Dhuruma ya madaraja kwa walimu waliojiendeleza kielimu na kubadirishiwa muundo

Mwaisa1202

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
480
1,069
Hivi kwanini hili swala la walimu wakitoka kusoma na wakapeleka vyeti vyao sehemu husika na wakabadilishwa muundo huwa hauna impact kwenye mshahara wao.?

SANA SANA inapelekea kutopanda madaraja kwa wakati
Mfano wilaya ya kyela, Kibaha, ilala, Kisarawe n.k mwaka huu wote waliobadilishwa miundo mwaka 2021( wote waliopeleka barua 2019 na wale waliopeleka 2020 baada ya tamko la waziri Mohamed Mchengerwa kuwa WALIMU WOTE WALIOJIENDELEZA WABADILISHIWE MUUNDO bila kuathiri upandaji wa madaraja yao walibadilishwa muundo mwaka 2021).

Walimu wengi tulishawishika kuandika barua za kubadilishiwa muundo baada ya kauli ya waziri wa UTUMISHI kipindi kile (Mwaka 2020)

Mh. Waziri alisema kuwa tuliojiendeleza tubadilishiewe muundo na haita athiri madaraja yetu hivyo wale wanaostaili kupanda Mei 2023 watapanda bila tatizo.

Lakini imekuwa tofauti na kauli ya waziri kwani mwaka huu Mei hatujapanda madaraja eti kwa kigezo kuwa hatujatumikia hicho cheo cha muundo mpya kwa miaka mitatu.

Cheo ambacho akijaongeza hata senti tano kwenye mshahara isipokuwa kimebadilisha jina tu

Toka Mwalimu daraja A kwenda Mwalimu daraja B kwa wale wale walimu wa Grade A waliojiendeleza na kuhitimu diploma

Pia toka Mwalimu daraja B kwenda Mwalimu daraja C kwa wale walimu waliojiendeleza toka Diploma na kuhitimu Digrii.

lakini pia tulishapanda daraja toka mwaka 2019 Mei hivyo huu ni mwaka wa 4. Ila hatujapandishwa sababu tu kubadilishiwa muundo 2021.

Mbaya zaidi wengine walimaliza chuo miaka 6, 7, 8, hadi miaka 10 iliyopita ila TSC (Tume ya Utumishi wa Walimu) ndiyo hawakutimiza jukumu lao la kuwabadilisha muundo kwa wakati.

Isipokuwa wanavinzia karibia na kupanda daraja kwa Mwalimu husika ndiyo wanabadilisha muundo ili asipande daraja kwa wakati na kumfanya ajute kwanini ameenda chuo kuongeza ujuzi na maarifa katika fani yake ya ualimu.

Hiii inatuvunja moyo wa kusoma.. kwani wale tulioanza nao kazi wamesha tuzidi mishahara ingali sisi tumeongeza elimu, pia hata wanafunzi tuliowafundisha na wakaamua kuwa walimu ambao sasa tupo nao ofisi, wengi wao tunafanana nao mishahara na wengjne wametuzi hii inaumiza sana.

NAOMBA TUJIULIZE MAMBO YAFUATAYO.

1.JE, KUSOMA NI ADHABU au NI KOSA ?

2. JE, KWANINI AWABADILISHI KWA WAKATI MUUNDO PALE MWALIMU ANAPOOMBA KUFANYIWA HIVYO?

3. NA KAMA SHIDA NI BAJETI YA VIKAO NI KWANINI WASISUBIRI PINDI MWALIMU ANAPOPANDA DARAJA WALE WENYE KUSTAILI KUBADILISHIWA MUUNDO WABADILISHWE KIPINDI HICHO HICHO?

Yaani waue ndege wawili kwa Jiwe Moja (Muundo na daraja)

Kwa mfano unampandisha daraja mwezi MEI kisha unambadilisha muundo mwezi Juni kwa azimio lililofanywa kwenye kikao kimoja ili muundo usiathiri daraja lake maana hapa ataenda au atapanda sambamba na wenzake.

4.JE, AU NI MPANGO WA TSC KUTUGOMBANISHA WALIMU NA RAIS WETU MPENDWA (MAMA SAMIA SULUHU HASSAN)?

Kama LENGO ni hilo mmeshindwa walimu na Mama Samia ni damu damu.

Naomba sambaza kadri uwezavyo jambo hili liwafikie viongozi wa juu ili watusaidie kupata haki yetu.

NB: Kujiendeleza kielimu sio dhambi bali nikuongeza ujuzi na maarifa na kuleta ufanisi zaidi sehemu ya kazi.
 
Mnabaki kubwata tu hamna impact yoyote mpo kama mazezeta, Aya Sasa hawakupandishi mtafanyaje uharo nyie. Mioga kama ngiri
 
Kwa uelewa wangu huwa kupanda daraja na kubadilishiwa muundo zote ni promotion. Kupanda daraja ni promotion inayoongeza mshahara. Kubadilishiwa muudo hakuna impact kwenye mshahara. Kama ulitangulia kubadilishiwa muundo, tegemea kuchelewa kupandishwa daraja. What matters ilotakiwa ukomae kupandishwa daraja kwanza kabla ya kubadilishiwa muundo. Daraja=pesa, muundo=mbwembwe!
 
Ok

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
“TUME YA UTUMISHI WA WALIMU YAAGIZA UHAKIKI WA WALIMU WANAOSTAHILI KUPANDA MADARAJA" IMERUSHWA KATIKA KIPINDI CHA 'UTV' KINACHOITWA 'ALASIRI LOUNGE' LEO 5 JULAI 2023.
 
Tatizo la kusoma kupata vyeti kama Fashen lakini kwenye utendaji tija hakuna value addition.
 
Back
Top Bottom