisha kilichomo, kishamhusika anasweka selo, contena zinarudishiwa kwa kufungwa tena, zinawekwa seals mpya, kisha rais anaarifiwa atafute muda aje kufanya ziara ya kushtukiza, muda ukipatikana, media zinaarifiwa, kuwa rais atafanya ziara ya kushutukiza bandarini, hadi muda wa ziara hiyo, kisha rais anafanya ziara, anaonyeshwa contena hizozikiwa zimefungwa, kisha zinafunguliwa mbele ya rais huku media ikilirekodi tukio zima huku watu wakijifanya kushangaa!.

Mkuu wakati unasoma hasa shule ya msingi hukupaka mawe chokaaa kwa kuwa kiongozi anakuja? kinachokushangaza nini kipi hasa hapa? hii ndio siasa sasa na ni mbinu kati ya mbinu za kuuza sera za chama ili uchaguzi ujao ushinde.

Tatizo lingekua baya kama hicho ambacho wamefanya ni kiini macho tu!

Mkuu Mayala ni wakati sasa wa kubadilisha mtizamo. kwakua ripoti mbalimbali zinazofanywa na wachumi duniani wanauweka uchumi wetu katika namba za juu mfano Hotuba ya Waziri Mkuu inasema uchumi wetu utakua kwa asilimia 7.4 mwaka huu ambao ni kiwango kikubwa kutokea katika Afrika ambapo tupo kati ya nafasi ya 2 na 5.

Utawala bora Tanzania inafanya vizuri pia. Sasa Mkuu Mayala unataka aje ambaye hana maigizo lakini uchumi wetu ukue kwa asilimia 6.2 au huyu unayemtuhumu kuwa mwana maigizo na uchumi ukue kwa asilia 7.4?

Hata Mungu hapendi watu vuguvugu mayala ni ima uwe Moto au Baridi.
 
Wanabodi,
Sisi Wana mitandao tumeshauriwa kuitumia mitandao kulisaidia taifa letu kuendelea, hivyo huu ni ushauri wangu.

Ili Tanzania tuendelee tunahitaji kujenga Taasisi Imara zenye an effective systems, yaani kujenga mifumo imara ambayo inakuwa automated, ikitokea kuna jambo lolote haliko sawa, the system ita detect na hivyo kuwa ejected out of system, hakutakuwa na haja ya tumbua tumbua, mtu akienda kinyume cha mfumo, ni mfumo ndio utamuondoa, na sio kumsubiria rais kumtumbua!.

Tanzania hatuhitaji sanaa za maonyesho ya drama na ze comedy za one man show za maigizo ya utawala bora na maonyesho ya uchapakazi kwa ziara za kushtukiza, ili jioni jioni kutokea kwenye TV zetu ili tuu watu waone jinsi viongozi wetu, wanavyochapa kazi, just to make believe something is being done na rais wetu!.

Ziara za Kushtukiza Vs Maigizo ya Ziara za Kushtukiza.
Kuna ziara za kweli za kushtukiza na kuna maigizo ya ziara za kushtukiza. Ziara za kweli za kushtukiza hufanyika kwa kushutikiza kweli, no one knows, hata media ni ile tuu ya rais, lakini maigizo za ziara ni pale wahusika wanaambiwa, media inaambiwa na kualikwa ili iwepo mahali husika panoposhtukizwa ili warekodi tukio, na jioni watu waje waone kwenye TVna kesho yake kwenye magazeti !.

Mfano kontena zimekamatwa, scanner zimeonyesha kilichomo, ndani, mhusika mwenye kontena ametafutwa, amepatikana na amekamatwa yuko kwenye selo ya polisi, contena zimefunguliwa mbele yake kujiridhisha kilichomo, kishamhusika anasweka selo, contena zinarudishiwa kwa kufungwa tena, zinawekwa seals mpya, kisha rais anaarifiwa atafute muda aje kufanya ziara ya kushtukiza, muda ukipatikana, media zinaarifiwa, kuwa rais atafanya ziara ya kushutukiza bandarini, hadi muda wa ziara hiyo, kisha rais anafanya ziara, anaonyeshwa contena hizozikiwa zimefungwa, kisha zinafunguliwa mbele ya rais huku media ikilirekodi tukio zima huku watu wakijifanya kushangaa!.

Igizo la Ziara ya Kushtukiza Jana Pale Bandarini.
Ni wajinga tuu na wale wasiofahamu process za bandari ndio wataamini kuwa jana rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza Bandarini Dar, na katika ziara hivyo amebaini contena 26 za mchanga wa dhahabu na contena 2 zilizoficha magari ya kifahari ili tuu kuonyesha rais wetu ni mchapa kazi, ameokoa tusiibiwe and he is doing something!.

Kilichotokea.
Kusafirisha containers is a process, by the time rais anapiga marufuku kusafirisha mchanga wa dhahabu, tayari consignment ya huo mchanga unaodaiwa kukamatwa, tayari iliishakuwa processed on transit na kuna mizigo iliishafika bandarini siku nyingi kabla ya marufuku ya rais, na kwenye ICDs, hapo bandarini, hivyo kupitia tangazo la marufuku ya rais, likapelekea hizo consignment zote zisimamishwe na kuzuiliwa bandarini. Sasa kujidai kukamata kitu kilichohifadhiwa na kuzuiliwa kihalali kabisa ni usanii!.

Containers za Mitumba Kumbe Magari!.
Zile contena za magari zilizoandikwa mitumba, zote ziliwasili nchini toka mwaka jana, na zilipitishwa kwenye scanners na kuona kilichomo ndani ni tofauti na kilicho kuwa declared kwenye the bills of landing. Mmiliki wa mzigo huo ni Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju ambaye ameisha kamatwa siku nyingi, tangu Mwezi February, containers zake zikafunguliwa mbele yake, na yuko kwenye mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huo wa February kwa kosa la kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyoingizwa nchini kinyemela kama nguo za mtumba, na toka alipokamatwa hiyo tarehe 4 mpaka leo, bado hajafikishwa mahakani ili tuu kusubiria mpaka rais apate nafasi ya kuja kufanya ziara ya kushtukiza huku mhusika akiozoea jela!. Standard time ya mtu kufikishwa mahakamani ni 24 hrs! . Mtu kukamatwa tangu tarehe 4 February hadi leo bila kufikishwa mahakamani ili kutengeneza igizo la kukamatwa hizo containers!. Kisha rais anakuja, wanaweka seal nyingine na kufungua upya!.

Ni Mchanga Au Makinikia?
Scanners zimeishaonyesha ya mchanga, ambao jina lake halisi ni makinikia, containers hizo zilipokelewa bandarini siku nyingi nyuma ya marufuku ya rais kusafirisha mchanga nje, na process iliisha anza kabla ya katazo la rais, hivyo rais kaelezwa ni mzigo mpya, ni kumdanganya!. Yaani kila kitu kinajulikana, kisha rais wetu anaitwa kuja kushtukiza akiandamana na media, na kesho yake ndio headlines, hili ni igizo la ziara ya kushtukiza!, but very unfortunately kwa this time around, igizo la jana limebuma ku attract the much intended attention ya front page kwa sababu kulitokea tukio kubwa zaidi, more news worth kuliko igizo hili!.

Drama na Igizo za Ziara ya Kushtukiza.
Baada ya hayo kubainika, daily report ilionyesha lakini ikaamuliwa kusichukuliwe hatua zozote bali mkuu wa nchi aarifiwe kwanza, kisha ipangwe ziara ya kushtukiza halafu ndipo hayo yaonekane yamebainishwa na ziara hiyo ya kushtukiza ili ionekana kama ni ziara ya kushukiza ya rais ndio imebaini hayo!. Everything was a premeditated moves, but it was well staged kuonekana ni issue kubwa, lakini ndio hivyo tena, sometimes hata sterling kwenye movie huwa ana bugi step na hulazimika kufanya take two or take three!. Jana kwenye media Nape ndio alikuwa sterling!.

Shows za Ze Comedy.
Kumuita Mkuu wa nchi kufanya ziara za kushtukiza katika tukio lililopangwa na kisha kufungua zile seals za yale makontena mbele ya rais huku akishuhudia na ku act kushangaa, kuwa ndio wamebaini hayo magari ya kifahari, ili tuu kuuaminisha umma kuwa ni ziara hiyo imebainisha hayo, ni kupoteza muda wa thamani wa rais wetu. Hivi sio vitu vya kulisaidia taifa letu. Tusifanye vitu tuu ili watu waone!. Viongozi wetu wasitumie media kufanyia maonyesho ya maigizo ya utendaji kazi, au utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku!.

What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na mission wala vision ya ni nini vipaumbele vyetu, Tanzania kama nchi inayotaka maenddeleo ya kweli, tunatakiwa tujue ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndipo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio. Nchi inakabiliwa na sitofahamu nyingi, kuna kiongozi amefoji vyeti, kuna kiongozi amefanya tukio la uvamizi wa media, kuna waziri anatimiza wajibu wake kwa waledi, anatumbuliwa, na kutishiwa bastola, halafu mkuu wetu wa nchi anakwenda kufanya igizo ziara ya kushtukiza bandarini! .

Ushauri on A Way Forward and What to do.
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na wakala, lazima ziwe na mission na vision statements, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas maonesho na kuita media na kutoa maagizo kwa kusema tutafanya hiki au kile, lakini hatuoni, utekelezaji.

Mfano tunapo hubiri kuhusu Tanzania ya viwanda, where is the blue print ya Tanzania ya viwanda?, zenye smart objectives zenye malengo ya short term, medium term na long term strategies?. Ili tuwe na Tanzania ya viwanda tunahitaji land, where is the land set out kwa Tanzania ya Viwanda?. Tunahitaji labor, jee tumeishajua tutajenga viwanda gani vya vyakuzalisha nini ili hiyo mainpower na labor force kuvihudumia hivyo viwanda itayarishwe?. Tunahitaji capital ya kuanzisha hivyo viwanda, kuna strategies gani kuwawezesha Watanzania kuimiliki Tanzania ya Wiwanda, au tunataka kujenga Tanzania ya viwanda lakini viwanda ni vya wageni, vya Mchina, Mhindi na Mzungu?, na Mtanzania kuja kuwa ni kibarua tuu kwenye hiyo,Tanzania ya Viwanda kama ilivyo kwenye Uchumi wa Gesi?. Tanzania ya viwanda itahitaji malighafi ya viwanda, uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo the biggest industries za Tanzania ya Viwanda zinapaswa kuwa ni agro processing industries, jee tuna mikakati gani ya kuinua sekta ya kilimo, ili izalishe malighafi ya viwanda?, au tunajenga Tanzania ya viwanda kama viwanda vya Bhakressa, vinatengeneza juces na unga wa ngano, lakini malighafi zote zinatoka nje!, hadi pulp ya mango juice tuna import, huku maembe ya Lushoto yakiozea mitini!. Tangu tumeanza kuhubiri wimbo wa Tanzania ya Viwanda, what is the plan?, tuko wapi, tumefanikisha nini? , tumekwama wapi and what is a way forward? .

Badala ya kuwahimiza ma bullies,impersonators, impostors na forgerist kuchapa kazi, tupewe matokeo ya hizo kazi zinazochwapwa, watu wanataka matokeo, na sio tuu kupokea maagizo na vitendo vya kuona sifa kutokelezea tuu kwenye TV huku wakitoa maagizo, na kuandikwa magazetini, sasa tujikite kwenye utendaji unaozingatia matokeo, na sifa zisiwe katika kutoa maagizo, bali ziwe katika matokeo ya utekelezaji wa maagizo hayo.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Pole sana Paskali,
kama unaweza pekua post zangu,hili tuliandika mwanzoni kabisa wakati nyie ndio mmepagawa.Tulifikia hata kuuliza ikiwa Mkuu "ataghairi" kuendelea na ukuu haya yanayofanyika yatakuwa endelevu?
 
Paschal hapa ulitulia sana.Ulikuwa unaitumia kalamu yako vyema. Lakini sikuizi sijawah huko bungeni ulipokwenda kuojiwa walikubinya mapumbu.
 
Wanabodi,
Sisi Wana mitandao tumeshauriwa kuitumia mitandao kulisaidia taifa letu kuendelea, hivyo huu ni ushauri wangu.

Ili Tanzania tuendelee kwa kupata maendeleo ya kweli, na sio maendeleo kiini macho, tunahitaji kujenga taasisi Imara ( strong institutions), zenye mifumo imara, ( an effective systems) ambayo inakuwa automated, ikitokea kuna jambo lolote haliko sawa, the system itself, it will detect na hivyo kuwa ejected out of system, hakutakuwa na haja ya tumbua tumbua, mtu akienda kinyume cha mfumo, ni mfumo ndio utamuondoa, na sio kumsubiria rais kumtumbua!.

Tanzania hatuhitaji sanaa za maonyesho ya drama na ze comedy za one man show za maigizo ya utawala bora na maonyesho ya uchapakazi kwa ziara za kushtukiza, ili jioni kutokelezea kwenye TV na runinga zetu ili tuu watu waone jinsi viongozi wetu, wanavyochapa kazi, just to make believe something is being done na rais wetu!.

Ziara za Kushtukiza Vs Maigizo ya Ziara za Kushtukiza.
Kuna ziara za kweli za kushtukiza na kuna maigizo ya ziara za kushtukiza. Ziara za kweli za kushtukiza hufanyika kwa kushutikiza kweli, no one knows, hata media ni ile tuu ya rais, lakini maigizo za ziara za kustukiza ni pale wahusika wote wakuu wanaambiwa, media inaambiwa na kualikwa ili iwepo mahali husika panoposhtukizwa ili warekodi tukio, na jioni watu waje waone kwenye TV na kesho yake kwenye magazeti !.

Mfano kontena zimekamatwa, scanner zimeonyesha kilichomo, ndani, mhusika mwenye kontena ametafutwa, amepatikana na amekamatwa yuko kwenye selo ya polisi, contena zimefunguliwa mbele yake kujiridhisha kilichomo, kisha mhusika anasweka selo, contena zinarudishiwa kwa kufungwa tena, zinawekwa seals mpya, kisha rais anaarifiwa atafute muda aje kufanya ziara ya kushtukiza, muda ukipatikana, media zinaarifiwa, kuwa rais atafanya ziara ya kushutukiza bandarini, hadi muda wa ziara hiyo, kisha rais anafanya ziara, anaonyeshwa contena hizo zikiwa zimefungwa na seal as if hazijafunguliwa!, kisha zinafunguliwa mbele ya rais huku media ikilirekodi tukio zima huku watu wakijifanya kushangaa!.

Igizo la Ziara ya Kushtukiza Jana Pale Bandarini.
Ni wajinga tuu na wale wasiofahamu process za bandari ndio wataamini kuwa jana rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza Bandarini Dar, na katika ziara hivyo amebaini contena 26 za mchanga wa dhahabu na contena 2 zilizoficha magari ya kifahari ili tuu kuonyesha rais wetu ni mchapa kazi, ameokoa tusiibiwe and he is doing something!.

Kilichotokea.
Kusafirisha containers is a process, by the time rais anapiga marufuku kusafirishwa mchanga wa dhahabu, tayari consignment ya huo mchanga unaodaiwa kukamatwa, tayari iliishakuwa processed on transit na kuna mizigo iliishafika bandarini siku nyingi kabla ya marufuku ya rais, na kwenye ICDs, hapo bandarini, hivyo kupitia tangazo la marufuku ya rais, likapelekea hizo consignment zote zisimamishwe na kuzuiliwa bandarini. Sasa kujidai kukamata kitu kilichohifadhiwa na kuzuiliwa kihalali kabisa ni kushutukiza au ni usanii!.

Containers za Mitumba Kumbe Magari!.
Zile contena za magari zilizoandikwa mitumba, zote ziliwasili nchini toka mwaka jana, na zilipitishwa kwenye scanners na kuona kilichomo ndani ni tofauti na kilicho kuwa declared kwenye the bills of landing. Mmiliki wa mzigo huo ni Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju ambaye ameisha kamatwa siku nyingi, tangu Mwezi February, containers zake zikafunguliwa mbele yake, na yuko kwenye mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huo wa February kwa kosa la kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyoingizwa nchini kinyemela kama nguo za mtumba, na toka alipokamatwa hiyo tarehe 4 mpaka leo, bado hajafikishwa mahakani ili tuu kusubiria mpaka rais apate nafasi ya kuja kufanya ziara ya kushtukiza huku mhusika akiozoea jela!. Standard time ya mtu kufikishwa mahakamani ni 24 hrs! . Mtu kukamatwa tangu tarehe 4 February hadi leo bila kufikishwa mahakamani ili kutengeneza igizo la kukamatwa hizo containers!. Kisha rais anakuja, wanaweka seal nyingine na kufungua upya!.

Ni Mchanga Au Makinikia?
Scanners zimeishaonyesha ya mchanga, ambao jina lake halisi ni makinikia, containers hizo zilipokelewa bandarini siku nyingi nyuma ya marufuku ya rais kusafirisha mchanga nje, na process iliisha anza kabla ya katazo la rais, hivyo rais kuelezwa ni mzigo mpya, ni kumdanganya!. Yaani kila kitu kinajulikana, kisha rais wetu anaitwa kuja kushtukiza akiandamana na media, na kesho yake ndio headlines, hili ni igizo la ziara ya kushtukiza!, but very unfortunately kwa this time around, igizo la jana limebuma ku attract the much intended attention ya front page kwa sababu kulitokea tukio kubwa zaidi, more news worth kuliko igizo hili!.

Drama na Igizo za Ziara ya Kushtukiza.
Baada ya hayo kubainika, daily report ilionyesha lakini ikaamuliwa kusichukuliwe hatua zozote bali mkuu wa nchi aarifiwe kwanza, kisha ipangwe ziara ya kushtukiza halafu ndipo hayo yaonekane yamebainishwa na ziara hiyo ya kushtukiza ili ionekana kama ni ziara ya kushukiza ya rais ndio imebaini hayo!. Everything was a premeditated moves, but it was well staged kuonekana ni issue kubwa, lakini ndio hivyo tena, sometimes hata sterling kwenye movie huwa ana bugi step na hulazimika kufanya take two or take three!. Jana kwenye media Nape ndio alikuwa sterling!.

Shows za Ze Comedy.
Kumuita Mkuu wa nchi kufanya ziara za kushtukiza katika tukio lililopangwa na kisha kufungua zile seals za yale makontena mbele ya rais huku akishuhudia na ku act kushangaa, kuwa ndio wamebaini hayo magari ya kifahari, ili tuu kuuaminisha umma kuwa ni ziara hiyo imebainisha hayo, ni kupoteza muda wa thamani wa rais wetu. Hivi sio vitu vya kulisaidia taifa letu. Tusifanye vitu tuu ili watu waone!. Viongozi wetu wasitumie media kufanyia maonyesho ya maigizo ya utendaji kazi, au utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku!.

What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na mission wala vision ya ni nini vipaumbele vyetu, Tanzania kama nchi inayotaka maenddeleo ya kweli, tunatakiwa tujue ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndipo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio. Nchi inakabiliwa na sitofahamu nyingi, kuna kiongozi amefoji vyeti, kuna kiongozi amefanya tukio la uvamizi wa media, kuna waziri anatimiza wajibu wake kwa waledi, anatumbuliwa, na kutishiwa bastola, halafu mkuu wetu wa nchi anakwenda kufanya igizo ziara ya kushtukiza bandarini! .

Ushauri on A Way Forward and What to do.
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na wakala, lazima ziwe na mission na vision statements, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas maonesho na kuita media na kutoa maagizo kwa kusema tutafanya hiki au kile, lakini hatuoni, utekelezaji.

Mfano tunapo hubiri kuhusu Tanzania ya viwanda, where is the blue print ya Tanzania ya viwanda?, zenye smart objectives zenye malengo ya short term, medium term na long term strategies?. Ili tuwe na Tanzania ya viwanda tunahitaji land, where is the land set out kwa Tanzania ya Viwanda?. Tunahitaji labor, jee tumeishajua tutajenga viwanda gani vya vya kuzalisha nini ili hiyo mainpower na labor force kuvihudumia hivyo viwanda itayarishwe?. Tunahitaji capital ya kuanzisha hivyo viwanda, kuna strategies gani kuwawezesha Watanzania kuimiliki Tanzania ya Wiwanda, au tunataka kujenga Tanzania ya viwanda lakini viwanda ni vya wageni, vya Mchina, Mhindi na Mzungu?, na Mtanzania kuja kuwa ni kibarua tuu kwenye hiyo,Tanzania ya Viwanda kama ilivyo kwenye Uchumi wa Gesi?.

Tanzania ya viwanda itahitaji malighafi ya viwanda, uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo the biggest industries za Tanzania ya Viwanda zinapaswa kuwa ni agro processing industries, jee tuna mikakati gani ya kuinua sekta ya kilimo, ili izalishe malighafi ya viwanda?, au tunajenga Tanzania ya viwanda kama viwanda vya Bhakressa, vinatengeneza juces na unga wa ngano, lakini malighafi zote zinatoka nje!, hadi pulp ya mango juice tuna import, huku maembe ya Unyanyembe na Lushoto yakiozea mitini!. Tangu tumeanza kuhubiri wimbo wa Tanzania ya Viwanda, where is the blue print?, what is the plan?, tuko wapi, tumefanikisha nini? , tumekwama wapi and what is a way forward? .

Badala ya kuwahimiza ma bullies, impersonators, impostors na forgerist kuchapa kazi, tupewe matokeo ya hizo kazi zinazochwapwa, watu wanataka matokeo, na sio tuu kupokea maagizo na vitendo vya kuona sifa kutokelezea tuu kwenye TV huku wakitoa maagizo, na kuandikwa magazetini, sasa tujikite kwenye utendaji unaozingatia matokeo, na sifa zisiwe katika kutoa maagizo, bali ziwe katika matokeo ya utekelezaji wa maagizo hayo.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Hii issue ni ya lini? Ukiacha timing kuna hoja nzito sana hapa na inamlenga CEO wa Nchi.
Mkuu! This is the best of Pasco!
 
Hii issue ni ya lini? Ukiacha timing kuna hoja nzito sana hapa na inamlenga CEO wa Nchi.
Mkuu! This is the best of Pasco!
ALIKUWA, ILA KUNA KIPINDI ALICHANGE KIDOGO, akawa wa kusifia hata pasipostahili… KWA SASA ANGALAU ANAANZA KURUDIA HALI YAKE YA ZAMANI... Tusubiri tuone..

Ngali K
 
Hili bandiko kuhusu needs ya Tanzania kuwa na mifumo imara, bado liko valid, tungekuwa na mifumo imara, siku nyingi tungeisha baini kama Bunge ni dhaifu, haikuhitaji hadi CAG aseme Bunge ni dhaifu ndipo watu wafungue macho kuuangazia udhaifu wa Bunge letu.

Kwenye uzi huu nimesisitiza tujenge taasisi imara zenye strateg objectives ambazo ni SMART. Ukiwa na SMART Government, SMART Bunge na SMART Mahakama, humujitaji CAG kusema Bunge dhaifu bali utekelezaji wa Bunge ungeonekana very transparent na kama kuna udhaifu ungeonekana wazi na ni nani hivyo kama ni Spika anakuwa ejected automatically.

We seriously needs effective systems
P.
 
Back
Top Bottom