Kuna kitu kimoja ambacho watu kama wewe hamuwezi kukielewa.
Ngoja nikupe scenario 2.
Umeitwa kwenye intavyuu moshi. Intavyuu inafanyika siku ya jumatatu. Sasa una option 2;
1. Upande basi Ubungo siku ya jumapili saa 12 asubuhi, (35,000) usafiri kutwa nzima ufike moshi saa 11 jioni. Ulale hotelini (30,000) uamke jumatatu uende kwenye intavyuu. Ulale moshi jumatatu, (30,000) uondoke jumanne asubuhi (35,000). Ushinde njiani ufike dar saa 2 usiku. Jumla = 130,000/- Muda masaa 60
2. Upande treni dar siku ya jumapili saa 10 jioni ukate ile ya ghali kabisa ya kulala (39,000) . Ufike moshi jumatatu saa moja asubuhi. Ujiandae uende kwenye intavyuu. Saa 10 jioni ukamate treni (39,000), saa mbili asubuhi jumanne uko dar unaendelea na shughuli zako. Jumla gharama = 78,000/- Muda masaa 36.