Kupanda madaraja: Adui wa staff development katika awamu ya Serikali ya tano

shafrael

Member
Feb 18, 2016
5
2
Mh. Rais, kwenye ualimu kuna program tunaita STAFF DEVELOPMENT. Kwamba kila mwaka kuwepo na utaratibu endelevu wa walimu kwenda kuendeleza taaluma zao ili kukuza ufanisi.

Huko nyuma walimu walikuwa wanaenda masomoni na bado madaraja yao yanapanda kama kawaida, lakini serikali yako imekuja na slogan ya kusema eti mwalimu akienda kusoma hapandishwi daraja.

Jambo hili limekatisha tamaa hata kwa tulioazimia kwenda kujiendeleza. Maana kama tunaona wenzetu walioenda kusoma hawajapandishwa madaraja wanaambiwa wasubir miaka mitano mbele lakini sisi tuliobaki tumepanda.

Tunapata picha kwamba, serikali hii ya uchumi wa kati, haina mikakati rafiki ya kuhamasisha walimu kuendeleza taaluma zao ili kujuza ufanisi.

Na pale inapobidi mwalimu kufanya hivyo anakuwa amerisk kupanda daraja kwa wakati au asipande kabisa.

Swali langu ni je, Mnawahamasisha vp walimu ambao wana elimu ya cheti, diploma au hata degree kwendeleza elimu zao ili kukuza ufanisi kwenye shule za serikali? Ifike mahali kama nchi iwe na mtaji wa wasomi wa ngazi za juu.
 
Hata ukienda kujiendeleza sasa hivi unajilipia mwenyewe miaka ya nyuma watumishi walikuwa wanasaidiwa fungu la kujiendeleza
 
na bado mnatumika kutenda dhambi ya wizi tena kwa kupora haki za watu! Adhabu yenu inafanana na hao wanaowatumia.
 
Back
Top Bottom