Kupanga ni kuchagua

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,803
Elimu ukiitumia vyema inakupa macho ya ubongo kuona sehemu ambayo wengine hawawezi kuiona ,Elimu ni kitu kizuri kuwa nayo ni fahari sababu inakupa hazina ya maarifa pamoja na aibu ya kutunza tabia na mwenendo wako bora kwa jamii inayokuzunguka .

Rosemary Wahu Kagwi ana degre ya Bsc Mathematics toka chuo kikuu cha University of Nairobi wakati huo huo ni mwanamusic mwenye tungo nzuri na zenye tija ,nacho penda toka kwa Wahu ni anatumia ubongo wake kutengeneza tungo nzuri na sio kutumia mwili wake kutengeneza video zenye mvuto.

David Mathenge a.k.a Nameless ndiye mwenye haki miliki ya mrembo huyu kwa lugha nzuri ndio mume wa huyu mrembo mwenye uzuri wa asili na mvuto ambao kwa pamoja wamebahatika kupata watoto wawili Tumiso aliyezaliwa mwaka 2006 na mdogo wake Nyakio aliyezaliwa mwaka 2013.

Nameless ana degree ya Architect toka chuo cha University of Nairobi na ni mwanamusic wa aina ya Pop na moja ya nyimbo yake bora ninayo ipenda ni Coming Home,hata kama umesoma unaweza kutumia karama yako unayoipenda kukuingizia kipato kuliko kufanya kazi usiyoipenda .Kazi bora na tamu ni ile unayoipenda na kuifanya kwa ubunifu na furaha.

Naandika post ya Wahuu huku nikimkumbuka Ray C ,watu walipenda ,nyimbo zake ,wakapenda shape yake na wakapenda mauno yake na yeye akachagua chaguo baya la wanaume na bahati mbaya hakuwa na elimu kichwani kwake,walipoanza kumchoka ,walimchoka yeye,mauno yake na tungo zake na kwa sasa anaishi kwa historia .

Ni kazi rahisi kumtekenya John Pombe na vigumu sana kupata A+ ya Hesabu kama huamini naomba niambie wewe O-level na A-Level pamoja na chuo hesabu ulipata ngapi?Better to be strong than pretty and useless.
GedsellianTz
 
Rosemary Wahu Kagwi ana degre ya Bsc Mathematics toka chuo kikuu cha University of Nairobi wakati huo huo ni mwanamusic mwenye tungo nzuri


Hapo kwenye Chuo kikuu cha University ndio kwenye umuhimu wa hii article.
 
Back
Top Bottom