DOKEZO Kupata Leseni ya Biashara Manispaa ya Temeke ni Biashara pia ya watu, lazima utoe rushwa ndio upate huduma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Upatikanaji wa leseni za biashara katika manispaa ya Temeke umekuwa ni biashara kwa waliopewa majukumu hayo.

Kumekuwa na utengenezaji mkubwa wa mazingira ya rushwa ambao upo wazi kabisa na bila kutoa rushwa huwezi kupata leseni ya biashara bila kujali ni kuomba kwa mara ya kwanza au kurenew.

Mtu anapofika pale unaambiwa unahitajika kuwa na TIN Certificate, mkataba wa pango pamoja na tax clearance. Ukiwa huna chochote kati ya hivyo unaambiwa utoe hela ili wapitishe application yako.

Unaweza ukaenda na vitu vyote hivyo lakini utaambiwa "kwa sasa mfumo umebadilika hivyo kafanye application online au kama huwezi basi utoe chochote tukufanyie pamoja na kwamba hairuhusiwi" au ""ukitaka nikusaidie utanipa nusu ya hela ambayo utatakiwa kulipa kwenye service levy ili nipitishe bila service levy.

Ili kuweza kufanyiwa mchakato wa kupata leseni kwenye manispaa ya Temeke ni lazima ujiandae kutoa kati ya elfu 30 hadi 50.

Binafsi nimekwenda manispaa ya temeke kwa ajili ya kurenew leseni yangu mara tatu na siku ya tatu baada ya kuona ntaendelea kupoteza muda nimetoa sh elfu 30 ili niweze kupata huduma.
 
1690096382016.jpg

Maombi yote ya leseni yanafanywa kupitia mfumo wa tausi.tamisemi.go.tz na hakuna kufika ofisi za Halmashauri.

Kila kitu kipo humo ikiwemo control number.

Huko Halmashauri wanaweza kukusaidia tu namna ya kutuma maombi basi.
 
Back
Top Bottom